We have 114 guests and no members online

Znateli

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb) akibadilishana mawasiliano na baadhi ya wafanyabiashara waliowasili Visiwa vya Comoro kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro, linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Aprili, 2015. Kushoto (mwenye miwani) ni Balozi wa Tanzania Visiwa vya Comoro Bw. Chabaka Kilumanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (mwenye tai) akishiriki kucheza ngoma ya asili ya Comoro mara baada ya kuwasili visiwani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb) ahudhuria Kongamano Kubwa la Biashara kati ya Comoro na Tanzania, litakalofanyika tarehe 23 Aprili, 2015 Visiwani Comoro.

Lengo kuu la kongamano hilo ni "kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro kwa kutambua fursa zilizopo kati ya nchi hizi mbili na kurasimisha biashara ambayo kwa sasa hairatibiwi".

Kongamano hilo ambalo litawakutanisha viongozi, maafisa wandamizi wenye dhamana ya kuendeleza biashara kutoka Tanzania na Comoro pamoja na wadau wa Sekta Binafsi, litafungua rasmi fursa ya kutangaza na kuuza bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwa wafanyabiashara watakaopenda kufanya hivyo kutokana na nafasi nyingi za biashara na uwekezaji zilizopo katika Visiwa vya Comoro.

Posted On Thursday, 23 April 2015 13:40

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu (kushoto) amekutana na wafanyabiashara wa Sweden kwenye mkutano ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Sweden na Afrika Mashariki(Swedish East Africa Chamber of Commerce).

Sehemu ya Wafanyabiara hao wa nchini Sweden wakiwa kwenye kikao na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu.

Sehemu ya Wafanyabiara hao wa nchini Sweden wakiwa kwenye kikao na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu.(Muro)

Posted On Thursday, 23 April 2015 07:54

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda akifungua kongamano kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.

Baadhi ya wajummbe kutoka nchini Korea ya Kusini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati alipokuwa fungua kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.

Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia mjadala wakati wa kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.

Posted On Thursday, 23 April 2015 06:41

Mkwawa

Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa (CCM) kupitia mkoa mpya wa Njombe ,Hassan Mkwawa akizungumza na mwandishi wa habari David John.

MJUMBE wa mkutano mkuu Taifa (CCM) kupitia mkoa mpya wa Njombe ,Hassan Mkwawa amesema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu watanzania watarajie mabadiliko makubwa ya viongozi na hasa wabunge , kwani kutakuwa na sura nyingi za vijana.

Amesema vijana wengi wameonesha nia na kiu kubwa ya kutaka mabadiliko hivyo kutokana na hali hiyo kutakuwa na changamoto za kutosha kutoka kwa vijana.

Kauli ya mjumbe huyo ameitoa jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na mtazamo wake juu ya uchaguzi wa mwaka huu.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 16:17

images

Mahmoud Ahmad Arusha

SERIKALI imesemasema kuwa imeridhishwa na maonyesho ya madini ya vito yaliyoandaliwa na jumuia ya wafanyabiashara wa madini nchini Tamida,kutokana na kuonyesha mafanikio makubwa yakiongozwa na madini ya Tanzanite.

Waziri wa Nishati na Madini,George Simba Chawene,ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua maonyesho ya nne ya madini ya vito yanayoshirikisha wauzaji, wanunuzi wakubwa wa madini hayo ulimwenguni .

Chawene,amesema kuwa hivi sasa serikali ipo katika hatua za uimarishaji wa kiutengenezaji madini ukataji wake na uchongaji hivyo kuyauza yakiwa yameongezewa thamani na kutoa ajira nyingi tofauti na awali ambapo yalikuwa hayatoi ajira hizo kutokana na kuuzwa yakiwa ghafi.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 16:15

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Afrika ya Kati na Kusini (ESAURP),Profesa Teddy Maliyamkono akifanya mahojiano mafupi na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa kuwajengea uwezo sekta biashara zisizo rasmi iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wadau na Wanahabari wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati kuhuisha biashara zao ili kupata huduma za kibenki iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Ufundi wa FSDT, Sosthenes Kewe alizungumza mbele ya wadau na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati kuhuisha biashara zao ili kupata huduma za kibenki,Bwa.Kewe amesema kuwa taasisi yake imesaidia mradi huu kwa kuwa unaendana na kazi yao ya kuwezesha wajasiriamali wadogo na wakati na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi, kutengeneza ajira na kupanua vyanzo vya kodi.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 16:00

hc1

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.

hc2

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.(Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 15:53

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wapili kulia), akimkabidhi tuzo, Makamu wa Rais wa kampuni ya Acacia, (Anayeshughulikia kampuni), Deo Mwanyika, baada ya mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni hiyo, kuibuka mshindi wa jumla wa mwaka 2014 wa tuzo ya Rais ya makampuni ya uchimbaji madini, yanavyotekeleza wajibu wa kampuni katika kusaidia jamii (CSRE). Hafla ya kutoa tuzo hizo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa muongozo mpya wa makampuni hayo katika kutekeleza CSRE. Aanayeshuhudia ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene

Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo, wakipiga makofi

Makamu wa Rais, akimkabidhi tuzo, Meneja Ustawi wa Kampuni wa Mgodi wa North Mara, Abel Yiga, baada ya mgodi huo kuwa kinara katika migodi iliyomstari wa mbele katika kusaidia jamii, Kulia ni waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.(Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 15:40

MZ1

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Tanzania – China Promotion Centre, Bw. Xian Ding. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MZ01

WAziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. (Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 08:12

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (Katikati) akiwa na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, CEO wa TTCL Dr. Kamugisha Kazaura wakiweka sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini.

Afisa Mtendaji Mkuu WA Mfuko WA Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (Kulia) akitia sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini pamoja na CEO WA TTCL Dr. Kamugisha Kazaura.

Afisa Mtendaji Mkuu WA Mfuko WA Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (WA pili kulia) akibidilishana mawazo na Waziri WA Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa baada ya kutia sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 06:57

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mfuko wa LAPF, Yesaya Mwakifulefule (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Christina Mndeme, msaada wa rangi zenye thamani ya sh. milioni 3 kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa maabara katika shule za Ulanga Mashariki.(Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 06:48

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akitoa maelezo ya jinsi Tanzania inavyoboresha uchumi wake kwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa (IMF)kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh wa katikati. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na ujumbe wa shirikala fedha la kimataifa (hawapo kwenye picha ). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akizungumza katika mkutano huo wa Changamoto za Milenia/Chamber of Commerce uliofanyika mjini Washington DC. Aliyeko nyuma ya Mhe Waziri ni Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 06:37
Page 5 of 29

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart