We have 222 guests and no members online

unnamed

Ditha nyoni – RUVUMA

Raia nane kutoka nchi ya Ethiopia wamekutwa wamefariki katika kijiji cha Amani makolo taarafa ya kingonsera wilayani mbinga mkoani wa ruvuma   huku wengine 25 wakiwa hai wanashikiriwa na jeshi la polisi.

Posted On Tuesday, 16 May 2017 04:26

 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akiteta jambo na mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga eneo la Neema mara baada ya kukutana njiani wakati mbunge huyo alipokwenda kukagua kujionea athari zilizotokana na mvua kubwa iliyonyesha kulia ni Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CUF) Thobias Haule

Posted On Tuesday, 16 May 2017 04:17

opd

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISeMI akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali, Madaktari Bingwa, Viongozi wa Dini na Siasa katika Hospitali ya Mvumi.

Posted On Tuesday, 16 May 2017 04:12

Katika siku za karibuni, tumesikia habari kuhusu tishio la usalama wa watumiaji wa kompyuta za Windows. Tishio hili limekuja kutokana na kusambaa kwa minyoo inayobeba udukuzi wa ransomware. Udukuzi huu umeshambulia sehemu nyingi duniani (Tanzania, haswa dar es Salaam ni mojawapo), ila nchi zilizoathirika sana ni zile nchi zilizoendelea kwakuwa wao wamekuwa wakitegemea sana matumizi ya kompyuta kwenye kila shughuli. Kama ilivyo ada yetu, tukiwa kampuni inayoongoza kwa Website design na Website Hosting Tanzania, ambapo zote zinahusika na matumizi ya kompyuta, tunakuletea ufafanuzi wa kina utakaokuwezesha kufahamu kiundani udukuzi huu na jinsi ya kujikinga.

Idara zaidi ya 48 huko Uingereza, kampuni za FedEX, Telefonica, renault na Nissan ni mojawapo ya zilizoathirika na udukuzi huu, pia inasemekana Idara za serikali za Urusi na ATM nyingi China nazo zimekuwa wahanga wa shambulio hili, kiufupi kompyuta na seva zaidi ya 200,000 duniani kote zimeathiriwa hata kuppelekea baadhi ya nchi kama Uingereza kusitisha baadhi ya huduma za Afya kutokana na kompyuta kushambuliwa zaidi.

Ushambulizi huu umesababishwa na mfumo wa kuvamia kwa watumiaji wa kompyuta unaojulikana kama Ransomware. Ransomeware ni suhambulizi wa kompyuta kwa kumzuia mtumiaji kutumia kompyuta mpaka atakapofanya tukio linaloamrishwa na mvamizi Utekaji wa kompyuta(Compyuta kidnaping).

Wadukuzi wa The Shadow Brokers wameiiba programu hii kutoka Shirika la Usalama wa Marekani (NSA)  ambalo moja ya kazi zake ni kufuatilia na kuchunga usalama wa kimtandao. NSA hutumia programu hizi kudukua na kupata umiliki wa kompyuta za magaidi, lakini mwezi April programu hiyo iliibiwa. Wadukuzi hao waliamua kuiweka kwenye mtandao bure kwa lengo la kuonesha kutokukubaliana na raisi Dornald Trump. Wadukuzi wakaitumia program hiyo yenye kuweza kushambulia kompyuta zenye Windows, ushambulizi (exploit) ambao ulipewa jina la EternalBlue na kampuni ya Microsoft. Ushambulizi huu, hutumia minyoo (worms) na kutengeneza aina ya Ransomware inayojulikana kama WanaCrypt0r 2.0, Wanacry au Wanacrypt au Wcry ambao husambaza ransomware kwa njia ya email zenye mtego /kugushi (phishing) ambapo huonekana zinatoka kwa mtu mwenye nyadhifa (kama bosi wako)  kumbe sivyo.

Kama ilivyo matoleo mengine ya ransomware, Wannacry ransomware inatumia udhaifu uliopo kwenye kompyuta nyingi zinazotumia Windows. Shambulio hili jipya, limepelekea kampuni ya Microsoft inayotengeneza mitambo endeshi ya kopyuta (Operating Systems) aina ya Window kutoa kiraka (pacth) kwa ajili ya matoleo hata yale ya zamani (kama Window XP, Windows 7, Windows Server 2003 na mengine), hivyo kama bado haujaupdate Windows yako, wakati ni sasa kuziba kiraka.

Kiufupi, Wannacrypt husambazwa kwa njia ya Minyoo (Worm) kutoka kwenye kompyuta iliyoshambuliwa kwenda kwenye kompyuta nyingine yao yenyewe (automatically), kusambaa na udukuzi huu huwezeshwa kupitia udhaifu (Vulnerability) uliopo kwenye sehemu ya operating system ya windows (SMB file Sharing). Ingawa udhaifu huu ulishapatiwa kiraka na kutatuliwa kwenye kiraka kilichotolewa Mwezi wa tatu, lakini kuna watu wengi bado hawakuupdate, haswa wale wanaotumia Windows zisizo halali au zile za zamani kama XP, Windows 7 na nyinginezo.

Baada ya kushambuliwa, programu hii huzuia muhusika huambiwa mafaili yake yamefungwa (encryted) na hupewa siku ambapo unatakiwa kulipia la sivyo basi mafaili yatafutwa. Malipo hayo yanatakiwa kufanyika kwa njia ya pesa ya kidigitali (Bitcoin), muhusika hupewa utaratibu wa jinsi ya kukamilisha malipo ikiwemo anuani ya malipo.Kwa wasiofahamu, Biticoin ni aina ya pesa kwa njia ya dijitali ambayo huwezesha kutuma na kupokea pesa bila kujulikana (Annonymously).


Ransomware hufanya nini

Ransomware hutofautiana, lakini zote zinafanana kwenye kitu kimoja, humzuia mtumiaji kutumia kompyuta, Ransomware hukutaka kufanya kitu fulani kabla ya kukuacha kutumia kompyuta. Shambulio hili huathiri aina zote za PC za Windows zenye udhaifu (Vulrnerable), iwe ni kwa ajili ya binafsi, iwe seva nk.

Posted On Monday, 15 May 2017 10:18

media

Emmanuel Macron anatarajiwa kumteua waziri wake mkuu.

Posted On Monday, 15 May 2017 05:09

01

Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Yusufu Singo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya mbio ya Km 21 ya Dasani Marathon 2017  baada ya kuwakabidhi zawadi zao eneo la Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo. Mshindi wa kwanza, Augustine Sule (aliyesimama juu), Mshindi wa pili Stephano Huche (wa pili kushoto) na mshindi wa tatu Said Makula. Kushoto ni Nalaka Hettierachchi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza iliyodhamini mashindano hayo kupitia kinywaji cha maji ya Dasani. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)

Posted On Monday, 15 May 2017 05:05

unnamed

Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Mabodi pamoja na viongozi wengine wakipeleka  bati  kwa mafundi wanaoezeka msikiti wa ijitimahi.

Posted On Monday, 15 May 2017 05:04

tf3

Frank Mvungi-Maelezo

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefunga jumla ya machinjio 26 kati ya 55 zilizokaguliwa katika Mkoa wa Dar es Saalam kufuatia ukaguzi uliofanywa kati ya mei 2 hadi 12,2017 katika Manispaa za Kinondoni,Ilala,Ubungo na Temeke.

Posted On Monday, 15 May 2017 05:02

MAA1

Mkuu wa Shule ya St. Joseph Cathedral, Sista Theodora Faustine akimkabidhi zawadi na cheti, Prof. Rwekaza Mukandala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya kidato cha sita, ili ampatie mhitimu. Mahafali hayo yalifanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo. (Picha na Irene Bwire)

Posted On Monday, 15 May 2017 04:59

Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akikagua athari za mafuriko kwenye barabara ya Soni hadi Mombo ambapo imefungwa kutokana na vifusi,mawe kudondoka barabarani na hivyo kusababisha adha hiyo

Posted On Monday, 15 May 2017 04:52

Picha ya Maggid Mjengwa

Mwaka 1995 Hata Ben Mkapa Hakupata Meza Ya Kuwekea Sanduku La Kupigia Kura .. Alitumbukiza Kura Yake Kwa Kuinama...

Ndugu zangu,

Picha hii iko kwenye maktaba yangu. Pichani Ben Mkapa amezungukwa na familia ya wanahabari wenzake; namwona hapo dada yangu Anna, Kaka yangu Tido Mhando na kaka zangu na walimu wangu wengine wengi.
Naam, tumetoka mbali..!
Maggid,

Posted On Monday, 15 May 2017 04:51

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Daily News la February 12, 1985 linaripoti, kuwa Mwanamama Elizabeth Olotu anaandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kurusha ndege. Amerusha kutoka Dar kwenda Mafia na kurudi. Bakari Mwapachu, Mkurugenzi Mkuu wa ATC aliyekuwa abiria kwenye ndege hiyo aina ya Twin Otter alikuwa na haya ya kusema;

" Betty ametua ardhini kwa namna bora ambayo sijapata kuishuhudia kabla!" ( Kutoka maktaba ya Kwanza Jamii na Mjengwablog)

Je, hali ikoje leo?
Mbali ya mwenzetu Cecylia Gellejah tuna marubani wangapi wanawake?

Yuko wapi Elizabeth Olotu?

Maggid.

Posted On Monday, 15 May 2017 04:48

IMG_8743

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bw.  Edward Marks, akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya Benki yake kutimiza miaka 50, tukio lililofanyika Mjini Dodoma Jana usiku.

Posted On Sunday, 14 May 2017 05:55

media

Daktari anayeshughulikia ugonjwa wa Ebola katika shughuli zake za kitabibu Afrika Magharibu mwaka 2013

Posted On Sunday, 14 May 2017 05:26

Nimesoma, kuwa huko kuna Makumbusho yenye mengi ya kumbukumbu ya Tanganyika kama koloni la Mjerumani.
Ubaki salama uko na ukiweza tembelea makumbusho yenye historia ya Tanganyika.
Kila La Heri John!
Maggid.

Posted On Sunday, 14 May 2017 05:22
Page 4 of 1972

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi