We have 122 guests and no members online

Znateli
×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

facebook a6957

Facebook na WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana.

Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.

Posted On Thursday, 20 February 2014 07:33

mcl 575b3

Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd mkoani Mara, Christopher Maregesi amejeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Bunda, baada ya kundi la watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa moja ya vyama vya siasa wakiwa na viongozi wao kumteka ambapo walimmpiga, kumtesa na kumjeruhi huku wakimpora vitendea kazi vyake ikiwamo kamera.

Posted On Sunday, 09 February 2014 08:03

IMG 52011 96653

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga(mbele aliyesimama) akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano kuhusu ushirikiano wa serikali na vyombo vya Habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini.Wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Habari na Mawasiliano leo Mkoani Tanga.

Posted On Saturday, 08 February 2014 10:45

kajubi ec130

Gazeti la Mwananchi kwa mara ya pili mfululizo waandishi wake wameongoza kwa kupeleka kazi nyingi zaidi ya vyombo vingine vya habari katika Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) kwa mwaka 2013. (HM)

Posted On Thursday, 30 January 2014 04:24

mfugale 17b9d

Mkurugenzi wa IRUWASA, Marco Mfugale (kushoto) akikabidhiwa mfano wa mashine ya kulipa maji na Athanas Leonce wakati wa uzinduzi wa malipo ya bili ya maji kwa njia ya mashine hizo.(HM)

Posted On Wednesday, 29 January 2014 14:24

kikwete1 243ba

Rais Jakaya Kikwete amesema ili kuhakikisha sekta ya kilimo inapiga hatua lazima ugunduzi wa teknolojia mpya zinazogunduliwa zitumike kwa vitendo. (HM)

Posted On Wednesday, 29 January 2014 05:44

BURUNDI_ce135.jpg

Serikali ya Burundi imezindua mradi wa dola milioni 25 za Kimarekani kwa ajili ya mtandano wa Intaneti wenye kasi kubwa nchini humo.

Mradi huo umezinduliwa leo huko Bujumbura na Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo ambaye amesema mashirika manne binafsi na serikali ndio wamiliki wa mkongo wa taifa wa mawasiliano (fiber optic) wenye lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata Intaneti kwa bei nafuu ifikapo mwaka 2025. Tayari kebo ya mkongo huo wenye urefu wa kilomita 1,000 imeshawekwa katika mikoa 17 ya nchi hiyo. Kebo hiyo itaunganishwa na kebo za chini ya bahari ambazo zinaunganisha Afrika na dunia nzima kupitia bandari za Mombasa, Kenya, na Dar-es-Salaam Tanzania. (R.M).

Posted On Wednesday, 22 January 2014 02:07

100 e5ed0Mfanyakazi wa zamani wa muda katika Shirika la Usalama la Marekani, NSA, Edward Snowden, ambaye alifichua kuwepo kwa mipango ya Marekani kufuatilia taarifa za mawasiliano ya watu, amesema amefaniskisha lengo lake.

"Kwa kuridhika binafsi, mpango wangu tayari umefanikiwa," ameliambia gazeti la Washington Post. (HM)

Posted On Wednesday, 25 December 2013 11:38

Jakaya-Kikwete21 22d1c

RAIS Jakaya Kikwete, amesaini hati ya dharura (Certificate of Emergency) ya kufanyika kwa marekebisho ya Muswada wa Fedha wa mwaka 2013, ili kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu (SimCard Tax). (HM)

Posted On Friday, 20 December 2013 09:34

Kama wewe ni mtumiaji wa website, basi moja ya vitu vinavyokera ni pale unapofungua website halafu haifunguki. Kutofunguka kwa website kunaweza kusababishwa na matatizo mengi. Kuna matatizo ambayo yanaweza kuwa ni upande wako wewe mtumiaji kama (intaneti yako kuwa chini sana, au programu ya ulinzi (anti virus) inakuzuia kufungua hiyo website nk, pia inaweza kuwa ni tatizo la website husika. Ili kuweza kusaidia kutambua chanzo cha tatizo na kurahisisha matumizi, kila kosa linalotokea kwenye website limepewa namba husika ambayo italitambulisha, ama kwa watumiaji ama kwa wamiliko na hii tunaiita namba ya utambulishi wa error (error status code) .

Kuna rundo la makosa unayoweza kukunana nayo, ila leo hii tutaangalia yale yanayotokea mara kwa mara;

Posted On Wednesday, 18 December 2013 08:30

Katika sehemu ya kwanza ya jinsi ya kupima mafanikio ya Website, tumeangalia dhumuni la upimaji wa mafanikio, pia tumeangalia vitu muhimu vya kuzingatia. Tumeona umuhimu wa kuwa na malengo yenye sifa kuu tano au kwa kifupi (SMART).

Katika sehemu hii ya pili, tutaangalia vizio muhimu vya upimaji wa mafanikio ya Website.

Kama tunavyojua, dhumuni la kuwa na website ni ili iweze kutumika kwa watu, wawe wateja, wafanyakazi au hata washirika. Kwa kujua takwimu za matumizi ya watu hawa, ni dhahiri utaweza kujua ufanisi wa Website yako. Vizio hivi vya
uchambuzi vitakuwezesha kupata picha kamili ya ni jinsi watu wanafika vipi kwenye website yako, wakifika wanatembelea kurasa gani, wanakaa muda gani nk. Google analytics ni moja ya website ambazo zinaweza kukusaidia kupata takwimu hizi.

Hebu, tuangalie vizio hivi;

Posted On Sunday, 15 December 2013 09:29

 

Katika makala zilizopita tumeangalia umuhimu wa kuwa na Website. Pia tumeangalani hatua muhimu za kupitia mpaka unakuwa na website. Lengo la website ni kufanya kazi na siku ya mwisho wewe kama mmiliki ni lazima uone matokeo ya kazi iliyofanywa na website.

Ingawa kumekuwa na mijadala sana kwenye uwanja wa IT juu ya upimaji wa matokeo ya IT, wengi wakisema, ni ngumu kupima matokeo yanayosababishwa na IT pale ambapo IT inakuwa ni  muwezeshaji, na website ikiwa ni sehemu moja wapo. Ukweli ni kuwa, kwa sasa IT si muwezeshaji tena, bali ni sehemu ya kazi. Hivyo, inatakiwa itoe matokeo tena yanayopimika, na website ni sehemu mojawapo. Na lazima ijumuishwe kwenye malengo ya kampuni / shirika.

Kitendo cha upimaji wa Website hutegemea na sababu ya kuanzishwa kwake, leo hii kuna mamia ya website kwenye kila idara, kuanzia blogu za habari hadi zile website za serikali. Hivyo hakuna njia moja kupima mafanikio hayo. Kwakuwa kila website ina malengo tofauti, lakini kuna kitu ambacho website zote zinahusika, nacho ni; zote zinamlenga mtumiaji na mmiliki.

Posted On Wednesday, 27 November 2013 12:34
Page 3 of 7

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart