We have 235 guests and no members online

Smart

Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya Dkt. Mohd Dahoma akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Wizara ya Afya juu tahadhari ya ukonjwa wa Kipindupindu hivyo amewashauri wananchi kununua chakula kilicho hifadhiwa vizuri ama chakula kimoto na kujiepusha kutumia juice zinazotengenezwa kienyeji. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar .

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya vyakula na vinywaji katika viwanja vya sikuu inayoanza kesho kutokana na tishio la maradhi ya kuharisha na kutapika ambayo yameanza kujitokeza katika nchi jirani.(VICTOR)

Posted On Thursday, 24 September 2015 08:49

Mkurugenzi wa Taasisi ya kinamama wa Kiafika inayohusika na ugonjwa wa Saratani ya matiti Bi. Ify Nwabuku(kushoto) akizungumza na wakina mama (hawapo pichani) wakati wa utoaji wa matibabu bure kwa wakina mama katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar. Kushoto ni Bi Asha Nyang’anyi ambaye ni mwanakamati wa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.

DSC_0179

Wakina mama wakimsikiliza kwa makini Bi. Ify Nwabuku wakati akitoa maelezo juu ya upimaji wa Saratani kwa wakina mama waliofika kupima afya zao katika hospitali ya Mwananyamala zilizokuwa zikitolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao walioamua kutoa huduma za kitabibu na madawa bure.

Posted On Thursday, 23 July 2015 04:33

Picha na maktaba

Na Woinde Shizza,Arusha

Mamlaka ya Chakula na dawa(TFDA) na Shirika la Viwango nchini(TBS), wameshauriwa kuwadhibiti zaidi wafanyabiashara wasio waaminini ambao wanaingia nchini bidhaa sizizo na ubora kwani wanaporomosha uchumi.

Meneja masoko wa kampuni ya Wrigleys (EA) Company Ltd, Emanuel Laswai, alitoa kauli hiyo juzi, katika uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni hiyo ya Doublemint nchini Tanzania.

Laswai alisema, uingizwaji wa bidhaa feki na zisizo na ubora zina athari za kiuchumi na kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

Posted On Wednesday, 03 June 2015 16:00

DSC_0360

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.

DSC_0289

Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.

DSC_0062

Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.

Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.

Posted On Tuesday, 26 May 2015 04:52

Muonekano wa jengo la Tropical Centre barabara ya Bagamoyo maeneo ya Victoria jijini Dar es salaam ambapo kituo cha AAR Healthcare kinapatikana hivi sasa katika ghorofa ya pili.

Sehemu za ndani za kituo kipya cha AAR

Kituo maarufu cha afya cha AAR Healthcare sasa kimehamia ghorofa ya pili katika jengo la Tropical Centre lililopo barabara ya New Bagamoyo road na Uporoto Street maeneo ya Victoria jijini Dar es salaam, kutoka mtaa wa Chato, na kinaendelea kutoa huduma zake bora kwa wananchi katika mazingira ya kisasa zaidi kila siku kwa kuanzia saa moja unusu asubuhi hadi saa mbili usiku.(Muro)

Posted On Tuesday, 19 May 2015 06:01

Mkurungezi wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, akizungumza na wataalam wanao endelea na uchimbaji wa visima vifupi katika Mradi Ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT kwa ajili wa utafiti wa mafuta na gesi kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.

Mkurungezi wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, akionyesha sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Mradi wa utafiti wa mafuta na gesi Ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.

Meneja wa Mradi wa MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT, Dkt. Amina Karega, akionyesha sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.

Na. Augustino Kasale - Kitengo Cha Mawasiliano-TPDC

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania limeanza utafiti wa mafuta na gesi eneo la Gombero, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga.

Mkurugezi wa Utafiti kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, mwishoni mwa wiki alitembelea kujionea shughuli inayo fanya na Shirika hilo.

Posted On Monday, 18 May 2015 18:27

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta (aliyesimama) akifungua Mkutano wa wafanyakazi wa Wizara hiyo mapema jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka na kulia ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Bwana Hassan Mabula.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akimshukuru Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta mara baada ya kufungua rasmi mkutano wa wafanyakazi wa wizara hiyo na taasisi zilizo chini yaka.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka mapema jana jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Posted On Tuesday, 28 April 2015 05:53

 Dk Mwele Malecela

Dk Mwele Malecela

TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imetengeneza dawa za asili zilizoboreshwa kwa ajili ya tiba kwa magonjwa mbalimbali, ikiwemo Ukimwi baada ya kuzifanyia utafiti kubaini uwezo na usalama wake.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Dk Mwele Malecela amesema iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa dawa asilia 11 ziingizwe sokoni.

Magonjwa mengine ambayo dawa hizo zilizoboreshwa zitatumika kwa ajili ya tiba ni kisukari na kupunguza mafuta (lehemu) mwilini, uvimbe wa tezi dume kwa wanaume na dawa inayoongeza nguvu za kijinsia kwa wanaume.

Posted On Thursday, 26 March 2015 05:19

DSC03176

Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.

Na Nathaniel Limu, Singida

JUMLA ya watoto 284 hadi 300, huzaliwa kila mwaka katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Singida wakiwa hawajatimiza umri wa kawaida wa kuzaliwa (njiti).

Kati ya watoto hao,inakadiriwa 60 hadi 83 hufariki kutokana na sababu mbalimbali kila mwaka ikiwemo ya tatizo la kupumua.

Posted On Sunday, 04 January 2015 04:43

NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii.

Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania.
Karibu uungane nasi

                                                                                              VICTOR SIMON

Posted On Monday, 29 December 2014 06:05

Kila tarehe 19 mwezi Novemba huwa ni maadhimisho ya siku ya choo duniani, kwa hiyo mjengwablog inasisitiza na kukumbusha umuhimu wa matumizi sahihi ya choo katika jamii ili kutunza usafi wa mazingira na kuepuka magonjwa yatokanayo na ukosefu wa vyoo bora.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu,ni Choo bora na mikono safi kwa afya bora,heshima na usawa".(Martha  Magessa)

Posted On Wednesday, 19 November 2014 09:05

Displaying 01.JPG

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Displaying 02.JPG

Mwandishi wa habari wa Redio Adhana Harith Subeit akitaka ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani kwenye mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.

Displaying 03.JPG

 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Mohd Dahoma akijibu maswali ya waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari katika mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.(Martha Magessa)

Posted On Saturday, 15 November 2014 08:32
Page 1 of 9

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi