We have 111 guests and no members online

Znateli

index

 

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya kimataifa ya utalii yanayojulikana kama Swahili Tuorism Expo yanayotarajiwa kufanyika Dar es Salaam Oktoba mwaka huu.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Razaro Nyalandu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam alipozindua rasmi tovuti ya taarifa za maonyesho hayo inayojulikana kama Swahili Tourism Expo (S!TE).
 
Maonyesho hayo yatakayohusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali kama Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na washirika wengine katika sekta hiyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 1 mpaka 4 Oktoba, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
 
Waziri Nyalandu alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kupanua wigo wa sekta ya utalii ambapo nchi zote za ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Sudan zinatarajiwa kushiriki lakini pia mataifa mbalimbali yataalikwa.
 
Alisema tayari 50% ya nafasi za maonyesho zimeshachukuliwa na kwamba mialiko kwa mataifa mbalimbali imeshatumwa ambapo ofisi yake itafuatilia kwa karibu mialiko hiyo na kuhakikisha nchi nyingi kwa kadri inavyowezekana zinashiriki.
 
“Kutokana na ukubwa wa tukio hili Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi lakini pamoja na TTB kupewa jukumu la kuratibu pia ofisi yangu itachukua jukumu la kipekee  kufuatilia mialiko iliyotumwa nchi mbalimbali kuhakikisha zinashiriki,” alisema Waziri.
 
Aliongeza kuwa maonyesho hayo yanatarajiwa kuongeza biashara ya kitalii nchini ambapo baada ya hapo Tanzania inatarajiwa kupokea watalii zaidi ya milioni 2 kwani maonyesho hayo yataitangaza nchi husika kwa kiasi kikubwa.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Balozi Charles Sanga alisema maonyesho hayo yatakuwa chachu ya kukuza utalii wa ndani na kuwajengea tabia watanzania kutembelea vivutio tulivyonavyo.
 
Alisema tumekuwa tukipokea watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kujionea utajiri wa maliasili tulizonazo lakini idadi ya watalii wazalendo imekuwa ndogo sana ambapo pamoja na mambo mengine muamko na taarifa za vivutio hivi zimekuwa haziwafikii na hivyo maonesho hayo yatakuwa chachu ya kuongeza idadi ya watalii wa ndani.
 
“Maonyesho kama haya ni maarufu katika nchi za wenzetu na yamekuwa yanawasaidia sana katika kukuza sekta zao za utalii hivyo nasi tunaanza na litakuwa linafanyika kila mwaka,”
 
“Kupitia maonyesho haya sekta na biashara nyingi za kitalii zitapanuka lakini kubwa zaidi tunaamini baada ya hapo watanzania wengi watakuwa na taarifa za kutosha kuhusu maliasili tulizonazo na watahamasika na hatimaye kuongeza idadi ya watalii wa ndani ya nchi,” alisema Balozi Sanga.
 
Wizara ya Maliasili kupitia TTB imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa na mchango wa kipekee katika pato la taifa ambapo pamoja na maonyesho hayo pia ina mikataba mbalimbali ya matangazo na nchi mbalimbali duniani katika kuhakikisha taarifa za vivutio vyetu zinawafikia watu wengi zaidi.(A.I)
Posted On Monday, 30 June 2014 14:29

Bandari ya Mombasa

Bandari ya Mombasa

Mashirika 25 yanayohudumu kazi katika Bandari ya Mombasa leo yanatia saini mkataba wa ushirikiano unaolenga kupunguza hasara ya mabilioni ya dola itokanayo na urasimu katika Bandari hiyo.

Sherehe za kusainiwa kwa mkataba huo zitaongozwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kumekuwa na utaratibu mrefu wa kusafirisha na kupokea bidhaa kutoka bandari ya Mombasa inayotegemewa na nchi za Afrika Mashariki na kati, hususan kwa shehena za mizigo kutoka mataifa ya ng'ambo.

Mkataba huo unaazimia kupunguza siku za ukaguzi wa shehena zinzoingia na kutoka kwenye bandarini hiyo, na kupunguza malalamiko ya wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kupitia bandari ya Mombasa.CHANZO BBC,(A.I).

Posted On Monday, 30 June 2014 08:31

1_70575.jpg

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (MP) (right) and the Tanzanian Ambassador in France H.E. Mrs. Begum Taj listening to officials from the French Development Agency recently in Paris. 

2_86531.jpg

Division Manager of the French Development Agency Mr. Jean-Luc Francois (left) and Project Manager of Biodiversity Agriculture and Rural Development of the French Development Agency Ms. Karen Collin de Verdiere speaking to Tanzanian delegation recently in Paris.(A.I)

Posted On Monday, 16 June 2014 07:34

120516100157 maggots 304x171 bbc nocredit f8087

Na Hudugu Ng'amilo

Je unaweza kula nyama ya mifugo waliolishwa Funza? Kufuga Nguruwe, Kuku, Samaki kwa kuwalisha funza, kunatarajiwa kubadili tunavyo fuga mifugo.
Haya hufanyika katika sehemu moja ya kufanyia majaribio inayomilikiwa na kampuni ya AgriProtein nchini Africa Kusini.

Posted On Monday, 09 June 2014 14:31

tanzania-rig-640x360_3431b.jpg

Kampuni tano zimepanda dau la kutaka kununua leseni za kutafuta mafuta na gesi katika himaya ya Tanzania.

Hata hivyo idadi hiyo ni ndogo zaidi kuliko vitalu vinane vilivyokuwa vikinadiwa katika duru hii, TPDC imeeleza.

Tanzania, ambayo imegundua kiasi kikubwa cha gesi ya asili katika mikoa ya kusini, ilitangaza vitalu saba vya maji marefu baharini na kimoja katika Ziwa Tanganyika.

Kampuni ya CNOOC Ltd na Gazprom inayoendeshwa na serikali ya Urusi ni miongoni mwa makampuni makubwa ya kigeni yaliyowasilisha maombi yao katika mzunguko huo wa nne.

Miamba mingine ya nishati Statoil na ExxonMobil, ambayo imegundua kiasi kikubwa cha gesi Tanzania, iliwasilisha maombi ya pamoja kupata kitalu kimoja.

"Mchakato wa kutathmini utaanza mara moja na tutatangaza washindi wa mnada haraka iwezekanavyo kadri muundo wa ushughulikiaji wa leseni unavyoruhusu," Yona Killagane, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) aliieleza Reuters.

Killagane hakusema lini washindi watatangazwa. Muda wa mwisho kuwasilisha maombi ilikuwa Mei 15.(E.L)

Posted On Thursday, 22 May 2014 10:42

131027133116_ethiopia_304x171__nocredit_e11f6.jpg

Dola bilioni nne za kimarekani kwa miundo msingi Ethiopia

131027133822_ethiopia_512x288__nocredit_414f8.jpg

Ethiopia inajitahidi kuimarisha miundo mbinu

140404081241_ethiopias_economy_304x171__nocredit_7686b.jpg

Changamoto hazikosekani katika kukuwa kwa uchumi huo

 

Miaka thelathini baada ya Ethiopia kukabiliwa na njaa iliyowauwa raia wengi, nchi hio ambayo ilitambulika kwa umaskini wa kukithiri sasa imeimarika na kuwa moja wapo ya nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika.

Ethiopia sasa imeanzisha mradi wa maendeleo wa kuboresha miundo mbinu ili kuinua maisha ya watu millioni 90 wa nchi hiyo.

Uchumi wa Ethiopia umeimarika katika kipindi cha miaka saba iliyopita huku shirika la fedha duniani, IMF likisema viwango vya ukuaji vimeongezeka kwa asilimia saba kila mwaka.

Na ni katika sekta ya ujenzi ambapo ukuaji huo umeshuhudiwa zaidi.

Maendeleo nchini

Ujenzi wa majumba makubwa, maeneo ya burudani na nyumba za wapangaji umeongezeka pakubwa.

Aidha ujenzi wa miundo msingi pia umetiliwa maanani.
Mwaka huu pekee, serikali ya Ethiopia imetenga takriban dola bilioni nne za kimarekani kwa ajili ya ujenzi huo.

Waziri wa fedha nchini humo, Sufian Ahmed anasema serikali itaendelea kuwekeza katika barabara na reli.

Tayari ujenzi wa reli katika mji mkuu wa Addis Ababa, umeanza na unatarajiwa kukamilishwa mwaka ujao.

Mradi huo utagharimu takribani dola milioni mia tano.

Changamoto

Licha ya hatua hizo, viwango vya umaskini ni vikubwa Ethiopia na serikali imeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa katika kupambana na mfumuko wa bei za bidha muhimu.

Ni suala ambalo waziri Ahmed anasema serikali inalitilia maanani.

Licha ya Ethiopia kukabiliwa na changamoto hizo, inasema imo katika mkondo wa kuwa taifa lenye utajiri wa kadri kufikia mwaka wa 2025.BBC,(A.I)

Posted On Wednesday, 21 May 2014 10:10

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa tatu kulia) akikata utepe kuzinduwa maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania leo jijini Dar es Salaam yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa tatu kulia) akikata utepe kuzinduwa maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania leo jijini Dar es Salaam yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, akizungumza na wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania kabla ya kuyafungua rasmi maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yameanza leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, akizungumza na wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania kabla ya kuyafungua rasmi maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yameanza leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.

Bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania zikioneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania.

 Bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania zikioneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania.

Posted On Saturday, 17 May 2014 20:18

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=146087d7908dbe46&attid=0.4&disp=inline&realattid=73604d45ca4f4fa0_0.6&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8d76iqYSkyIl6GfJbE8oEh&sadet=1400355843015&sads=46B_oZF-ZMESb2Ua7Jy_-_Eiovw

Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan wakitia saini mkataba huo wa thamnai za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=146087d7908dbe46&attid=0.9&disp=inline&realattid=73604d45ca4f4fa0_0.11&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8d76iqYSkyIl6GfJbE8oEh&sadet=1400356007529&sads=WLVYvEJJI73O0z5aI_gL1_0Lscw

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (kushoto) akimkabidhi zawadi Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) mara baada ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=146087d7908dbe46&attid=0.10&disp=inline&realattid=73604d45ca4f4fa0_0.12&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8d76iqYSkyIl6GfJbE8oEh&sadet=1400356191437&sads=MQbEpKQd-JAWQlBdNyP5vtMxcT0

Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (aliyekaa kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (aliyekaa mstari wa mbele kushoto) mara baada ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO. (FS)

Posted On Saturday, 17 May 2014 19:41
Page 9 of 29

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart