We have 102 guests and no members online

Znateli
×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

Katika dunia hii ya utandawazi, ushindani ni kitu kisichoepukika. Haijarishi wewe unafanya biashara ya kuuza peni au una blogu yako au hata unauza dhahabu. Utandawazi umeweza kuwafanya wanunuzi wawe na sauti na machaguo mengi toka kila pande, pande hizi zinaweza kuwa hata nje ya mipaka ya nchi. Pia, wanunuzi wamepewa uwanja mkubwa wa kuijadili na kupata taarifa za biashara yako kwa urahisi zaidi, mitandao jamii ni moja ya kitendea kazi kwenye hili.

Ingawa ushindani ni mkubwa sanasana, lakini leo hii, kama utatembelea kwenye biashara kadhaa nchini Tanzania, utakubaliana na mimi kuwa, wengi tunafanya biashara kwa mazoea (business as usual)na ubunifu umekuwa mdogo sana kwa makampuni mengi sana. Iwe ya serikali au hata ya watu binafsi, iwe madogo yaliyoanza jana au hata yale yenye umri wa miongo.

Posted On Monday, 01 September 2014 12:00

website Design & Hosting in Tanzania

Siku hizi ni kitu cha kawaida kuona vitu vya ajabu vikitumwa tokea akaunti ya mtu unayemuamini sana na haukutegemea kama mtu kama yeye angeweza kutuma (post) vitu kama hivyo, na ikakufanya hata utake kujitoa (Unlike / Unfriend) toka kwenye urafiki au ufuatiliaji kwake. Je unadhani ni kweli kila kitu kinachotumwa kwenye Facebook hutumwa na na muhusika? Jibu ni hapana. Mara nyingi ni wavamizi walioingia kwenye akaunti ya muhusika na kuitumia kadri wawezavyo ama kwakuwa umeruhusu vipachiko (apps) zitume kwa niaba yako.

Siku hizi, uvamizi wa akaunti kwenye Facebook umekuwa mkubwa, na asilimia kubwa ya uvamizi huu hutokana na ama wahusika kutofahamu athari wa wanachokichagua ama kutokujua jinsi ya kujilinda. Kama ilivyo ada, Dudumizi itakuelezea namna ya kujilinda na uvamizi huo kwenye Facebook.

Posted On Tuesday, 26 August 2014 08:10

Mitandao jamii imekuwa moja ya nyenzo imara kabisa ya kujitangaza na kuwafikia walengwa wengi kwa uharaka na mapana zaidi kwa njia ya mtandao. Jiulize swali dogo tuu, je kwa siku za karibuni umekuwa ukitumia njia gani kufahamu juu ya bidhaa au huduma fulani.

Je kwa kutumia tangazo la kwenye TV au Radio ambapo hauna uhakika hata saa ngapi wataonesha tangazo unalohitaji? Au kwa kupitia gazeti ambapo wengi wetu sasa inapita hata mwezi bila kusoma gazeti lililochapishwa? Au ni mara ngapi umetumia muda wako kusoma lundo la emails kwenye sanduku la email za matangazo (Junk emails)?

Matumizi ya facebook kwa Biashara

Siku hizi watu wamebadilika sana, wateja hupendelea kutafuta huduma toka mahali ambapo wanapata taarifa zote kwa upamoja tena pindi wanapohitaji, baadhi ya njia watumiazo kwa sana ni kama; kwa kutumia mitambo ya utafutaji (search engines) au toka kwa marafiki zao walio kwenye mitandao jamii (Social networks). Na huko ndiko kunakoshibisha njaa ya huduma na kujibu maswali yao yote.

Je wewe ni mmoja wa watoa huduma wanaoshibisha njaa ya taarifa za huduma au kujibu maswali ya wateja? Facebook siyo sehemu ya kupotezea muda kama wengi wanavyofikiria, pia siyo sehemu ya vijana peke yake na wala siyo sehemu ya kukimbiwa na wafanyabiashara makini.Facebook ni sehemu inayounganisha watu pamoja, na wewe kama mfanyabishara makini,Facebook ni sehemu sahihi itakayokuwezesha kujitanua na kukutana na wateja wengi wa sasa na wa baadae.

 Twende kazi, ili kuwasaidia wafanyabiashara na Wakurugenzi juu ya matumizi thabiti ya Facebook kibiashara, Dudumizi Technologies imeandaa kitabu kifupi juu ya matumizi ya Facebook kwa biashara,kitabu hiki kimelenga na kujikita moja kwa moja kukuongoza kwenye kila kitu muhimu unachotakiwa kukifahamu kwenye matumizi thabiti ya Facebook kwa biashra yako. Utakapomaliza kitabu hiki, basi utakuwa na uelewa mzuri siyo tuu kuhusu mitandao Facebook yenyewe kama Facebook, bali mahusiano yake na biashara yako
 

 
 
Kwa makala zaidi za IT fuatilia kurasa wetu wa Facebook http://www.facebook.com/dudumizi
Posted On Wednesday, 13 August 2014 09:47


Katika dunia ya leo, kama wewe ni mfanyabiashara basi hauwezi epuka ushawishi wa mitandao jamii. Ingawa wengi wetu tumekuwa tukiitumia mitandao jamii kwa ajili ya mawasiliano pekee, ila kuna mengi yanaweza kufanyika na kusaidia kukuza ufannisi wa biashara yako.

Kwa kulitambua hilo, Dudumizi Technologies LTD inakuletea mafunzo juu ya njia na namna sahihi za kutumia Facebook kukuza na kuboresha Biashara.

Mafunzo haya yatakuwa ya wiki mbili, bila kukuchosha (tukitambua muda ni kitu muhimu kwa mjasiriamali), tutakutumia dondoo (kwa email fupi) iliyojikita moja kwa moja kwenye utendaji. Hivyo, kila siku utapokea email moja inayokufundisha jinsi ya kutekeleza hatua husika. Mwisho wa siku, utakuwa umejijngea uwezo mkubwa wa kutumia Facebook kwa ajili ya biashara yako.

 Pia, washiriki wote watapata nafasi ya kuuliza maswali kwa email kwenda kwa wataalamu wetu kwa muda wote wa mafunzo bila gharama yoyote. Pia washiriki watajumuishwa kwenye muendelezo wa mafunzo ya matumizi mbalimbali IT kwenye biashara kwa Video kwa siku za usoni.

 

Walengwa: Wamiliki wa biashara wadogo na wa kati

Gharama: Bure, unachotakiwa ni kujiunga tu na fomu ya mlisho wa email chini

Muda wa mafunzo:  July 21 - Agosti 5

Muda wa mwisho kujiunga: July 20

Idadi ya Washiriki: 100

Lugha: Kiswahili

Muandaaji: Dudumizi Technologies LTD

 

Fomu ya Kujiunga bofya Hapa

 

 

Posted On Tuesday, 15 July 2014 14:24

Katika maisha ya kiujasiriamali ya sasa, hauwezi kuepuka maumizi ya Tekinolojia.Tekinolojia siyo tu inakuwezesha kufikia watu wengi zaidi, bali pia kuongeza ubora na ufanisi wa huduma zako kitu kitakachokufanya uwe wa kipekee.

Wajasiriamali wengi wamekuwa na shauku na hamu kubwa ya kutumia tekinolojia ili kuongeza ufanisi wa huduma zao. Kwakuwa wengi wa wajasiriamali hawa hawana uelewa mkubwa wa mambo ya tekinolojia (na si kazi yao), hivyo hujitoa kafara kwa watu wa tekinolojia wakiamini wao ndiyo msaada wao mkubwa. Lakini si mara zote mambo yanaenda sawa.

Tangu kuanzishwa kwa Dudumizi Technologies, tumekuwa tukipokea wateja wengi ambao wamekuwa wakilizwa au kukatishwa tamaa na hawa watu wa tekinolojia. Hivyo ili kuwasaia wengine, katika makala hii, tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia pindi unapochagua mtoa huduma wa tekinolojia (IT).

1. Kadri uwezavyo, fanya shughuli na kampuni, na siyo mtu binafsi

Moja ya kitu cha msingi wakati unachagua mtoa huduma wa IT ni kuhakikisha unafanya kazi na kampuni na si mtu binafsi. Ingawa watu wengi wanaona kufanya kazi na mtu binafsi ni rahisi, lakini wengi wa watu binafsi hawa si wale walio makini na kazi yao, hivyo rahisi itakugharimu mno mno.

Posted On Saturday, 12 July 2014 06:08


Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.

Nia ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja wake wamebadili tabia ya kuweka

Posted On Monday, 30 June 2014 15:20

140106143640 google car 512x288 0 nocredit 9da55

Na Hudugu Ng'amilo

Kampuni ya Teknologia ya Google imesema itaanza kutengeneza magari yasiyohitaji madereva .
Kampuni hiyo ambayo imejijengea sifa kwa njia ya kipekee ya utendakazi wake katika sekta ya kiteknolojia imekuwa ikikarabati magari ya kawaida.

Posted On Wednesday, 28 May 2014 16:04

tehemaaa_9f0b2.jpg 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA toka  Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Emmanuel Mahinga akitoa maelezo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu jinsi Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.05) unavyofanya kazi  na  malengo ya kuanzishwa kwa mfumo huo ikiwemo kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini.

 

tehema.2_f58b4.jpg

Afisa Msimamizi wa Fedha (TEHAMA) toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw.  Elisa Rwamiago (katikati)akifafanua kwa waaandishi wa habari jinsi  Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.) utakavyoongeza tija katika utendaji wa Serikali za Mitaa na kuondoa malalamiko ya kuwepo mianya ya  vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma.kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi Rebecca Kwandu.kulia,  ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama

fafafaff_642fa.jpg 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi Rebecca Kwandu (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.05) Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo Halmashauri 133 na Mkoa 21 ya Tanzania Bara imeunganishawa katika mfumo huo, katikatika ni Afisa Msimamizi wa Fedha (TEHAMA)  toka TAMISEMI  Bw. Elisa Rwamiago na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama. (FS)

 

Posted On Friday, 18 April 2014 04:38

Mnamo tarehe 8/4/2014 kampuni ya utengenezaji wa mitambo endeshi ya kompyuta (Operating Systems) ya Microsoft ilisitisha utoaji wa huduma za muda mrefu kwa mitambo ya XP, ni moja ya mitambo endeshi inayotumika na watu wengi sana.Tangu kutoka kwa taarifa hizo, kumekuwa na maneno na mikanganyiko mingi mno kwa wateja hususan hapa Tanzania.

Kwa kuwa ni mitambo inayotumika kwa weingi kwenye kompyuta nyingi zinazotumika kwenye mabenki na maofisini, hivyo watu walifika mbali hata kusema eti pesa zetu hazipo salama tena. Hivyo, ili kuondoa hofu hizi zinazoizunguka jamii, ungana nasi Dudumizi kwenye kujua nini maana ya kikomo hiki cha huduma na jinsi gani kinaweza kuathiri biashara yako?

 Kwa nini XP imefikia kikomo?

XP iliingia sokoni miaka 12 iliyopita, tangu kuingia kwake, imekuwa ni mtambo endeshi unaotumika kwa wingi na makampuni mengi duniani kote. Na pia ni moja ya mtambo endeshi kutoka Microsoft uliokaa kwa muda mrefu sokoni. Ingawa katika uhai wa Windows XP, kumekuwa na matoleo mengine mengi kama Windows Vista, Windows 7 na ya sasa ambayo ni Windows 8, lakini kampuni ya Microfost imeendelea kutoka msaada wa kiufundi na kimatumizi kwa wateja wake wote, hivyo kwa maneno mengine tunaweza kusema,muda wake wa maisha umefika na ni mzigo kiutendaji na hata kibiashara kwa Microsoft kuendelea kuhudumia Windows XP ndiyo maana wameamua kusitisha huduma kwa Windows XP.

Je nini maana ya usisitshwaji wa Huduma?

Hapa ndipo palitokea mkanganyiko miongoni mwa watu wengi, kusitishwa kwa huduma hakumaanishi kuwa kompyuta zote zinazotumia XP hazitotumika tena kama wengine walivyoifananaisha na uhamaji wa mitambo ya analog kwenda Digital. Kusitisha kwa huduma kwa XP kunamaanisha, kampuni ya Microfot haitoendelea kutoa huduma (Support) kwa watumiaji wa windows XP tena, huduma hizi ni kama masasisho (updates) ya kiusalama, maboresho ya ufanyaji kazi (kama vile XP SP1, 2..) na huduma nyongine za utumiaji.

Hivyo, unaweza kuendelea kuitumia XP bila shida kama una uhakika kukosa huduma hizo hakutoathiri biashara.

Je kama ninatumia Windows XP, kompyuta yangu itaendelea kutumika?
Jibu ni ndiyo ila kuwa makini. Kusitishwa kwa huduma kwa Windows XP hakumaanishi kuondolewa kwa XP toka kwenye kompyuta yako, bali ni kutoweza pata huduma, hivyo Windows iliyopo kwenye komputa yako itaendelea kutumika kama kawaida, ila kuanzia sasa uhakika wa usalama wako utaendelea kupungua siku hadi siku.

Nini athari za kuendelea kubakia kwenye Windows XP?

Kama nilivyofafanua hapo juu, kusitishwa kwa utoaji wa huduma kwa XP, kunamaanisha Microsoft haitohusika na chochote kinachotokea kwenye matumizi ya XP, hivyo basi kuendelea kutumia XP inamaanisha ni kama mtoto aliyeamua kujitegemea yeye mwenyewe.

Kama wengi walivyowahi kusema, Windows XP ni moja ya mitambo endeshi ambayo haikuwahi kuwa tengevu (stable), imekuwa ikishambuliwa sana na virusi, minyoo nk, mara nyingi Microsoft wamekuwa wakitoa masasisho ya kuja kuzuia hizi vamizi, hivyo kama utaamua kuendelea kubaki kwenye XP, unatakiwa ujiandae na matumizi bora bila kusahau programu za usalama (Anti Virus) zilizo thabiti.

Virusi vinavyoishambulia Windows XP vilianza kupungua baada ya kuja kwa Windows Visa na Windows 7, ila kwa siku za hivi karibuni, tangu kutangazwa kwa kusitishwa kwa huduma, tumeshuhudia kurudi tena tena kwa kasi zaidi vamizi zinazolenga windows XP.

Je ni Windows ipi ninashauriwa kuhamia?

Kwa watu binafsi wanaweza kuhama kwenda Windows 8 kwa kununua leseni binafsi, na wale wa makampuni, wanaweza kuhama kwa kununua leseni ya kampuni na kuhama kwa ujumla. Timu yetu ya Dudumizi inaweza kukusaidia kwenye ushauri juu ya hili.

Ushauri:

Kwa wale wanaotumia Windows XP kwa watumiaji wakubwa (kama mabenki), ni dhahiri kuwa hawatoweza kuhama kwa mara moja, watahitaji muda mpaka waje kuhama, hivyo wanahitaji kuja na njia ya mpito itakayowawezesha kupambana na matatizo yoyote yatakayojitokeza kipindi wanajipanga kuhamia kwenye matoleo mengine ya Windows. Kwa mfano, Umoja wa nchi za Ulaya umeingia mkataba na Microsoft kuendelea kutoa huduma kwa Windows XP kwa miaka miwili hadi hapo watakapokuwa wamehama moja kwa moja.Na kwa watu binasi, unaweza kununua nakala ya Windows 8 na kuhamia huko bila kupotea chochote. Dudumizi Technologies inaweza kukusaidia kwenye hili, wasiliana nasi kwa kutuandikia info@dudumizi.com au tupigie 0768816728.

Timu nzima ya Dudumizi inakushauri kuhakikisha unakuwa na mpango thabiti wa matumizi ya kompyuta katika kampuni yako, na kama ni kwa matumizi binafsi, basi hakikisha unafuata kanuni bora za matumizi ya kompyuta, na hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha unakuwa salama.

Posted On Monday, 14 April 2014 11:58

Ramani inayoonesha nchi tatu barani Afrika zenye juhudi ya kuongeza nishati ya nuklia

Ramani inayoonesha nchi tatu barani Afrika zenye juhudi ya kuongeza nishati ya nuklia.

Nchi tatu barani Afrika zimeanza juhudi za kuongeza nishati ya nuklia katika mikonga yao ya umeme. Kenya na Nigeria zinataka kuanza nishati ya nuklia wakati Afrika kusini – nchi pekee kusini mwa bara la Afrika ambayo ina mitambo ya nuklia – inataka kupanua uwezo wake. Mpaka sasa, mataifa ya Afrika yamekuwa yakitegemea mifumo ya kizamani kuzalisha umeme – nguvu za maji au mkaa wa mawe. Lakini vyanzo hivyo vimekuwa na madhara ya kijamii na mazingira, na hata kusababisha watu kuhama makazi yao. Lakini swali kubwa linaloulizwa ni jee Afrika ina uwezo wa kuanza nishati ya nuklia?

Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia ni chini ya asilimia 10 tu ya jumla ya makazi yote ya watu barani Afrika ambayo yanapata umeme. Hali hiyo kwa namna kubwa inaathiri pia maendeleo ya viwanda na sekta nyinginezo katika bara masikini kuliko yote duniani.

Shida hiyo ya umeme ndio inasababisha baadhi ya nchi za Afrika kutafakari nishati ya nuklia – mfumo ambao unatumiwa katika baadhi ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea kama vile Marekani, India na China.

Kelvin Kemm, mtaalam wa fizikia ya nuklia huko Afrika Kusini, anasema Afrika inahitaji kuangalia nje ya mifumo ya uzalishaji umeme inayotumika sasa. Anasema "kwa jumla inapata umeme unaotokana na nguvu ya maji, na kila mtu anajua kuwa ukame wa miaka kadha barani humo unawezekana. Kwa hiyo ni hatari kujenga uchumi kwa kutegemea umeme unaotokana na maji."

Posted On Friday, 28 March 2014 09:57

Katika ulimwengu wa leo neno blog siyo kitu kigeni, leo hii karibu kila mtumiaji wa internet anayo blog yake. Blogu hizi kuna zile zinazotembelewa na watu wengi na kuna zile zinazopata watembeleaji kwa mdondo.Je umewahi kujiuliza kwanini watu hawatembelei blog yako kama wanavofanya kwa blog fulanifulani? Ingawa kuna sababu nyingi kama umri wa blog, umarufu wa mmiliki wa blog nk lakini kuna kuna vitu ambavyo unaweza kuvifanya na vikakuongezea idadi ya watembeleaji.

Hivyo kwenye makala ya leo tutaangalia ni vitu gani vya msingi kuzingatia ili blog yako ivutie wasomaji wengi zaidi.

 

 1. Ishi kwenye blogu yako, chagua uelekeo unaokufaa.

Kama umekuwa ukifuatilia tasnia hii ya blogu, utagundua kuwa makala nyingi zinazoandikwa kwenye blogu nyingi za Tanzania huwa zinafanana sana, na hata muelekeo wa hizi blogu huwa ni uleule. Ingawa ni jambo la kawaida kwa kila mtu kukimbilia sehemu inayopendwa na wengi (blogu za habari), lakini jinsi unavyokimbilia sehemu yenye watu wengi, ndivyo jinsi unavyongeza ushindani.

Siyo tu ushindanni, bali wengi wamejikuta wakiingia kwenye uelekeo ambao hawaumudu hivyo siku ya mwisho wanajikuta wakikopi na kupaste.

Posted On Wednesday, 12 March 2014 20:32

1_9db31.png

Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uwekezaji Mhandisi Decklan Mhaiki (katikati) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) pamoja na Waandishi wa habari moja ya mashine za kufua Umeme zitakazofungwa katika eneo la Kinyerezi I jijini, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Mradi wa ujenzi huo, Bw. Shaun Moore.

2_77512.png

Mmoja wa mitambo ya kufua umeme ambao utafungwa katika eneo la Kinyerezi I mara baada ya ujenzi kukamilika. Mitambo hiyo, inatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati za umeme 150 ambazo zitaunganishwa katika gridi ya Taifa.

3_33f1a.png

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wa kampuni inayojenga kituo hicho ya Jacobsen Elektro.

4_26516.png

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kinyerezi I, Bw. Shaun Moore, wakati akimweleza maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

(J.G)

 

Posted On Wednesday, 12 March 2014 15:16
Page 2 of 7

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart