We have 60 guests and no members online

Simu

Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Tanzania Peter Zhang, akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwekezaji katika Tekinolojia ya ICT nchini.Mazungumzo hayo yalifanyika Makao makuu ya HUAWEI Tanzania jijini Dar es Salaam.

Tarehe 18 na 19 Juni 2015, ndani ya ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) uliopo mkoani Dar es Salaam, kampuni ya Huawei Tanzania itashirikiana na Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kufanya kongamano la sekta ya Teknolojia ya IT.

Kongamano hili litazungumzia teknolojia mpya ya IT ikiipa kipaumbele sekta mpya ya kuhifadhi data kwa kutumia njia ya mawingu/cloud storage. Lengo na dhumuni ya kongamano hili ni kuendelea kuwawezesha Watanzania kwa njia moja au nyingine kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

kila mmoja wetu anaelewa kua kwenye karne hii ya mawasiliano; teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimu sana hususani katika shughuli zetu za kila siku ziwe za kibinafsi au za kibiashara . Kwa kupitia teknolojia ya Habati na Mawasiliano, dunia inakua connected zaid na zaid huku viwanda vilivyopo vikihitaji revamp kuhakikisha biashara inaendeshwa efficiently and sustainability.

Posted On Monday, 08 June 2015 16:38

Makamu wa Rais wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) Kamran Khan ( wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (katikati) na wawakilishi wa makampuni 10 ya Kimarekani, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Bw. Khan aliongoza ziara ya wawakilishi hao wa makampuni ya kimarekani, Wizara ya Biashara ya Marekani na MCC ili kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini Tanzania.

Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), Wizara ya Biashara ya Marekani na makampuni 10 ya Kimarekani hivi leo wamemaliza kwa mafanikio mkubwa ziara yao ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya nishati katika nchi za Tanzania.

Ziara hii ya kwanza na ya aina yake katika historia ya miaka 11 ya MCC, ililenga kukuza mauzo ya nje ya bidhaa zinazozalishwa na makampuni ya Kimarekani na kuongeza uwepo wa makampuni hayo barani Afrika kwa kutambulisha kwayo fursa mbalimbali zilizopo za uwekezaji katika sekta ya nishati. Aidha, ziara hii ililenga kuchangia katika kufikia malengo ya Mpango Maalumu wa Serikali ya Marekani wa Kusaidia Maendeleo ya Sekta ya Nishati barani Afrika uitwao “Power Africa” unaolenga kuongeza mara mbili kiwango cha upatikanaji wa umeme katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

Posted On Sunday, 07 June 2015 17:57

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini. Kushoto kwake ni Idd Mruke, Meneja Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mkoa wa Dodoma.

Meneja wa Takwimu za Biashara na Utalii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ambaye ni Msimamizi wa Sensa ya Viwanda nchini akiwaelezea waandishi wa habari leo mkoani Dodoma kuhusu vigezo vilivyotumika katika kuchagua sampuli ya viwanda vilivyochaguliwa kufanyiwa utafiti. Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza nao leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini.

Posted On Thursday, 04 June 2015 17:22

Meneja Masoko wa Huwawei Bi Aneth Muga akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu aina ya Huwawei Met 7 ambayo zitauzwa katika Airtel Bazaar linalofanyika mlimani City ijumaa, jumamosi, na jumapili hii ikiwa na ofa ya simu ya bure aina ya 'Huwawei Kishkwambi' iliyoshikiliwa na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga. Pia simu hiyo itaunganishwa na ofa kabambe ya kifurushi cha Airtel papo hapo.

Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanahabari (hawapo pichani) simu ya kisasa ya Airtel Red itakayopatikana kwa gharama nafuu katika Airtel Bazaar litakalofanyika wiki hii ijumaa, jumamosi, na jumapili hii pale mlimani City kwa gharama nafuu huku ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha Airtel bure. Anaetazama ni Meneja Masoko wa Huwawei Bi Lydia Wangari.

Na Mwandishi wetu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ikishiriakiana na Huawei leo imetangaza kuanza Bazaar lake maalum litakalowawezeha watanzania kujipatia simu za kisasa za Smart phone na kuweza kufurahia huduma za zote za intaneti kupitia mtandao wa Airtel

Bazaar la Airtel na Huawei limepangwa kufanyika kuanzia ijumaa, jumamosi na jumapili hii kuanzia saa 3asubuhu hadi saa moja usiku katika eneo la ndani la Mlimani City na litakuwa na muendelezo hapohapo na baadae litazunguka katika maeneo mbalimbali nchini.

Posted On Thursday, 04 June 2015 17:13

1

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe (katikati) akiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kulia) wakiwasili kwenye ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha lililofanyika leo mjini Morogoro. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile.

2

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha lililofanyika leo mjini Morogoro.

3

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe akiwakaribisha wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha kwenye ufunguzi wa kikao cha kikao cha baraza hilo lililofanyika leo mjini Morogoro.

Posted On Thursday, 04 June 2015 05:29

Mwenyekiti wa Kikao cha kwanza siku ya leo katika Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Shirika hilo, Magret Ikongo akiongoza kikao hicho leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Mipango,Uwekezaji na Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Yacoub Kidula akiwasilisha mada iliyohusu mambo ya Uwekezaji, kwenye Mkutano wa tano wa Wadau NSSF unaoendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha

.

Mkurugenzi wa Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Lightness Mauki akitoa hoja kwenye Mkutano wa tano wa Wadau NSSF unaoendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Posted On Wednesday, 03 June 2015 15:51

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Equality for Growth (EfG), JaneMagigita akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.

Ofisa Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)

Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.(VICTOR)

Posted On Wednesday, 03 June 2015 15:48

On June 1, 2015, Vice President for the Millennium Challenge Corporation (MCC) Kamran Khan, speaks to journalists during the Energy Sector
Business Development Conference held at the Hyatt Kilimanjaro HOTEL IN Dar es Salaam. MCC and the U.S. Department of Commerce are hosting 10 American companies for a trade and investment mission to Tanzania to explore business opportunities in the energy sector.

On June 1, 2015, Vice President for the Millennium Challenge Corporation (MCC) Kamran Khan meets with Tanzanian Prime Minister Mr. Mizengo Pinda (left). Also attending the meeting where delegations from 10 American companies visiting Tanzania on a trade and investment mission.(Muro)

Posted On Wednesday, 03 June 2015 15:44

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Equality for Growth (EfG), JaneMagigita akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.

Ofisa Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)

Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo. Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.

Posted On Wednesday, 03 June 2015 15:08

Moto ukiwa unawaka katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga

Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Juni 2,2015 ndiyo kilele cha maonesho ya bidhaa za viwandani kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na shirika la Viwanda Vidogo nchini SIDO.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ndiye aliyefunga maonesho hayo yaliyodumu kwa siku 5 yakihusisha wajasiriamali 260 kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Kabla ya kufunga maonesho hayo ambayo yamefanyika mkoani Shinyanga,mkuu wa mkoa huo Ally Rufunga alitembelea mabanda mbalimbali.

Mwanafunzi Asha Hamis kutoka chuo cha VETA Shinyanga akipanda kwenye mtambo unaitwa Loader na kuonesha utaalam wake wa kufanya kazi kwa kutumia mtambo huo,baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kutembelea banda la chuo cha VETA

Mwanafunzi wa chuo cha VETA akiendesha mtambo katika viwanja vya Shycom.

Posted On Wednesday, 03 June 2015 05:48

Mhe Samuel Sitta akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi mkuu Ndg Awadh Massawe.

Mhe Samuel Sitta pia alipata fursa kuongea na wafanyakazi wa Bandari ya Tanga ambapo walieleza changamoto zinazowakabili wafanyakazi hao ikiwepo kodi inayokatwa kwenye mishahara ni kubwa ukilinganisha na kipato na Pia Mhe Sitta ameteua wajumbe wapya wa bodi ya bandari.(Muro)

Posted On Wednesday, 03 June 2015 05:48

 Meneja msaidizi wa uchangiaji wa hiari Matilda Nyallu wa mfuko wa pensheni wa (PSPF) akieleza namna ya mfuko wa Hiari unavyo kuwa na nijinsi gani utafaidika pindi unapo jiunga na kuwa mmoja wa wadau wa (PSPF)

 Kushoto Muandaaji wa sherehe ya wanawake wajasiliamali shamimu mwasha ambaye ni mdau wa (PSPF) akitoa ufafanuzi wa sherehe hiyo na kuwakaribisha wageni walioweza kuhudhuriapembeni ni mshereheshaji wa sherehe hiyo jokate mwegelo.

 Afisa wa mfuko wa pensheni wa (PSPF)kushoto Hadji Jamadary akiwa na balozi wa mfuko huo Flaviana Matata katika sherehe hiyo

Posted On Tuesday, 26 May 2015 05:48
Page 2 of 29

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi