We have 120 guests and no members online

Znateli

ndugai31_fa5e9.jpg

Naibu spika Job Ndugai

WABUNGE wameitaka Serikali kuharakisha mazungumzo yake kuhusu tatizo lililopo la mgomo wa wafanyabiashara nchi nzima, ili suala hilo lipatiwe ufumbuzi mapema.

Hayo yalibainishwa bungeni hapo na Naibu Spika Job Ndugai, wakati wakati akijibu miongozo mbalimbali iliyoombwa na wabunge kuhusu suala hilo ambao wengi wao walitaka mijadala ya Bunge hilo iahirishwe ili suala hilo lijadiliwe kama dharura.

Hata hivyo, Ndugai alisema kutokana na hali halisi iliyopo sasa ni muhimu mazungumzo hayo yakaendeshwa kwa haraka ili kufikia mwafaka na kupata ufumbuzi wa mgogoro uliopo.

Posted On Wednesday, 01 April 2015 03:28

Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Harrison Mwakyembe akihutubia wajumbe wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaofanyika Mjini Addis Ababa –Ethiopia.

Naibu Katibu Mkuu –Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nd. Armantius C.Msole (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua wakifuatilia hotuba ya Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr.Harrison Mwakyembe (Hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango wa Afrika unaofanyika Mjini Addis ababa – Ethiopia.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua akipata maelezo kuhusu utaratibu wa Mkutano kutoka kwa kamishina msaidizi wa Fedha za nje Bi.Judica Omari baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaoendelea Mjini Addis Ababa – Ethiopia. Katikati ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa.(Muro)

Posted On Tuesday, 31 March 2015 07:40

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akizungumza wakati wa kukabidhi Ripoti yake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Akimkabidhidhi Ripoti yake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad(kushoto)ikulu jijjini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika

Posted On Friday, 27 March 2015 16:43

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akipeperusha bendera kuashiria kuanza kwa safari za treni ya kisasa katika Kituo cha Reli Dar es Salaam jana huku Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakishuhudia. (Na Mpigapicha Wetu).

Raisi wa Burundi Pierre Nkurunzinza akipeperusha bendera kuashiria kuanza kwa safari za treni ya kisasa katika kituo cha Reli cha Dar es salaam jana huku Raisi Jakaya kikwete  na viongozi wengine wa nchi za Afrika mashariki wakishuhudia.

TRENI nne za kisasa za mizigo mali ya Shirika la Reli nchini (TRL) zinazokwenda nchi nne za Ukanda wa Kati zimezinduliwa jana jioni Dar es Salaam kwenda kwenye nchi hizo, tukio lililoshuhudiwa na marais na wawakilishi wa nchi husika.

Nchi hizo ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda na Uganda ambapo mwenyeji wao Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete aliongozana nao kuzindua treni hizo, ikiwa ni moja ya mikakati ya kuendeleza Ukanda wa Kati.

Uzinduzi wa treni hizo, ulitanguliwa na mkutano wa marais hao waliokutana jana jijini Dar es Salaam, kuzungumzia masuala mbalimbali ya uwekezaji kwenye ukanda huo.

Posted On Thursday, 26 March 2015 05:04

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi 'SimBanking' kupitia kwa mawakala wa 'FahariHuduma'.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama 'Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo', Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.

Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.

"Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,".

Akielezea namna ya kushiriki na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.

Posted On Friday, 30 January 2015 04:33

 

Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Mkuu wa Kongane ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe (Kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory).

Mtaalamu wa Masuala ya Forodha kutoka TRA, Bw. Stambuli Myovela (Kulia) akizungumza wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Posted On Monday, 26 January 2015 11:26

bei-petroli_7ba43.jpg

BEI ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, imeshuka kuanzia leo, huku watumiaji wa petroli wakipata nafuu zaidi kutokana na kuuzwa chini ya Sh 2,000 baada ya kipindi cha muda mrefu.

Kutokana na kushuka kwa bei ambako pia kunachangiwa na kushuka kwa bei katika soko la dunia, sasa petroli itauzwa lita moja kwa Sh 1,955, dizeli itakuwa Sh 1,846 kwa kila lita moja na mafuta ya taa yatakuwa yanauzwa kwa Sh 1,833 kwa kila lita moja.(MM)

Posted On Wednesday, 07 January 2015 08:48

Displaying 01.jpg

Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.

Displaying 03.jpg

Baadi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia suala la mfumuko wa bei nchini.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)(Martha Magessa)

Posted On Monday, 10 November 2014 07:53

 Captain Sagar Chavda ambaye ndiye Muongozaji wa Ndege  Kutoka Dar es salaam kuelekea Entebe

 Jean Uku Commercial Manager akiwa anaongea na wateja wa Fastjet

 Kushoto ni Jean Uku Commercial Manager wa Fastjet na Jimy Kibati General Manager wa Fastjet wakizindua Rasmi safari za Kwenda Entebe kutokea Dar es  salaam.(P.T)

Posted On Thursday, 25 September 2014 03:51

pix 1-day 2

Wadau wa madini ya vito kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakipatiwa huduma katika Banda la Tanzania katika Maonesho ya 54 ya Kimataifa ya Vito na Usonara – Bangkok, Thailand.

pix 6-day 2

Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Latifah Abdallah akitoa maelezo kuhusu madini hayo kwa wadau waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok.

pix 8-day 2

Baadhi ya Washiriki kutoka Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok wakipozi kwa picha muda mfupi kabla ya kuanza  kwa siku ya tatu ya maonesho hayo. Kutoka Kushoto ni Asimwe Kafrika, Iddi Pazzi, Gregory Kibusi, Nelson Magawa, Teddy Goliama na Matiko Sanawa.

Posted On Friday, 12 September 2014 04:52

Displaying 589hotel.pic 5 (2).jpg

Moses Mashalla

Mahakama kuu nchini kitengo cha biashara kanda ya Arusha imemuamuru mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa ndani ya hoteli hiyo.(Martha Magessa)

Posted On Monday, 25 August 2014 05:50

Picha TANSORT

Imeelezwa kuwa Tanzania inatarajia kuwa kitovu kikuu cha madini ya vito barani Afrika baada ya kubainika kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya vito.
Hayo yalisemwa na mtaalamu wa madini ya vito na almasi kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi (TANSORT) kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini Teddy Goliama kwenye semina iliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Afisa Madini Wakazi na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini inayoendelea mjini Bagamoyo
Goliama alisema Tanzania kupendekezwa kuwa kitovu kikuu cha madini ya tanzanite ni matunda ya ziara iliyofanywa na Kitengo cha TANSORT kwa kushirikisha wataalamu wa wizara ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika maonesho ya kimataifa ya vito ya Thailand yajulikanayo kama Bangkok Gem and Jewellery Fair
Alisema sababu zilizopelekea Tanzania kupendekezwa kuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito Afrika ni kutokana na wingi na aina mbalimbali za madini hayo pamoja na madini hayo kupendwa na wafanyabiashara wengi kutoka Thailand na nchi nyinginezo duniani.
Alisema awali Waziri Mkuu wa Thailand aliitembelea nchi ya Tanzania na kukutana na Serikali pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini na kukubaliana maeneo ya kushirikiana ambapo aliahidi kuisaidia Tanzania katika kukuza biashara ya madini ya vito.
Goliama aliendelea kusema kuwa Waziri Mkuu huyo aliikaribisha Tanzania kutembelea Thailand pamoja na kukutana na wataalamu wa sekta wa madini wa nchi hiyo ambapo ujumbe wa wataalamu wa madini ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Mh. Stephen Maselle ulitembelea nchi ya Thailand na kukutana na uongozi wa chama cha wafanyabishara wa madini Thailand unaoshirikiana na Serikali ya Thailand bega kwa bega.
Alisema kuwa moja ya mikakati ya kukuza biashara ya madini ya vito iliyowekwa ilikuwa ni kutoa fursa kwa nchi ya Tanzania kushiriki katika maonesho ya kimataifa ya Bangkok Gem and Jewellery Fair ambayo hufanyika mara mbili kwa mwaka, Februari na Septemba.
Alisisitiza kuwa mara baada ya Tanzania kufanya vizuri katika maonesho hayo na kubainika kuwa na hazina kubwa ya madini ya vito ilipendekezwa kuwa kitovu cha biashara ya madini hayo barani Afrika.
“ Mpaka sasa kwa bara la Afrika hakuna kituo cha biashara ya madini ya vito, maonesho ya Arusha Gem Fair yamekuwa yakitumika kama njia ya kuwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali barani Afrika.’’ Alisisitiza Goliama
Aliendelea kusisitiza kuwa Tanzania imeweka mkakati wa kuboresha maonesho yao kuwa ya kimataifa zaidi barani Afrika na kukutanisha wafanyabiashara kutoka mabara mengine duniani pamoja na kuwa kituo kikuu cha madini barani Afrika.
Akizungumzia mchango wa biashara ya madini ya vito nchini Thailand, Goliama alisema kuwa biashara hiyo ni ya tatu katika kuchangia pato la nchi ya Thailand.
Wakati huo huo akizungumzia biashara ya madini ya vito inavyofanyika mtaalamu mwingine kutoka TANSORT Sanawa Matiko alisema kuwa biashara ya madini ya vito mara nyigi inafanyika kwenye maonesho ikihusisha kukutanisha wafanyabiashara yaani wauzaji na wanunuzi wa madini hayo.
“ Maonesho hayo hutumika kama njia moja wapo ya kujenga mtandao wa kibiashara pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika madini ya vito nchini’’ alisema Matiko
Matiko aliendeTANZANIAea kusema kuwa mara nyingi maonesho ya kimataifa hutumika kwa wafanyabishara kupata taarifa mpya (updates) za biashara ya madini ya vito pamoja na vifaa vya kisasa kwa ajili ya madini ya vito vilivyogunduliwa na taasisi zinazotengeneza vifaa hivyo.
Akizungumzia biashara ya madini kwa upande wa Tanzania Matiko alisema Tanzania inatakiwa kutumia heshima kubwa iliyopewa kwa kutangaza zaidi madini yake hususan ya vito ndani na nje ya nchi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi.

 

A.I

Posted On Friday, 15 August 2014 10:46
Page 7 of 29

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart