We have 117 guests and no members online

Znateli

Mkulima (wa pili kulia) wa Shayiri katika mashamba ya Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha akiendelea na uvunaji wa Shayiri kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wameweza kuvuna hadi gunia 1o kwa hekari moja. Wakulima wa Monduli Juu wameanza kuvuna mazao yao, baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) iliyowapatia mafunzo, mikopo ya mbolea na dawa. Pia shayiri hiyo hununuliwa na TBL kwa ajili ya kutengenezea kimea katika kiwanda kilichopo Moshi,

 

Mkulima wa Shayiri Goigoi Kivuyo akionyesha sehemu ya shamba linalotarajiwa kuvunwa Shayiri eneo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha, baada ya kulima kwa kufuata maelekezo na mkopo  wa mbegu na dawa kutoka Kampuni ya TBL
Meneja wa Barley kutoka  Kiwanda cha Bia nchini (TBL) Dk. Bennie Basson akiwaonyesha waandishi wa habari hawao pichani namna Kampuni hiyo inavyowawezesha wakulima wa Shayiri katika kulima kilimo bora chenye tija.
A.I
 
Posted On Sunday, 10 August 2014 10:56

Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika banda lao
wakati wa Maonesho ya Wakulima Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Watoto waliotembelea Banda lka WQizara ya Viwanda na Biashara.

Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika banda lao wakati wa Maonesho ya Wakulima Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

(Awadh Ibrahim wa mjengwa Blog/Kwanza jamii radio)

Posted On Saturday, 09 August 2014 06:24

image

Chinisi zilizooteshwa kwa Ustadi mkubwa katika Banda la Jeshi la Magereza katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Magharibi, Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa kwanza katika Mapando Bora katika Jeshi la Magereza.

image_2

Kikombe cha Ushindi kilichokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza katika Kanda ya Magharibi, Mkoani Tabora ambapo Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Vipando Bora kwa Mwaka 2014 katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Magharibi yaliyofanyika Mkoani Tabora(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

(Awadh Ibrahim wa Mjengwa blog/Kwanza jamii).

Posted On Saturday, 09 August 2014 06:04

1 (10)

Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST ) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya makongamano  ya Wajiolojia  Afrika na  wanasayansi vijana Duniani, Profesa Abdulkarim Mruma (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu  kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika na   mkutano wa tatu  wa vijana wanasayansi  kutoka nchi mbalimbali duniani. Makongamano hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 11- 16 Agosti, 2014 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud. Wengine, kwanza kulia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Vijana wanasayansi kwa upande wa Tanzania Steven Nyagonda, Rais wa Vijana wanasayansi Duniani  Meng Wang na Katibu wa Kamati ya Maandalizi, Profesa Nelson Boniface.

2 (9)

Rais wa Wanasayansi Vijana duniani, Meng Wang (wa pili kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea kuhusu mkutano wa tatu wa wanasayansi vijana kutoka nchi mbalimbali duniani, kulia ni Mwenyekiti kongamano la vijana wanasayansi upande wa Tanzania Steven Nyagonda, wengine wanaosikiliza niMtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Katibu wa kamati ya maandalizi, Profesa Nelson Boniface.

3 (8)

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wakitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika na kongamano la tatu la wanasayansi vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani. Kushoto ni Michael Msambi mjumbe wa kamati ya maandalizi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya makongamano hayo, Profesa Abdulkarim Mruma (kulia).

Na Awadh ibrahim wa Mjengwa Blog/ Kwanza jamii radio

 

Tanzania imepata fursa ya kuwakutanisha wanasayansi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na duniani katika kongamano la 25 la Wajiolojia litakalokwenda sambamba na mkutano wa tatu wa kimataifa wa mtandao wa wanasayansi vijana.

Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya makongamano hayo, Profesa Abdulkarim Mruma, ameeleza kuwa, kongamano la Wajiolojia  litafanyika tarehe 15-16 Agosti, 2014, likijikita katika

kujadili masuala ya Jiolojia na namna Afrika inavyoweza kunufaika na taaluma hiyo kupitia sekta za nishati, madini, maji, utalii, na masuala mengine yanayohusu sekta hiyo.

Aliongeza kuwa, kutokana na mada mbalimbali zitazowasilishwa, na tafiti mbalimbali zitakazoainishwa katika kongamano hilo la wajiolojia, zitasaidia kuziwezesha nchi za Afrika kutangaza na kuhamasisha maeneo ya uwekezaji kupitia sekta za madini, mafuta, gesi ikiwemo kuendeleza masuala ya utalii na kuangalia namna inavyoweza kurithisha taaluma hiyo kwa kizazi kijacho.

“Tanzania ina masuala mengi ya kijiojia, utafiti mwingi wa kisayansi kupitia taaluma hii, umefanyika Tanzania, hivyo lazima tuiambie dunia kuhusu masuala ya kijiolojia na utalii lakini hasa kile tulichonacho hapa kwetu kwa maendeleo yetu na dunia,” aliongeza Mruma.

Aliongeza kuwa, zipo tafiti ambazo zimefanywa na kampuni mbalimbali zinazofanya utafiti wa mafuta vikiwemo vyuo vikuu mbalimbali kutoka Afrika ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa katika kongamano hilo.

Akielezea kuhusu kongamano la vijana wanasayansi litakalofanyika kuanzia tarehe 11-14 mwezi huu, Profesa Mruma alieleza kuwa, linafanyika kwa mara ya 3 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2009 na kwamba, lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba masuala ya sayansi ya dunia yanarithishwa ipasavyo katika kizazi kijacho kwa lengo la kuendeleza rasilimali asilia zikiwemo mafuta, nishati ya jotoardhi ikiwemo kuendeleza sayansi ya jiolojia kwa vijana kwa maendeleo ya Afrika na dunia.

Aliongeza kuwa, kongamano hilo litawashirikisha vijana wanasayansi kutoka katika nchi 45 Afrika na mabara mengine na litatoa fursa kwa vijana wanasayansi kujadili masuala mbalimbali ya kisayansi.

Naye Rais wa vijana wanasayansi duniani,  Meng Wang, alieleza kuwa, kongamano la vijana    ni muhimu kwa Afrika na hususani Tanzania  kutokana na kuwa ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mwingi wa masuala ya kijiolojia na masuala ya utalii.

“Mengi yanayotarajiwa kuzungumzwa katika makongamano haya yanaigusa Tanzania moja kwa moja, hii ni fursa kubwa hasa kwa vijana wanasayansi na wasio wanasayansi kutokana na kwamba jambo hili litachangia kujenga ari ya vijana kuingia katika taaluma hii”, alisisitiza Wang.

Akieleza zaidi kuhusu kongamano la vijana Mwenyekiti wa   mtandaohuo wa vijana kwa upande wa Tanzania Steven Nyagonda, alieleza vijana, waliona ipo haja ya kukutana kuangalia namna masuala mbalimbali yanayoikabili dunia kupitia taaluma ya sayansi ili kuunganisha jitihada za kizazi kilichopo na kijacho jambo ambalo litawezesha kizazi kijacho kuirithi taaluma hiyo.

Aliongeza kuwa, kongamano hilo litaangalia masuala mbalimbali ikiwemo kujadili matatizo yanayotokana na taaluma hiyo, kupata uzoefu wa namna nchi nyingine duniani zinavyotumia sekta ya nishati, namna elimu ya sayansi inavyoweza kuisaidia dunia, katika mazingira, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na masuala mengine yanayohusu dunia kupitia sayansi na jiolojia.

“Zaidi pia tunalenga kuwavutia vijana wengi wapende masomo ya sayansi hususani somo la hisabati, lakini zaidi sisi vijana wanasayansi wa Tanzania tunataka vijana wa kitanzania waipende sayansi,” alisisitiza Nyagonda.

Aliongeza kuwa, zaidi ya tafiti 400 kutoka kwa vijana wanasayansi sehemu mbalimbali duniani zimewasilishwa kwa kamati ya vijana ya dunia, ambapo kati yake tafiti 50 ziliwasilishwa na vijana wanasayansi wa watanzania.

Makongamano yote la Wajiolojia Afrika na wanasayansi vijana kutoka nchi mbalimbali duniani yanatarajiwa kufunguliwa rasmi  tarehe  11 Agosti, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Jakaya  Mrisho Kikwete.

Posted On Friday, 08 August 2014 12:15

 

o1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Goodluck Jonathan wakati muda mfupi kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani  Agosti 6, 2014

 

o4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

(A.I)

Posted On Thursday, 07 August 2014 11:00
sp
Bunge  Maalum la Katiba limepitisha azimio la mapendekezo marekebisho ya baadhi ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ili kuwezesha ili kuwezesha kijadili  Rasimu ya Katiba kwa muda  siku 60 za nyongeza  na tatu zilizobakia.
Marekebisho hayo yamepitishwa  kufuatia  Mwenyekiti wa   Kanuni na Haki za Bunge Maalum  la Katiba, Mhe. Pandu Ameir Kificho  kuwasilisha  mapendekezo ya kanuni hizo mapema leo asubuhi  katika  Bunge hilo mjini Dodoma mara baada ya kuanza kikao cha 30.
Azimio hilo,limepitishwa baada ya baadhi ya wajumbe kuchangia hoja hiyo na kuungwa mkono, ambapo uamuzi huo ulitangaza na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta.
 Mhe . Sitta alisema Bunge hilo ,litaanza kujadili rasimu ya Katiba Mpya katika kamati 12 kuanzia kesho tarehe 6 Agosti, mwaka huu kwa muda wa siku 15  yaani hadi  Agosti 27, mwaka huu.
“ Hivi sasa watumishi wa Bunge  na Sekretarieti  wanaweka nyezo zote za kupitia , ambapo pia Katibu wa Bunge Maalum la Katiba yupo nao anashughulikia suala hili pamoja na kamati ndogo ili kuwezesha kazi hii kufanyika bila buguza,” alisema Mhe. Sitta.
Aliongeza kwamba baada ya hapo kutakuwa na siku tatu  kwa kamati kukamilisha Rasimu zao za Katiba.
“ Kamati zinatakiwa kutumia sekretarieti ndogo kuandika sura wasisubiri hadi Agosti 28,mwaka huu. Tumeongeza Idadi ya wataalamu katika kila sekretarieti ndogo,” alisisitiza.
 Aidha Mhe. Sitta alisema kutokana na marekebisho ya Kanuni  ya 32 kifungu cha 2  kinachosema kamati kubadilisha sura za rasimu  na sura, hivyo zinatakiwa  kutumia muda wa siku saba kupendekeza sura mpya kuanzia Agosti  6,mwaka huu hadi Agosti 13,mwaka huu.
 Akizungumzia kuhusu maudhurio ya wajumbe wa Bunge hilo, alisema watakiwa kutia saini kwenye maudhurio hayo na hakuna kusainiana kila mtu atatia saini mwenyewe.
Mhe .Sitta akifafanua kuhusu utaratibu wa kutoa taarifa za kamati kwa vyombo vya habari alisema utatolewa.
 Alisema Bunge hilo litarejea Septemba 2, mwaka huu baada ya kukamilisha kazi za kamati.
Bunge hilo limeanza vikao vyake kwa mara nyingine  leo, baada ya kuairishwa Aprili 25, mwaka huu.
Posted On Wednesday, 06 August 2014 10:45

 

IMG-20140806-WA0003

Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi. Edith Nguruwe (katikati) akimuelekeza mwananchi aliyetembelea banda la NHC, kujaza dodoso la kufahamu uwezo na mahitaji ya nyumba kwa wananchi

 

IMG-20140806-WA0000

Afisa Mauzo, Deogratius Batakanwa na Afisa Masoko Chediel Msuya wa NHC wakiwaelimisha Maafisa wa TFDA juu ya utaratibu wa kumiliki nyumba za NHC. Maafisa hao walifika katika banda la maonyesho la NHC kufahamu shughuli za Shirika la Nyumba na utaratibu wa manunuzi ya nyumba.

 

IMG-20140806-WA0002

Wageni mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa maafisa wa shirika la nyumba la taifa

(A.I)

Posted On Wednesday, 06 August 2014 10:30

http://1.bp.blogspot.com/-jtoYCNqINKc/U-DBcwqziGI/AAAAAAACJeQ/G5yA-aLD76g/s1600/10.jpg

Ofisa Mauzo wa Vifaa vya Kilimo wa Kampuni ya Balton Tanzania, Moses Lembris (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi wa jijini Arusha, waliofika katika Banda la kampuni hiyo, kwenye maonesho na Sikukuu ya Wakulima Nane Nane, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Themi jijini Arusha

 

Mtaalamu wa Kilimo wa kampuni ya Balton, Jane Remmy, (kushoto) akitoa maelezo ya jinsi ya kuotesha miche mboga mboga kwa baadhi ya wananchi, waliofika kwenye banda la maonesho ya Nane nane jijini Arusha leo.
Sufiani mafoto naye hakuwa mbali kupata ujuzi wa kilimo katika banda hilo.
Chanzo full shangwe.
A.I
Posted On Tuesday, 05 August 2014 16:24

 

20140805_101820_1ff2d.jpg

Naibu waziri wa sayansi na Tekinolojia Mh. Makame Mbarawa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mtandao uliounganisha vyuo na taasisi za elimu ya juu nchini uliofanyika katika chuo kikuu huria cha Tanzania leo tar 5,mwez 8 mwaka 2014.

20140805_102402_ca9f9.jpg

Meza kuu naibu waziri wa sayansi na tekinolojia Mh. Makame Mbarawa wa pili kutoka kulia akiwa na mwakilishi kutoka benki ya dunia Bw. Mkahiga Kaboizo pamoja na makamu mkuu wa chuo kikuu huria wakati wa uzinduzi wa mtandao uliounganisha vyuo na taasisi za elimu ya juu nchini uliofanyika katika chuo kikuu huria cha Tanzania leo 

20140805_103140_5bd96.jpg

 

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba kutoka kwa naibu wazili Mh. makame Mbarawa hayupo pichani. Picha zote na (Awadh Ibrahim wa Mjengwa Blog/kwanza jamii)

Posted On Tuesday, 05 August 2014 12:06

Gari_f91ae.jpg

Wakati Watanzania wanalala na kubaki kulalama kuwa maisha magumu, huku wakiwaza namna ya kufika peponi bila kufa,

Posted On Saturday, 02 August 2014 06:55

 

20140704_114713

Tanzania imekuwa moja ya nchi nne Afrika iliyotunukiwa tuzo ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga duniani (ICAO) kutokana na mchango wake mkubwa katika ukuaji na usalama wa anga katika bara la Afrika.

 

Tuzo hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini Dakar, Senegal na Rais wa ICAO, Dk. Bernard Aliu katika kikao cha 24 cha Kamisheni ya usafiri wa anga afrika.

 

Pichani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, John Chacha akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Rais wa ICAO, Dk. Aliu

A.I

 

Posted On Sunday, 27 July 2014 14:20
Page 8 of 29

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart