We have 138 guests and no members online

Znateli
×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

 

 

001 fe673

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akimkaribisha ofisini kwake jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza ambapo baadae viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.

Posted On Sunday, 21 April 2013 05:59

 

IMG_0154

Mtoa huduma kwa wateja Bi. Florence Ngowi akionyesha na kumueleze Mh. Jerry Silaa Meya wa Manispaa ya Ilala baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika kituo hicho wakati alipotembelea maonyesho ya vifaa mbalimbali  alipozindua kituo hicho ambacho kimeanzishwa maalum kwa ajili ya kushughulia  masuala ya huduma kwa wateja wa Kampuni hiyo

Posted On Friday, 22 March 2013 05:49

2- Mwambene kush na Mkuunzi David Wiggins 441a1

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kushoto) akizungumza na mkufunzi wa kozi fupi David Wiggins kutoka Stockport Uk ,katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

6- mwl drasani 63435

Mkufunzi David Wiggins akitoa mafunzo kuhusu matumizi mbalimbali ya mitandao ya kijamii kwa baadhi ya maafisa mawasliano serikalini katika ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam. PICHA NA MWANAKOMBO JUMAA

Posted On Thursday, 21 March 2013 14:57

 

8E9U7541

Rais Dkt.Jakaya Mriusho Kikwete,Waziri wa Elimu dkt.Shukuru Kawambwa(kulia) na Balozi wa Korea ya Kusini Mhe.Chung wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa jijini Dar es Salaam.Picha na Fred Maro

Posted On Tuesday, 19 March 2013 07:48

A

 

DSC_0869Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknologia Dr. Hassan Mshinda
akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mashindano ya “INFOMATRIX AFRICA”
yanayoshirikisha nchi zaidi ya 17, kulia kwake ni  Mkurugenzi mkuu wa shule
za Feza Ibrahim Bicaku na kushoto kwake ni Balozi wa Uturuki nchini Tanzania
Balozi Ali Davudoglu.

Posted On Thursday, 14 March 2013 14:09

02 af8ba

Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Mtondoo akitoa hutuba wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki  iliyofanyika katika Wilaya yake ya Mafia,semina hiyo ilikuwa na  lengo la kutoa elimu  kwa wannchi wa Wilaya hiyo juu ya Haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za Mawasiliano, katikati ni Mkurugenzi wa Watumiaji na watoa huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema,(Kulia ) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mohamed Kimbule.

Posted On Tuesday, 12 March 2013 06:34

Kikwete-707591

Over twenty African Ministers, Senior policy makers, Industry representatives as well as representatives of Research and Development (R&D) Institutions and Innovation centers will participate in the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property (IP) Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness.

The Conference is organized by the World Intellectual Property Organization (WIPO) and the Japan Patent Office, in cooperation with the Government of the United Republic of Tanzania. The conference will be opened by H. E Dr. Jakaya M. Kikwete, President of The United Republic of Tanzania.

 

Posted On Monday, 11 March 2013 12:30

01 31dae

Hawa Sulemani akijisomea moja ya vipeperushi vya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania baada
ya kugawiwa katika semina ya Majukumu ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika katika
Wilaya ya Mafia kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo.

02 97330

Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki
iliyofanyika katika Wilaya ya Mafia wakijisomea majaridi yenye ujumbe mbalimbali na Kazi za
Mamlaka hiyo. Baaada ya kugawiwa na Mhasibu wa TCRA BW.Patrice Lumumba.

Posted On Sunday, 10 March 2013 15:23

 

07Mkuu wa Wilaya ya Mfia Sauda Mtondoo akimkabidhi  Prudence Nyombi zawadi ya King’amuzi cha Star timu baada ya kujishindia kutokana na kujibu swali aliloulizwa juu ya matumizi ya Mawasiliano, wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika Wilayani Mafia.katikati ni Mkurugenzi wa Watumiaji na Watoa Huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema akishuhudia.

Posted On Sunday, 10 March 2013 14:51

 Rais wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ISACA Tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu teknolojia ya mawasiliano na Utawala Bora vinavyoweza kuchangia maendeleo ya uchumi na kufanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na ISACA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Norway Registers Development. (Picha na Habari Mseto Blog)

Posted On Saturday, 02 March 2013 16:55

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba akizungumza na wafanyakazi wa TTCL wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni ya Simu ya TTCL na migogoro iliyopo kwenye

Posted On Tuesday, 22 January 2013 05:05

 Nikiwa kama mjukuu kipenzi wa bibi yangu, huwa napenda sana kutumia muda wangu wa mapumziko kujadiliana naye mambo mbalimbali yanayohusu jamii, iwe yaliyokuwa yanatokea hapo awali au yanayoendelea kutokea. Ilikuwa ni siku ya jumapili baada ya kutoka kwenye mihangaiko, niliingia ndani na kumuita bibi kwa jina lake la utani ‘Nyaksi’ ili twende nje tukapunge upepo na mazungumzo ya hapa na pale.

   Kama ilivyo ada yangu, huwa napenda sana kutafiti mambo mbalimbali, nikamuuliza bibi, eti bibi nimewahi kusikia kuwa wakati wa enzi zenu mlikuwa hamruhusiwi kula mayai wakati wa ujauzito kwa kuwa mtoto atazaliwa bila nywele? Bibi Nyaksi huku akitabasamu akanigeukia na kusema, "umeshaanza, kwanza usikumbushe enzi zile bado nipo mbichi" akimaanisha wakati yupo msichana. Wote tukatabasamu kwa pamoja. Nyaksi akaendelea kusema sio mayai tu, bali vyakula vyote nyenye virutubisho kwa wingi ambavyo ninyi vijana wa leo mnaviita ‘purotini’, akiitamka protini kwa lafudhi ya kizee. Nyaksi alisema tulizuiliwa kula vyakula hivyo kwa mlengo wa mwiko, akaendela kusema, unajua Babu (jina langu alilopenda sana kuniita Nyaksi) wazee walitumia mwiko ili kututisha lakini ukweli ni kuwa wakati ule hakukuwa na tekenolojia (akimaanisha teknolojia) hivyo kama utakula vyakula vyenye virutubisho sana vitamfanya mtoto awe mkubwa, na hivyo kama utashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida basi hakutakuwa na njia nyingine ya kukusaidia. Nyaksi akaendelea ninyi vijana wa siku hizi mna raha, hospitali nyingi, madaktari wengi huku mna njia nyingi mbadala ikiwemo ya upasuaji na nyinginezo. 

Posted On Monday, 14 January 2013 04:11
Page 6 of 7

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart