We have 117 guests and no members online

Znateli

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameyataka makampuni yanayojihusisha na mafuta na gesi nchini, kuhakikisha yanatimiza mahitaji ya Soko la Ndani na ukanda wa Afrika Mashariki kabla ya kufikia Soko la Nje.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Utafiti na ufunguzi wa kozi ya Shahada ya Uzamili ya Mafuta na Gesi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika hotuba iliyosomwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki bado una mahitaji makubwa ya rasilimali ya gesi hususani katika viwanda na nyanja zote.

Posted On Tuesday, 19 May 2015 06:10

Sehemu ya Wawakilishi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa katika siku yao ya kwanza ya mkutano wa siku nne unaojadili juu ya mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Maendeleo Endelevu ya Maendeleo baada ya 2015. Majadiliano hayo ni moja ya eneo muhimu kueleleka ukamilishaji wa Mchakato wa Ajenda na Malengo SDGs. Mkutano huu unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Afisa Mkuu wa uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla, akizungumza wakati wa Mkutano wa pembezoni ( Side-Event) ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Uwakilishi na Asasi za Kimataifa, kwaajili ya kubadilishana mawazo kuhusu nafasi za Ki Kanda na Kitaifa katika mfumo wa ufuatiliaji na udhibiti, fursa na changamoto za Malengo ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 kwa upande wa Afrika.

Sehemu wa Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki pamoja na mambo mengine walisisitiza haja na umuhimu wa wananchi kushirikishwa kikamilifu katika eneo hilo la ufanyaji wa tathmini na ufuatiliaji kwa kile walichosema malengo hayo ya maendeleo endelevu yanawahusu wananchi hiyo ushiriki wako ni muhimu.

Posted On Tuesday, 19 May 2015 05:52

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015', wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre VVIP Room'. Mkutano huo umeanza leo Mei 18 2015 jijini Wuhan, Jiombo la Hubei.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wa nchini China, Katibu wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto) na wengine, wakati alipofungua Maonesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015', yaliyoanza leo Mei 18, 2015, Jimbo la Hubei, Jijini Wuhan nchini China.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Katibu wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015'.

Posted On Monday, 18 May 2015 18:04

Displaying 01.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (kushoto), akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) , Rished Bade (kulia) katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake, baadhi ya wafanyabiashara na watendaji kutoka taasisi mbalimbali ili kufahamiana. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu.

Displaying 02.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wateja pamoja na maofisa wa benki hiyo katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wake, baadhi ya wafanyabiashara na watendaji kutoka taasisi mbalimbali ili kufahamiana. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Displaying 03.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (katikati), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chemi Cotex, Lakshmi Narayan Rathi (kulia) katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wake, baadhi ya wafanyabiashara na watendaji kutoka taasisi mbalimbali ili kufahamiana. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu.

Posted On Monday, 18 May 2015 04:56

Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Martin Mmari, (kushoto), akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa Mfuko huo kutoka kanda ya Ziwa, Bernard Kyaduma, wakati wa hafla ya kuwapatia tuzo wafanyakazi bora wa Mfuko huo mwaka 2014.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Kam Mganga, (wapili kushoto), akitunuku cheti Mfanyakazi bora wa jumla wa Mfuko huo kwa mwaka 2014, Angelina Napacho kutoka kurugenzi ya Operesheni ya Mfuko huo, wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi bora kutoka kila idara kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumapili Mei 17, 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani, Hoseah Kashimba, na Mkurugenzi wa Fedha, Martin Mmari.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Kam Mganga, akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, William Erio.

Posted On Sunday, 17 May 2015 16:39

Afisa Kodi Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard Mwafongo akiwasilishaji kwa Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 ambapo alisema kuwa moja kati ya sababu ya kuandaa sheria hiyo ni kuongeza pato la taifa kupitia makusanyo mbalimbali wakati wa kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali leo jijini Dar es salaam.#

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akijibu hoja mbalimbali kuhusu Sheria Mpya ya Ongezeko la Thamani toka kwa wadau waliohudhuria mkutano huo na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano kuelekea upatikanaji wa sheria hiyo na hatimaye kuwezesha kuinua uchumi wa nchi.

Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akichangia kwenye moja ya maeneo ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili maboresho ya sheria hiyo.(Muro)

Posted On Thursday, 14 May 2015 20:09

Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Dk. Matern Lumbanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandimisho ya miaka 10 ya PPRA katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Laurent Shirima.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano na Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA leo jijini Dar es salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Saada Salum Mkuya anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) yatakayofanyika Mei, 19 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Dk. Matern Lumbanga, amesema lengo la maadhimisho ni kukutanisha wadau wa manunuzi ya umma nchini kujadili mafanikio katika udhibiti wa manunuzi ya umma na changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta hiyo.

Posted On Thursday, 14 May 2015 06:03

Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Bima ya UAP wakiwa na Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto) wakitenbelea kiwanda hicho kujionea shughuli za utendaji ikiwa ni pamoja na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho mara baada ya kukipatia bima ya shilingi milioni themanini (80,000,000/=) kufuatia kuunguliwa na pamba yake katika ghala la kuhifadhia lililopo kiwandani hapo.

Mwanzoni mwa mwaka huu 2015 pamba iliyokuwa imehifadhiwa kwenye moja ya maghala katika kiwanda cha pamba JIELONG Holdings Tanzania LTD iliungua na kuharibika kabisha mara baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu hali iliyosababisha pamba hiyo kuchemka na kuwaka moto.(Muro)

Posted On Thursday, 14 May 2015 06:00

Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini (Kushoto) wakiwa katika Kikao na Wataalamu wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd (Kulia). Kikao kilijadili kuhusu ushirikiano katika sekta ya nishati na kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara, Dar es Salaam.

Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Takato Nishizawa (Kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu shughuli zinazofanywa na Kampuni yake kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini (Kushoto), wakati wa Kikao kilichokutanisha pande hizo mbili Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mei 12, 2015 kwa lengo la kujadili ushirikiano katika sekta ya nishati.

Makamu Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Satoshi Uchida (Kulia), akifafanua jambo kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, wakati wa kikao baina yao kilichojadili ushirikiano katika sekta ya nishati. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Posted On Tuesday, 12 May 2015 19:17

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Kazi Maalim, Mh. Prof. Mark Mwandosya (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mkazi wa Mradi wa nyumba 13 za kisasa kwa ajili ya Wafanyakazi wa Halmashauri ya Busokelo zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu Nyangi, wakati alipotembelea mradi huo.(Muro)

Posted On Tuesday, 12 May 2015 17:18

Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (katikati)

Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (katikati)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (kulia).

BENKI ya EximTanzania imezindua kampeni inayolenga kuwahamasisha wateja wake juu ya matumizi ya kadi zake mpya za 'Faida Chip and PIN Debit card' ambazo zimeundwa kwa kuzingatia vigezo vya kiusalama zaidi.

Kwa mujibu wa Meneja Bidhaa wa benki hiyo Bw. Aloyce Maro hatua hiyo ni sehemu ya jitiahada za benki hiyo kuhakikisha kwamba huduma zake zinatolewa kwa uhakika na usalama zaidi kwa faida ya wateja wake.

Posted On Tuesday, 12 May 2015 07:21

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania. Picha zote na Mpiga Picha wetu.

Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Posted On Saturday, 09 May 2015 17:24
Page 3 of 29

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart