We have 166 guests and no members online

Znateli

Image result for LWANDAMILA

Baada ya mchezo wa hapo jana dhidi ya St Louis ya Shelisheli, Kocha wa Yanga, George Lwandamina amekubali kuwa kikosi chake hakikucheza vizuri kama walivyotarahia. Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Washelisheli hao katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Posted On Sunday, 11 February 2018 02:48

Tokeo la picha la epl

Hapo jana January 31, 2018 ilishuhudiwa michezo kadhaa katika ligi ya Uingereza (EPL)

Mechi kubwa ilikuwa ni kati ya Tottenham dhidi ya Manchester United mchezo uliomalizika kwa Tottenham kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Michezo mingine ilikuwa kama ifuatavyo;

                       Chelsea 0-3 Bournemouth

                       Everton 2-1 Leicester City

                       Southampton 1-1 Brighton and Hove Albion

                      Manchester City 3-0 West Bromwich Albion

                       Stoke City 0-0 Watford

Baada ya michezo hiyo huu msimamo wa ligi kuu uko hivi;

Posted On Thursday, 01 February 2018 05:10

Tokeo la picha la AUBAMEYANG

Mshambuliaji wa klabu ya Borrussia Dortmund ya Ujerumani raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang leo ametia saini mkataba wa muda mrefu kuichezea klabu ya Arsenal.

The Gunners waliwasilisha maombi mawili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambayo yalikataliwa na Dortmund kabla ya kukubali dau la juu ya £46.5m walilomsajilia Alexandre Lacazette.

Klabu ya Arsenal imeandika kwenye mtandao wao kwamba Aubameyang ni Mchezaji wao wa pili kumnunua katika kipindi cha kuhama wachezaji mwezi Januari.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 13:10

Tokeo la picha la juma nyosoMkurugenzi wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema sakata la Juma Nyoso kumpiga shabiki wanaliacha chini kamati ya nidhamu ambayo mpaka sasa bado inaendelea na uchunguzi ili kutolea uamuzi wa mwisho.

Posted On Sunday, 28 January 2018 03:34

Mshambuliaji wa Stoke na Uingereza Peter Crouch, 36, analengwa kusajiliwa na Chelsea baada ya majeruhi kumnyima Andy Carroll , 29, fursa ya kuhamia klabu hiyo.(Telegraph)

Mshambuliaji wa Stoke na Uingereza Peter Crouch, 36, analengwa kusajiliwa na Chelsea baada ya majeruhi kumnyima Andy Carroll , 29, fursa ya kuhamia klabu hiyo.(Telegraph)

Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 31, na beki wa Itali Emerson Palmieri, 23, kutoka Roma. Wawili hao wanaweza kugharimu jumla ya £77m. (Daily Star)

Chelsea itamtumia mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 kumsajili Edin Dzeko. (Sky Italia)

Kipa wa Manchester United David De Gea, 27, anasema kuwa katika klabu hiyo ni kitu maalum .Raia huyo wa Uhispania alitaka kuzima uvumi ambao umekuwa ukisambaa kuhusu hatma yake katika uwanja wa Old Trafford.(ESPN)

Posted On Friday, 19 January 2018 15:58

Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi kocha wake Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre pamoja na Kocha wa viungo, Aimen Habibi ambapo leo wamesaini mkataba na klabu hiyo. 

Akizungumza baada ya kusaini mkataba na klabu ya Simba, Lechantre amesema Simba iko vizuri ila inatakiwa kuimarika na kwamba ndiyo sababu ya yeye kufanya kazi na klabu hiyo, huku akiwaahidi wanachama wa Simba ushindi.

Posted On Friday, 19 January 2018 15:47

Pierre-Emerick Aubameyang

Pierre-Emerick Aubameyang

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ''alitukosea heshima'' kwa kuzungumza hadharani kuhusu mchezaji Pierre-Emerick Aubameyang, amesema mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorc.

Arsenal ina hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Gabon kwa dau la £60m.

Siku ya Alhamisi , Wenger alisema kuwa Aubameyang atafaa sana Arsenal , matamshi ambayo hayakuifurahisha klabu ya Dortmund.

''Tunahisi kwamba ni kukosa heshima kwa Wenger kuzungumzia kuhusu wachezaji wa klabu nyengine'', alisema Zorc.

Posted On Thursday, 18 January 2018 17:04

Klabu ya Simba leo imemtangaza rasmi kocha wake mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lechantre.

Taarifa ya Msemaji wa Simba, Haji Manara imeeleza kocha Lechantre ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma.

“Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kwamba imempata kocha wake Mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lechantre. Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

“Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Afrika 2000. Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 ba pia barani Asia mwaka 2012. Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi.” imeeleza taarifa hiyo.

Posted On Thursday, 18 January 2018 16:50

Sanchez

Mkataba wa Manchester United kumsaini mshambualiaji wa Arsenal raia wa Chile utagharimu pauni milioni 180 baada ya Sanchez kukubali mkataba wa miaka minne unusu. (Telegraph)

Mkataba wa Sanchez na Manchester United utamlipa mchezaji huyo wa umri wa miaka 29, paunia 400,000 kwa wiki. (Independent)

Posted On Thursday, 18 January 2018 16:40

Ronadinho astaafu kucheza soka

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu za PSG, Barcelona na Ac Milan Ronaldo de Assis Moreira Maarufu kama Ronadinho Gaucho amestaafu soka.

Licha ya Ronadinho kutocheza soka la kiushindani toka mwaka 2015 amekuwa akicheza michezo ya mabonanza

Kaka na wakala wa mchezaji huyo Roberto Assis amethibitisha kuwa umefika mwisho kwa fundi huyo wa Brazil kucheza soka.

Posted On Wednesday, 17 January 2018 09:06
Alexis Sanchez

Manchester United wana nafasi nzuri sana ya kumnunua Alexis Sanchez kutoka kwa klabu yake ya Arsenal.

Hii ni baada ya habari kuibuka kwamba wako tayari kulipa £35m, ambazo ndizo pesa ambazo Arsenal wamekuwa wakitaka kulipwa kumwachilia.

Posted On Tuesday, 16 January 2018 08:29

Image result for Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Na.Paschal Dotto-MAELEZO

SERIKALI ya Awamu ya Tano kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imewashauri wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kuweza kugundulika mapema iwapo wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Posted On Saturday, 30 September 2017 08:42
Page 1 of 196

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu