We have 248 guests and no members online

Watumishi

Ndo mana a'ke. Jibu ni hilo kwa kimoja kati ya viwili hivyo, na hasa ukiwa nyumbani kwa mwenyekiti!
Naam, wanadamu tupendane. Tukigombana tupatane. Hata mbwa na paka wanatufundisha hilo. Kwamba umoja ni nguvu. Miongoni mwetu wanadamu kuna wenye hulka za kuchonganisha wanadamu wenzao. Kwa majungu yao. Kwa fitina zao. Ni kama panya, aliye tayari kumfitini paka kwa mbwa. Na mnajua kwanini.
Shukran ya picha ni kwa Mary Kisinga.
Maggid,
Iringa.

 

Posted On Monday, 14 August 2017 19:33

Image may contain: 3 people, people smiling

Pichani ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi Asia Abdallah, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mama Masenza kwenye tukio la uzinduzi wa TTCL 4 G Lte, Iringa, leo asubuhi. Kulia ni DC wa Iringa, Ndugu Richard Kasesela.

Maggid, 

Iringa.

 

Posted On Monday, 14 August 2017 19:28

Image may contain: 2 people

Ndugu zangu,

Pichani ni Mtendaji Mkuu wa TTCL, Ndugu Wazir Kindamba. Pichani akitoa hotuba yake kuzindua TTCL 4 G Lte, kwenye viwanja vya Posta, Iringa, leo asubuhi.

Waziri Kindamba ni CEO Mzalendo kwa maana ya neno mzalendo. Ana usongo na maendeleo ya nchi kwenye eneo la mawasiliano.
Ni mjumbe wangu kwenye jukwaa letu hili. Asubuhi aliniambia kwa simu;

" Mwenyekiti nazindua TTCl 4 G kwenye mji wako!"

Nami nikamjibu;

" Simtumi mtoto, nakuja mwenyewe kushuhudia!"

Nikaahirisha ratiba zangu za asubuhi ya leo. Nikabeba kamera yangu hadi viwanja vya TTCl, pale maeneo ya Posta , Iringa.

Nikawa mwanahabari wa kwanza kuripoti kwenye tukio la kihistoria kwenye mkoa wetu wa Iringa.

Asanteni sana TTCL. Ni Shirika letu Watanzania kwa asilimia mia moja, Shime tuliunge mkono.

Maggid,

Iringa.

Posted On Monday, 14 August 2017 19:24

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwakabidhi bendera ya taifa askari kumi (10) waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.

Posted On Monday, 14 August 2017 06:24

Police are seen on a street following an attack by gunmen on a restaurant in Ouagadougou, Burkina Faso

Polisi wakiwa na gari lisilopenya risasi walifika eneo hilo kukabiliana na washambuliaji

Watu 17 wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa katikati ya mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, serikali ya nchi hiyo imesema.

Posted On Monday, 14 August 2017 06:20

media

Raila Odinga akiwa katika mtaa wa Kibera jijini Nairobi, Agosti 13 2017

Posted On Monday, 14 August 2017 06:18

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mke wake Mary wakimjulia hali Mbunge wa Viti maalumu CCM Mkoa wa Kigoma  Mheshimiwa Josephine Ngezabuka .ambaye amelazwa kwa matibabu katika Hosptali ya Muhimbili (MOI) Baada yakupata ajali hivi karibuni Mkoani Kigoma. katikati mwenye miwani ni Naibu spika Dkt. Tulia Akson.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Posted On Monday, 14 August 2017 06:15

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano ambazo kati ya nyumba 10 zilizojengwa na NHC, nyumba saba zimeishanunuliwa.

Posted On Monday, 14 August 2017 06:12

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole (wa pili kushoto) akiongoza nyimbo ya hamasa mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana kuwasili  kufunga  mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa  CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma

Posted On Monday, 14 August 2017 06:07

IMG-20170813-WA0062

Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka ,mwenye suti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja baada ya misa kwenye kanisa la KKKT Tumbi Kibaha. bPicha na Mwamvua Mwinyi

Posted On Monday, 14 August 2017 06:04

DSC_5433

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir (kushoto) mara alipowasili katika Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo,

Posted On Monday, 14 August 2017 06:02

Image may contain: 1 person, standing and suit

Mimi nina imani na Karia. Nina imani atausukuma mpira wetu upae juu na utue mbele zaidi. 

Mimi najua, kwa mifano, kuwa Karia ni mtu anayetaka ubora. Nasi tunataka soka letu liwe Bora. 

Wallace Karia ni chaguo sahihi. Walioshindwa, kwa vile nao ni wanafamilia ya soka, waungane na Karia kwenye kuutafuta ubora wa mpira wetu.

Kila La Heri Wallace Karia.

Maggid Mjengwa, 

Iringa.

Posted On Sunday, 13 August 2017 11:39

Image may contain: 4 people, people standing, beard, outdoor and nature

Image may contain: tree, outdoor and nature

Image may contain: 1 person, smiling, standing, child, outdoor and nature

Image may contain: 2 people, people standing and outdoor

Image may contain: 6 people, child and outdoor

 

Ndugu zangu,

Februari 20, 2016 nilifanya moja ya safari muhimu kupata kuzifanya maishani mwangu nikiwa na makamanda wangu, Manfred na Gustav.

Tuliianza safari alfajiri kutoka Iringa Mjini kwenda Pawaga ambako kulikuwa na wananchi walioathirika na mafuriko na waliohitaji msaada.

Vijana wangu walishiriki kuhamasisha kukusanya misaada. Tukapata vingi muhimu ikiwamo mahema.

Nakumbuka ulikuwa msimu wa masika. Barabara ilikuwa mbaya kwenye sehemu nyingi. Kilomita 87 tulitumia saa tatu.

Tulipofika Kimande, Pawaga, tulipokewa na Mtendaji wa Kata ya Mlenge.

Tulianza na kupokea taarifa ya msiba wa mwanakijiji wa Kisinga aliyefariki akihofiwa kufa kwa kipindupindu. Niliongozana na Mtendaji Kata, Sarah Mbilinyi hadi kituo cha polisi Pawaga, maana, alitoka Kisinga, kilomita 14 kutoka Kimande ili akatoe taarifa ya kifo hicho kwa vile aliyekufa alifia shambani.

Pale polisi tulikutana na Kaimu Mkuu wa kituo, alijitambulisha kwangu kama Detective Jafar. Naye alikuwa msomaji wa makala zangu Raia Mwema!

Ili ufike kituo cha polisi ni lazima upite kwenye kituo cha afya na ilipokuwa kambi ya wagonjwa wa kipindupindu.

Kisha tukaongozana na mtendaji Sarah Mbilinyi hadi kijijini Kisinga ambako kulikuwa na kambi ya wahanga walioathirika na mafuriko yaliyosomba kitongoji chao cha Kilala.

Ni kilomita 14 hivi kutoka Kimande. Kuna mito miwili ya kuvuka. Tukapewa taarifa kuwa mto mmoja jana yake ulijaa na magari yalishindwa kuvuka. Kulikuwa na korongo la Luhapula ambalo nilikuwa sijapata kuliona maishani, nalo lilitisha sana . Tulivuka salama tukafika Kisinga majira ya saa 4 asubuhi.

Hapo kukawa na taarifa ya msiba mwingine. Misiba miwili kwa siku moja. Ziara iliendelea na Mtendaji Kata alifanya kazi njema ya kutupitisha maeneo mbalimbali kukagua hali halisi ikiwa ni pamoja na kunikutanisha mimi na wahanga.

Kwa muda wote huo vijana wangu walikuwa karibu nami wakiwa tayari kusaidia. Tulipofika kambini ndipo vijana wangu nao wakaanza kazi ya kusaidia ikiwamo kushusha mizigo na kuwafariji watoto wenzao kwa michezo.

Kama wazazi, tuna wajibu pia wa kuwashirikisha watoto wetu kwenye masuala ya kijamii ikiwamo kazi za kijamii kila inapowezekana. Wana mengi wanayojifunza na kupata uzoefu nayo.

Adia, Msanii Oliver Ngoma..https://www.youtube.com/watch?v=fZ8LUQgbKz0

Maggid, 
Iringa.

Posted On Sunday, 13 August 2017 11:36

Image may contain: 1 person, sittingNdugu zangu, 

Miaka ile ya 90 mwanzoni, Michael Jackson alikuja Tanzania na alifikia pale Hoteli ya Kilimanjaro. 

Jioni moja, Michael Jackson alishangazwa sana kutembelewa na Rais wa Jamhuri aliyeonekana yuko ' simple' sana. Mzee Mwinyi alipiga stori na Michael Jackson na kumkaribisha Tanzania kwa kuona vivutio vyake pia. 

Inasimuliwa, kuwa jioni ile pale Kilimanjaro Hotel, Michael Jackson alisikia kelele za watu wakiimba nje ya hotel . Kwa vile tangu akitua Uwanja wa Ndege hakukuta mashabiki wake waliofika kumpokea, basi, Michael Jackson akadhani muda huo ndipo mashabiki wake wa Tanzania wamepata habari na wamekuja hotelini kumshuhudia.

Michael Jackson akaambiwa na wenyeji; 

" Hao ni washabiki wa klabu ya Simba, timu yao imeshinda mechi muhimu. Muda huu wametembea kwa miguu wakiimba wakitokea National Stadium. Wanaelekea kupanda Pantoni kwenda Kigamboni!

Naam, ziara ya Michael Jackson ilifahamika zaidi kwa wanahabari, lakini si kwa raia wa Jamhuri ambao, kwa wakati huo, hata televisheni hazikiwepo. 

Na hakika, ziara ile ya Michael Jackson haikuifikia ile ya bondia Muhammad Ali aliyepata mapokezi makubwa tangu alipotua uwanja wa ndege!

Mohammed Ali alikuwa maarufu mno. Ingawa hivyo, Michael Jackson alivutiwa sana na Nchi ya Tanzania, na bila shaka, lugha ya Kiswahili, maana, kwenye moja ya tungo zake amepata kukitumia.

Liberian Girl, Nakupenda Piya, Nakutaka Piya, Mpenzi Wee!

https://www.youtube.com/watch?v=Tm2BsOnAYcM

Maggid,
Iringa.

Posted On Sunday, 13 August 2017 11:32

Image may contain: outdoor and nature

 Picha hii niliipiga Mikumi, 2009.

Maggid.

Posted On Sunday, 13 August 2017 11:30
Page 6 of 2026

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi