We have 143 guests and no members online

Znateli
×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

Siku hizi, katika kila watu kumi wanaotumia mtandao, basi angalau watano kati ya hao wanatumia mitandao jamii. Kuna baadhi ya watu wamegeuza mitandao hii kuwa kama ni sehemu ya mawasiliano, ama ya mtu kwa mtu au ya kibiashara. Siku hizi, si kitu cha kushangaza kusikia mtu maarufu au kiongozi fulani atakuwa kwenye Facebook saa fulani kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi / mashabiki wake. Mitandao hii ni kama vile Facebook, Twitter, Jamiiforums nk, hivyo basi, hatuwezi kuepuka ushawishi wa mitandao jamii katika jamii yetu.

Matumizi bora ya mitandao jamii huweza kuleta faida nzuri sana, ila huwa kinyume pale inapotumika sivyo, ama kwa kutokujua ama kwa kuamua. Hivyo leo hii tuangalie mambo kadhaa ya kuepuka unapotumia mitandao jamii.

1. Epuka kujiacha wazi kwenye mitandao jamii.

Posted On Wednesday, 13 November 2013 05:17

Timu nzima ya Dudumizi Technologies, inayo furaha kukutaarifu kuwa tumefanya mabadiliko ya Logo, Hivyo, kwa matumizi yote ya kiofisi, hakikisha kuna Logo kama inavyoonekana hapo juu na si vingine. 

Pia, tunapeda kuwataarifu kuwa majina ya Website yanayomilikiwa na Dudumizi Technologies ni Dudumizi.com, Dudumizi.net na Dudumizi.co.tz tu. Hivyo kwa matumizi yoyote ya kibiashara na Dudumizi Technologies, tafadhali hakikisha Emails zinatoka kwenye majina hayo tu na si vinginevyo.

Endapo utakutana na utata, ushauri au maoni, tafadhali tutumie email kwenda info at dudumizi.com au simu +8615271818525 / +255716157157 au Skype Dudumizi

 

Mkata Nyoni

Business Developement Office - Dudumizi Technologies

Posted On Saturday, 09 November 2013 12:47

kenya 441cb

Polisi nchini Kenya wamewahoji maafisa wakuu watendaji wa kampuni za huduma za simu za rununu kuhusu usajili wa kadi za simu za mkononi zinazotumia huduma za kampuni hizo. (HM)

Posted On Wednesday, 09 October 2013 03:56

karsan e3347

UMOJA Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umesema jopo la wanasheria wake lipo katika hatua za mwisho za kuandaa mashitaka dhidi ya Serikali kutokana na mauaji ya kinyama ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi. (HM)

Posted On Saturday, 28 September 2013 03:21

Kuna usemi wa kiswahili unaosema, "mali bila daftari, hupotea bila habari". Maana ya msemo huu sio kwamba kwenye daftari ndio utahifadhi mali zako, la hasha, bali kwa kuwa na mipango na kumbukumbu za matumizi ya mali zako kimaandishi, basi utaweza kufuatilia mwenendo wake. Hili ni sawa na kwenye Website, kuwa na website bila kuwa na maandalizi ni sawa na kujenga nyumba bila msingi, ndio maana siku ya mwisho utaona Website ni mzigo usio na maana.

Kuna wakati niliwahi kufanya kazi na mmoja wa wanablog maarufu Tanzania ambaye hadi leo hii amekuwa akiogopa mabadiliko baada ya kufeli kwenye badiliko moja alilotaka kufanya kwenye blog yake.Baada ya kukutana na mimi aliniambia, Nyoni, nimewahi kujaribu, ila tulifeli vibaya, nikamuambia, mulifeli kwakuwa mulikuwa munajaribu na sio muliamua. Kwani kama mungeamua, basi mungekuwa na maandalizi na mipango ya awali kabla ya kuanza maboresho ya blog yako, hivyo mulifeli kupanga, ndio maana mukaja kufeli kutekeleza.

Posted On Friday, 27 September 2013 13:28

jaji d9157Mahakama ya kimataifa ya ICC imetoa onyo kali kwa wanablogu nchini Kenya,wanaotoa taarifa kuhusu mashahidi waliofika mbele ya mahakama ya ICC.

Hii ni baada ya taarifa kuhusu shahidi wa kwanza mbele ya mahakama hiyo kujitokeza kwenye mitandao hasa kwenye blogu, twitter na Facebook kumhuusu. (HM)

Posted On Friday, 20 September 2013 04:10

Makosa 5 wanayoyafanya wamiliki wa Website na jinsi ya kuyaepuka

Katika dunia ya leo, kuwa na website ya kampuni au biashara si kitu cha anasa na pia si kitu cha hiyari bali ni cha lazima kwa kila mfanya biashara makini.

Maendeleo ya tehama yamefanya bei na gharama za kutengeneza na kumili website kushuka huku watengenezaji wa website hizi wakiwa karibu kabisa na mteja, leo hii unaweza kupata makampuni ya kutengeneza website kila kwenye kila kona ya mji. Sio hivyo tu, siku hizi kuna makampuni mengi ya Tehama yamekuwa yakiwawezesha watumiaji wake kuwa na website au blog bila gharama yoyote, mfano wake ni Wordpress na Blogspot.

 Kumiliki Website sio mwisho wa safari ya kibiashara, kwani unatakiwa kuifanya website yako iwe inayofanya kazi. Usiiche ilale usingizi mnono huku wewe ukiwa mmiliki wake unashindwa kuiamsha. Website inatakiwa kufanya kazi, iwe kama sehemu ya kuleta wateja (mfano saluni au hoteli), iwe kama sehemu ya biashara na mauzo(mfano wale wanaouza vitu online)na pia iwe sehemu ya kuwasiliana na wateja wako.

Wengi wamekuwa wakishindwa kufikia matokeo haya, ama kwa kutofahamu au kushindwa kujua fursa ambazo wanaweza kuzitumia. Hivyo leo hii tuangalie makosa ambayo wamiliki wengi wamekuwa wakiyafanya na jinsi ya kuyaepuka au kuyatatua.

Posted On Monday, 16 September 2013 14:09


Ni ukweli usiofichika kuwa, katika dunia ya leo, zaidi ya nusu ya vijana wa Kitanzania wanaotumia Internet, basi hutumia Facebook. Tumeona matukio kadhaa ya watu kudhalilishwa na wengi kuamua hata kususa kutumia mitandao jamii. Juzi tumesikia naibu waziri mwenye dhamana ya ICT akitangaza kujitoa What's Apps kutokana na watu ambao ni marafiki zake huko kutochunga matumizi yao.

Posted On Friday, 30 August 2013 09:57

Baada ya kukamilisha mafundisho ya Joomla, nimekuwa nikipokea barua pepe nyingi sana toka kwa watu ambao wamekuwa wakiniuliza juu ya template gani bora, kiendelezo gani bora na mengineyo.

Ingawa hakuna jibu la moja kwa moja juu ya ubora, ila kuna jibu la moja kwa moja juu ya nini kinashauriwa. Hapa ninamaanisha, siwezi kusema kiendelezo hiki ni ndio bora au sio bora kuliko kingine kwani kuna njia na mambo mengi ya kuzingatia pindi unapochagua viendelezo vya Joomla. Ila ninaweza kusema kinedelezo kipi kinaweza kukusaidia vipi.

Posted On Friday, 16 August 2013 10:17

 

DSC_9458Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Bw. Profesa John Nkoma  akizungumza katika uzinduzi huo kushoto ni Inocent Mungi Meneja Mawasiliano wa TCRA.

Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

Ongezeko la matumizi ya Intaneti kwa watanzania nchini limeongezeka kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 Kwa takwimu za hivi karibuni.Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Profesa John Nkoma wakati wa Kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mawasiliano yaliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Profesa Nkoma amesema kuwa wengi wa         M.M

Posted On Wednesday, 31 July 2013 16:09

Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi sehemu mbalimbali Tanzania, lengo langu kubwa halikuwa kwa ajili ya kutafuta kazi, bali nilitaka kujua uelekeo wa ajira kwa nchi yetu ya Tanzania. Kwani, uelekeo huu ndio utakaoweza kubadirisha mustakabali wa ufanisi wa kazi na maendeleo kwa taifa letu.Pia, nilitaka kujua je waajiri wanajua nani wanayemtafuta?

 Mwaka juzi nilipata nafasi ya kuwa mmoja msemaji mkuu (Key note speaker) katika mkutano wa kimataifa juu ya E Commerce na E Governance ulioandaliwa na IEEE hapa China, hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuwa katika uwanja kama ule mbele ya magwiji toka makampuni makubwa duniani. Katika mkutano ule, nilizungumzia kuhusu aina mpya ya biashara ya online kwa kutumia mitandao jamii (Social Commerce), ni mada iliyovuta hisia za watu wengi sana hivyo ilikaribisha maswali mengi mno.

Moja ya swali nililoulizwa na Mr Jen Yao Chung toka kitengo cha tafiti cha IBM Marekani( IBM T.J Watson Research Center) ni jinsi gani tutaweza kupima faida au mchango wa mitandao jamii(social networks) kwenye biashara za mitandaoni(ecomerce). Katika kumjibu swali lake, nilimuambia kuwa, tunatakiwa kuifanya mitandao jamii(social networks) kuwa sehemu ya biashara ili tuweze kupima na kuuchunga mchango wake.

Posted On Tuesday, 23 July 2013 09:14

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba akizungumza na waandishi kuhusu mipango ya kamati yake kuangalia tat

Na:Lorietha Laurence-Maelezo

Taasisi huru isiyo ya kiserikali kutoka nchini Marekani inayoitwa ISACA tawi la Tanzania kwa kushirikiana   na kampuni ya Norway inayoshughulikia maendeleo Afrika Mashariki (Norway Registers Development  East Africa Limited –NRD-) wameandaa semina  ya usalama wa matumizi ya  kompyuta na mitandao yake katika nyanja mbalimbali kwa mashirika ya umma, benki, serikali na watu binafsi.Semina hiyo 

Posted On Monday, 22 July 2013 15:58
Page 4 of 7

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart