We have 222 guests and no members online

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Yawezekana kuwa si wengi wenye kufahamu, kuwa panapoitwa leo Kimara Temboni miaka mingi iliyopita palikuwa ni mapito ya tembo kutoka Selous kupitia Kazimzumbwi, Kisarawe, na kuvuka hapo panapoitwa leo temboni kuelekea Sadani, Bagamoyo.

Watu walikuwa wakiwaona tembo wakipita mahali hapo na ndio maana wakapaita temboni.

Kama ilivyotokea kule UDOM, shughuli za mwanadamu ndizo zilizopelekea tembo waache kupita njia hiyo.

Lakini, kama wataalamu wanatwambia kuwa tembo ana kumbukumbu za ajabu na hawezi kusahau mapito yake hata kwa zaidi ya miaka 50, ndio kusema inaweza kutokea wakazi wa Kimara Temboni, asubuhi moja wanaweza kuamka na kuwakuta tembo wakiomba njia ya kupita kwenda au kurudi kutoka Saadani, Bagamoyo?

Maggid Mjengwa.

Posted On Sunday, 14 May 2017 05:18

unnamed

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye kofia katikati akizungumza jambo na Mwanaharakati wa kipindi cha Wanawake Live Joyce Kiri wa kwanza kulia , wakati wa ufunguzi wa semina ya vikundi vya wakina mama vya wanawake Live iliyofanyika Pugu jijini hapa.kushoto ni Diwani wa kata ya Pugu Henry Kilewo

Posted On Sunday, 14 May 2017 05:16

TIB1

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na watumishi wa wizara hiyo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi na kuwataka waongeze jitihada za makusanyo ya kodi ya pango la ardhi.

Posted On Sunday, 14 May 2017 05:14

SERENGETI-BOYS-1

Siku chache baada ya DStv kutangaza kuwa itarusha moja kwa moja (Mubashara) Michuano ya vijana ya AFCON itakayoanza kesho huko Gabon, habari mpya na njema zinasema sasa DStv itarusha mechi zote za Serengeti boys katika michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili.

Posted On Sunday, 14 May 2017 05:10

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa

Posted On Saturday, 13 May 2017 05:18

Posted On Saturday, 13 May 2017 05:17

unnamed

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na wadau wa michezo wakati wa uwekaji saini wa msaada wa fedha wa Shillingi Bilioni 2.1 baina ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kulia ni Rais wa TFF Jamal Malinzi na Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji  wa SBL Bibi. Helene Weesie.

Posted On Saturday, 13 May 2017 05:16

Posted On Saturday, 13 May 2017 05:15

Picha ya Maggid Mjengwa

Rungwe ni Banana Republic. Wenyeji wakarimu. Wamenikarimu Mikungu ya ndizi.

Posted On Saturday, 13 May 2017 05:14

Picha ya Maggid Mjengwa

Na Tukuyu hakuna wa kufa njaa..!
Ukikosa wali nyama, au kwa maharage, chemsha njugu mawe. Ndoo nzima elfu tano.
Sokoni kuna mpaka ndizi za kuokota.
Tatizo la dada muuzaji huyu alikuwa akinisemesha kwa kuchanganya Kiswahili na Kinyakyusa. Muda wote akidhani mimi ni Mnyakyusa. Sasa sijui Mwenyekiti wenu nimekaa kinyakyusanyakyusa..?!

Posted On Saturday, 13 May 2017 05:11

Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo, wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio. Kutoka kushoto ni Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nitesh Patel.

Posted On Saturday, 13 May 2017 05:07

Picha ya Maggid Mjengwa

Ukiamka mapema asubuhi unaona mandhari nzuri ya mji.

Posted On Friday, 12 May 2017 07:05

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Majuzi hapa nilifika Mbinga na kwenye Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi, Mbinga.

Posted On Friday, 12 May 2017 07:03

UF3A1002

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mheshimia Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ametembelea Zahanati ya Solwa iliyopo katika kijiji cha Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoa wa Shinyanga kisha kutoa msaada wa viti vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama,vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia na viti vya wagonjwa (wheel chairs) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.

Posted On Friday, 12 May 2017 06:59
Page 5 of 1972

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi