We have 374 guests and no members online

Maji
×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

untitled4 00487Baadhi ya watoto wakiwa tayari kushindana katika mbio za Vodacom Cheka Nao zilizofanyika Dar Live,Mbagala siku ya kifamilia iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwaajili ya Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kila mmoja kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika na ofa piga *149*01#

untitled5 85eb9

 

Bi.Tumu Saidi ambae ni mkazi wa Mbagala,Dar es Salaam akimsikiliza Ofisa wa Vodacom Tanzania jinsi anavyomfafanunua faida za kujiunga na Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwa mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#,Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa kanda ya Mbagala Idd Mawe na kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu.

Posted On Sunday, 23 June 2013 10:00

untitled 78498www.greensolar.se

Posted On Friday, 21 June 2013 14:23

Katika habari zilizotawala uwanja wa Tehama kwa wiki hizi ni habari ya Snowden, mfanyakazi wa shirika la usalama la marekani (NSA) pia ni muajiriwa wa zamani wa CIA aliyelikisha taarifa za siri zinazoelezea jinsi marekani inavyofuatilia taarifa za watumia mtandao bila idhini yao. Kuna wanaomuona Snowden kama hero na wengine wanamuona kama msaliti. Kulingana na maelezo ya Snowden kama alivyonukuliwa na mtandao wa Guarnian, inamaana kila unachoongea, unachotuma kinachunguzwa, wanafanya hivi kila mahali hadi kwa washika dau wakuu kwenye hii nyanja ambao ni Facebook na Google. Taarifa inaelezea kuwa, mashirika haya yametakiwa kuwapa NSA uwezo wa kuingia kwenye mitambo yao na kuchota chochote wanachotaka bila taarifa ya ziada.

 

Snowden ameamua kutoa taarifa hizi kwa kile alichokiita ni kuingiliwa kwa uhuru na unafasi wa watu (Privacy). Katika maelezo yake, Snowden anasema, taarifa nyingi zinazochunguzwa ni za watu na sio mashine hivyo watu hawa hawapo huru tena. Hii inakuja wakati serikali ya marekani ipo katika mvutano mkubwa wa masuala ya uvamizi wa mtandaoni na serikali ya China.

Posted On Friday, 14 June 2013 12:38

sms f6b99

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Tido Mhando (kushoto) akimwangalia Mkurugenzi wa Kampuni ya Vodacom, Rene Meza alipokuwa akijisajili katika huduma ya habari zilizotokea hivi punde (Breaking News) kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Dar es Salaam, jana. Picha na Silvan Kiwale

Posted On Tuesday, 11 June 2013 06:44

airtel c964a

AIRTEL Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yao ya kuwapatia wateja wake unafuu zaidi kupitia huduma yake ya AIRTEL YATOSHA nchini ambapo sasa wateja watafurahia Vifurushi vya Airtel Yatosha kwa masaa 25 kwa siku,   hii itawawezesha watanzania kufurahia kupiga simu mtandao wowote kwa gharama nafuu kwa muda mrefu zaidi.

Posted On Saturday, 08 June 2013 17:26

Tumefanya maboresho kwenye mtambo wa kutuma maoni, sio tu tumeboresha muonekano wa maoni, bali pia tumeongeza machaguo ya mtumaji. Kuanzia sasa utaweza kutuma maoni ama kama mwanajumuiya ama kama mgeni (anonymous). Pia unaweza kupokea ujumbe kwenye barua pepe pindi tu kukiwa na majibu ya maoni yako.

 Bali ya Wanajumuiya, pia kwa watembeleaji wengine wanaweza kupokea taarifa kwa kuweka email yako kwenye kisanduku cha email kilicho kwenye kiboski cha maoni, tutakutumia ujumbe kwenye barua pepe yako(email) punde tu kukiwa na majibu au maoni mapya kwenye makala uliyochangia maoni. Hii itakusaidia usipitwe kwenye majadiliano.

 Kurasa mpya ya maoni: kumbuka: Jina na Email SI lazima, ukipenda andika na usipopenda unaweza kuacha wazi.

Posted On Wednesday, 05 June 2013 10:38

untitled9 c1ef3

Katibu mkuu wa ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma GEORGE YAMBESI amewataka wajumbe wa umoja wa vituo vya elimu kwa njia ya mtandao barani AFRIKA washirikiane na makampuni ya TEHAMA na simu za mikononi kuwafikishia elimu wananchi walio maeneo ya Vijijini

Picha na Chris Mfinanga

Posted On Monday, 03 June 2013 17:33

 

tcra 0 fcb88

THE TCRA DIRECTOR GENERAL, PROF JOHN S. NKOMA  AT THE 14TH ORDINARY MEETING OF THE AFRICAN TELECOMMUNICATIONS UNION ADMINISTRATIVE COUNCIL, 21 MAY DAR ES SALAAM.

 

00 7c644

Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo

Angalio Picha zaidi....

Posted On Wednesday, 22 May 2013 05:10


tcra3 5198b

Makamu wa Rais Mhe:Dr Mohammed Gharib Bilali akisoma hutuba ya ufunguzi kwenye mkutano wa 14 wa umoja wa nchi za Afrika katika masuala ya TEKNOHAMA,  unaofanyika jijini DSM,PICHA NA HUDUGU(mjengwablog) 

Posted On Tuesday, 21 May 2013 09:23

1 c9c96

Mkurugenzi wa TCRA, Prof John Nkoma akitoa hotuba ya ufunguzi wa wiki ya teknolojia, habari na mawasiliano inayofanyika Dar es Salaam.

Posted On Thursday, 16 May 2013 13:49

Swali ambalo mara nyingi huwa ninajiuliza ni kuwa, maisha yatakuwaje siku bila Internet au kompyuta au simu? ni dhahiri kuwa maisha yatakuwa ya upweke yenye visirani vingi. Ukweli ni kuwa Internet imetuletea mabadiriko mengi sana, sio tu imeweza kurahisisha utendaji kazi na kuwa sehemu ya kazi bali pia imeweza kuufanya ulimwengu kuwa mdogo na wenye ushirikiano. 

 Tatizo kubwa la binadamu ni mazoea, kwani kama wewe unasoma makala hii, ni dhahiri utakuwa tayari umeshazoea Internet na baada ya kuzoea utakuwa umeonja faida zitokanazo na Internet, ni kweli kabisa, siku atakapotutoka, tutammiss sana Bw Internet.

 

 Internet imeweza kuondoa siri na maficho ambayo hapo zamani ni wachache mno walikuwa wenye uwezo nayo. Kwa maneno mengi tunaweza kusema, internet ni mkombozi wa mwanadamu. Katika siku za karibuni kumetolewa takwimu ya matumizi ya internet na vinasaba vyake, mwenye macho haambiwi tazama, hebu tuangalie kwanza. Halafu tutakuja na tafakari juu ya umuhimu au maana ya takwimu hizi kwa Tanzania.

Posted On Friday, 03 May 2013 15:22
Page 5 of 7

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji