We have 152 guests and no members online

Simu

Tokeo la picha la kingunge ngombale mwiru

Mwanasiasa mkongwe Tanzania amabaye pia alikuwa ni mmoja wa viongozi wa muda mrefu na mwenye ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale-Mwiru, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo ijumaa ya Februari 2. Kifo cha mwanasiasa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 87, kimetokea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Posted On Friday, 02 February 2018 04:18

Kwa mara ya kwanza tangu kurejea nchini Tanzania, balozi mteule Dkt Wilbroad Slaa amekutana na kufanya mazungumzo na rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao na Rais, Dkt Slaa amesema ameamua kukubali kufanya kazi na Rais baada ya kuridhika na kazi kubwa inayofanywa na Rais kwa wananchi.

Posted On Monday, 29 January 2018 13:04

Tokeo la picha la fire break in langata nairobi

Watu wanne wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya moto uliotokea usiku wa kuamkia leo January 29 katika mtaa wa Kijiji eneo la Langata-Nairobi, huku wengine wakiripotiwa kukesha baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa moto.

Kwa mujibu wa Maafisa wa serikali nchini humo, nyumba 6,000 makazi ya watu karibu 14,000 ziliharibiwa na moto huo.

Posted On Monday, 29 January 2018 12:06

Meli iliyokuwa na manusura (L) na meli ya uokozi katika bahari ya Pacific. Januari. 28, 2018.

Kikosi cha anga cha New Zealand kimewagundua Jumla ya watu sita akiwemo mtoto mmoja, waliokutwa wakiwa hawajitambui baada ya kuelea kwenye maji zaidi ya wiki moja katika boti ndogo ya mbao katika bahari ya Pacific.

Posted On Sunday, 28 January 2018 22:03

Deutschland | Polizei löst Kurden-Demo in Köln

Chanzo, DW.

Jeshi la Polisi nchini Ujerumani limewatawanya  waandamanaji takribani 15,000 wa kikurdi waliokuwa wamebeba mabango yanayoonesha  nembo  za  chama  cha  wafanyakazi wa  Kikurdi PKK, zilizopigwa marufuku  nchini  humo.

Posted On Sunday, 28 January 2018 12:59

Tokeo la picha la Deadly blast rocks Kabul

Watu 95 wamepoteza maisha na wengine 158 kujeruhiwa katika shambulio la kubwa la kigaidi katika mji mkuu wa Afghanistan -Kabul.

Kundi la kigaidi la Taliban limehusishwa kutekeleza shambulio hilo ambalo ni la tatu kutokea katika kipindi cha muda wa siku saba zilizopita.

Posted On Saturday, 27 January 2018 16:48

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Diwani kata ya Yaeda Chini (CCM) Bryson, wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga

Posted On Friday, 26 January 2018 06:22

CD

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Seleman Jafo akipokea taarifa za maendeleo ya ujenzi wa madarasa shule ya msingi Chang’ombe ‘’A ‘’kutoka kwa Afisa mteule daraja la -I-  ambaye ni Fundi mkuu kutoka (JKT) Aluleyani Mapunda wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa shule ya msingi  hiyo unaofanywa katika kata ya Chang’ombe mjini Dodoma.

CD 1

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Seleman Jafo akitoa shukrani zake za dhati baada ya kuridhishwa na utendaji wa kazi ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Chang’ombe A na ukarabati wa majengo ya shule wakati wa ziara aliyoifanya katika shule hiyo

CD 2

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)  Selemani Jafo akiwa na mwanafunzi George John wa darasa la saba ambaye ni mlemavu  na kutoa agizo kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma  Godwin Kunambi,kuhakikisha mradi wa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi Shule ya Msingi Chang’ombe A unazingatia miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wa ulemavu wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.

CD 4

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo akipokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma  Godwin  Kunambi juu ya ukamilifu wa ujenzi wa choo cha walimu shule ya msingi Chang’ombe ‘B’ pia uendelevu wa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi  katika ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.

CD 3

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo akitoka kukagua ujenzi wa choo cha walimu katika shule ya msingi Chang’ombe ‘B’ wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe

CD 5

Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI) Selemani Jafo  akimalizia ziara yake kwa kukagua miundo mbinu ya majitaka katika shule ya msingi Chadulu.

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda kuanza shule huku akiwasisitiza wazazi watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto hao wachukuliwe hatua za kisheria.

Jafo ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali katika shule za msingi, Chadulu, Chang’ombe A na B, Manispaa ya Dodoma.

Katika ziara yake ya kukagua maagizo aliyoyatoa kwenye shule hizo kuhusu masuala ya miundombinu, Jafo amesema  “Sisi kama serikali hatutaki mtoto akose elimu hasa katika kipindi hichi ambacho serikali imeamua kuelekeza nguvu za kutosha kwenye elimu kwa ajili ya watanzania.”

Ameongeza “Kwa mzazi ambaye mtoto wake atabainika hajaenda shule na kupewa kazi zingine kama kuendesha bodaboda hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,”.

 Pamoja na hayo, Jafo amekemea tabia ya wazazi kutotilia mkazo masuala ya elimu na kuwakabidhi watoto wao kuendesha bodaboda kama ajira yao badala ya kuwapeleka shule na kuwataka kuhakikisha wanawanunulia mahitaji yote ya shule.

Aidha amesema serikali haitarajii kuna vijana waliochaguliwa wakishawishiwa na wazazi kufanya vibaya kwenye mitihani kutokana na elimu kuwa ni bure.

Akizungumzia kuhusu watoto walioandikishwa kuanza kusoma elimu ya awali na msingi, Jafo amesema kumekuwepo na mwitikio mkubwa katika suala la uandikishaji watoto hao na linatokana na uwepo wa elimu bure.

Hata hivyo, amesema shule nyingi idadi ya wanafunzi imeongezeka zaidi na kwa serikali ni faraja kuona watanzania wengi sasa wanapata elimu huku akiwataka wazazi wahakikishe watoto walioandikishwa wanahudhuria shule ipasavyo  na wakurugenzi kuendelea kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

Kadhalika, Jafo ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu mbalimbali kwenye shule hizo huku akiwaahidi walimu kuwa serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, amesema kwasasa Manispaa hiyo inaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja ujenzi wa shule za msingi na sekondari na kuongeza madarasa kwenye baadhi ya shule ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi hasa wanaohamia Dodoma.

 Kwa upande wake, Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Scholastika Kapinga, amesema hadi sasa watoto zaidi ya 8,000 wameandikishwa kwenye manispaa hiyo kuanza kusoma elimu ya awali na msingi.(P.T)

Posted On Thursday, 12 January 2017 06:15

Posted On Sunday, 27 November 2016 03:18

langa

Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Kongo- Brazzaville, Langa Lesse Bercy ameshindwa kuwasili Cairo, Misri kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi juu ya umri wake kama alivyotakiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimkatia Rufaa CAF Langa Lesse Bercy baada ya kujiridhisha amevuka umri wa kucheza mashindano ya U-17.

Na hiyo ilifuatia Kongo- Brazzaville kuitoa Tanzania, Serengeti Boys katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania fainali za U-17 Afrika mwakani nchini Madagascar.

Kutokana na rufaa hiyo, Langa Lesse Bercy alitakiwa na CAF kufika makao makuu ya shirikisho hilo, Cairo, Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).
Na TFF ilikubali sharti la CAF kugharamia zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake  pamoja na kulipia gharama za vipimo.

Wakati zoezi la vipimo limepangwa kufanyika leo, Shirikisho la Soka la Kongo- Brazzaville limetoa taarifa kwamba Langa Lesse Bercy hataweza kutokea kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wao.
Zoezi limepangwa kufanyika leo kuanzia Saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.

Na jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko “vitani”,eneo hilo halikutajwa.
Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari leo, imesema kwamba wanaendelea kufuatilia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .(P.T)

Posted On Saturday, 19 November 2016 14:06

IMG_4116

Katika kusaidia uboreshwaji wa elimu ya Tanzania, Shirika la Kimataifa la ActionAid kwa kushirikiana na serikali ya Norway kupitia Wakala wa Maendeleo na Ushirikiano (NORAD) wamezindua mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).

Akielezea kuhusu mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama alisema mradi huo unataraji kusaidia uboreshwa wa elimu nchini na zaidi maeneo ya vijijini sehemu ambapo zimekuwa zikionekana kuwa nyuma kielemu.

Alisema ili kupatikana kwa elimu bora kunahitajika uwekezaji wa kuboresha elimu kwa maeneo yote yanayohusika na elimu na inatakiwa kuanza na elimu ya shule ya msingi ili kuweza kumwandaa mwanafunzi kuanzia akiwa mdogo kwa kupata elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.

“Elimu bora inataka kuwepo kwa uwekezaji kuanzia kwenye shule za msingi kwa kila jambo kama ni uniform, kalamu, uji, walimu kupatiwa stahiki zao na mengine yote yatimizwe,

“Ukitaka elimu bora lazima ujue inahitaji uwekezaji na mradi huu unataka kuongeza fursa kwa wanafunzi kwa kuanzia shule za msingi na zaidi tunaangalia vijijini,” alisema Dkt. Lwaitama.

Nae mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo, Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad alisema Norway na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na ana furaha kuona mradi huo unafanyika kwa maendeleo ya baadae ya Tanzania.

Alisema Norway itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya elimu nchini katika kusaidia vijana kupata elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vya ufundi ili kuweza kuongeza wasomi ambao watasaidia ukuaji wa uchumi nchini.

“Nina furaha kuona mradi ambao utakuwa na mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sasa na baadae kwa Tanzania ninataraji kuona miradi inafanikiwa na ushirikiano wa Norway na Tanzania kwa miaka 50 sasa unazidi kuimarika na Tanzania inaushirikiano mzuri na Norway,” alisema Kaarstad.

Kwa upande wa Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu alisema kupitia Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 11 (2) inaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kujielimisha na kusoma ngazi zote za elimu hadi anapoamua kuacha kuendelea kusoma na hivyo mradi huo utasaidia watanzania kupata haki yao ya kikatiba.

Mradi huo unataraji kufanyika katika wilaya za Kilwa na Singida na utakuwa wa miaka mitatu ambao unataraji kuzifikia shule 60, 30 kwa kila wilaya.

Aidha unataraji kuwafikia wanafunzi wa kiume 7,758 na wakike 8,474 kwa wilaya ya Singida na Kilwa kuwafikia wanafunzi wa kiume 6,607 na wakike 6,546 lakini pia walimu 287 kwa Singida na 290 kwa Kilwa.

IMG_3912

Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).(Picha na Modewjiblog).

IMG_3943

Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).(P.T)

Posted On Friday, 26 February 2016 07:51

Msemaji wa chama cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Bujumbura.

 

Patrice Gahungu wa chama cha Union for Peace and Development aliuawa alipokuwa akiendesha gari kwenda nyumbani kwake siku ya jumatatu usiku.

Kiongozi wa chama hicho Zedi Feruzi naye aliuawa kwa kupigwa risasi mwezi Mei wakati wa maandamano ya kumpinga rais Pierre Nkurunziza.

Watu wengine wawili waliuliwa hapo jana mjini Bujumbura lakini polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

Maandamano hayo yaliitishwa na upinzani kupinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Watu kadha wameuawa na maelfu ya wangine wameikimbia nchi hiyo tangu kuzuka kwa mzozo mwezi Aprili. BBC, A.I

 

Posted On Tuesday, 08 September 2015 12:26
Page 1 of 5

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli