We have 69 guests and no members online

Simu

NEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani kutoka kundi la Young Money Records, Nick Minaj, amefanikiwa kumtoa kaka yake, Jelani Miraj, kifungoni baada ya kulipa dola 100,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 200.

Jelani alipelekwa jela kutokana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12, ambapo alianza kukitumikia kifungo tangu Aprili mwaka huu, lakini msanii huyo alifanikiwa kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kaka yake.

Nick amekuwa akifanya makubwa kwa kaka yake ambapo kabla ya kwenda jela, Nick alitoa mchango wa harusi ya kaka yake huyo wenye thamani ya dola 30,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 60.

Hata hivyo, msanii huyo alizidi kuonyesha upendo wa dhati kwa kaka yake ambapo alimpa nyumba kwa ajili ya kuishi na mke wake mara baada ya kufunga ndoa.(VICTOR)

Posted On Saturday, 12 December 2015 07:37

International Labour Organization (ILO) has announced today that the National Capstone Conference in Tanzania will take place on the 7th of May at the Julius Nyerere International Convention Centre aiming to showcase the success of The Youth Entrepreneurship Facility (YEF) and its partners over the past five years and celebrate the achievements with its young beneficiaries and partners.

Since its inception, the YEF has unleashed entrepreneurial potential of more than 30,000 emerging and existing entrepreneurs through the business development training, supported the start- up and growth of 17,000 businesses and the creation of 40,000 jobs for young people, by far exceeding the initial outreach and impact targets.

Speaking about the upcoming conference ILO Tanzania Country Director, Mr. Alexio Musindo, said the program will be closing in June 2015 and the Capstone Conference in Tanzania will present results from country-level activities, and investments on skills and entrepreneurship; on improving the productivity of young people, and on sustainable business models and offshoots that are expected to carry forward some activities of the project.

'The Conference will be a platform to convene a variety of 300 stakeholders, partners and beneficiaries who are committed to entrepreneurship, promoting policies and programs to enhance employment, especially among youth' said Mr. Jealous Chirove, Chief Technical Advisor.

Conference participants will include policy makers; representatives from different ministries ( e.g. Ministry of Labour and Employment; Ministry of Information, Youth ,Culture and Sports; Ministry of Education and Vocational Training); representatives from donor community ; private sector, industry representatives; civil society youth serving-organizations; researchers; and YEF beneficiaries among many others. These include;

· promoting a culture of entrepreneurship

· integrating entrepreneurship in education system

· increasing the evidence base on what works on youth employment

· facilitating youth led organizations to implement innovative solutions to youth entrepreneurship

· facilitating access to business development services and finance for young people

The participants especially the project partners will be expected to make presentations and facilitate discussions based on specific initiatives implemented in collaboration with the project.

The Guest of Honour is expected to be the Hon. Minster of Labour and Employment, Ms. Gaudencia Kabaka.(Muro)

Posted On Tuesday, 05 May 2015 13:48

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .

Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.

Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali.CHANZO:BBC (Muro)

Posted On Tuesday, 05 May 2015 13:23

John Kerry azuru Mogadishu

Rais wa Somalia

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewasili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo anakutana na rais Hassan Sheikh Mohamud,viongozi wa eneo la Afrika mashariki pamoja na mashirika ya kijamii.

Ni waziri wa kwanza wa kigeni kutoka Marekani kuutembelea mji huo.

Kerry hataondoka katika uwanja wa ndege wa mji huo unaolindwa sana.

Posted On Tuesday, 05 May 2015 13:14

Shambulizi la Texas

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wamekiri kwamba ndio waliotekeleza shambulizi katika shindano la vibonzo vya kumkejeli mtume Mohammed katika jimbo la Texas nchini Marekani.

Kundi hilo limesema kuwa wapiganaji wawili wa kundi hilo walitekeleza shambulizi hilo katika mkutano uliokuwa karibu na mji wa Dallas.

Taarifa ya habari ya Redio ya kundi hilo Al-Bayan imesema kuwa maonyesho hayo yalikuwa yakionyesha picha mbaya kumhusu mtume Muhammad.

Washukiwa wote wawili walipigwa risasi baada ya kufyatua risasi katika maonyesho hayo siku ya jumapili.CHANZO:BBC (Muro)

Posted On Tuesday, 05 May 2015 13:10

Waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu

Polisi nchini Israel wakiwa juu ya Farasi wamekabiliana na waandamanaji kutoka makundi ya Wayahudi wenye asili ya Ethiopia ambao wanadai kubaguliwa na Polisi wa taifa hilo.

Katika maandamano hayo yalitokea Tel Aviv, Polisi walitumia mabomu ya machozi na maguruneti kuwatawanya mamia ya waandamanaji hao. Watu kadhaa wamejeruhiwa wakiwemo maafisa wa Polisi 20. Wayahudi wenye asili ya Ethiopia waliitisha maandamano kufuatia picha za video zilizosamabaa wiki iliyopita ambazo zinaonyesha askari wenye sare wenye asili ya Ethioppia wakiteswa na Polisi. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa wito kurejesha hali ya Amani na kuahidi kuwa polisi watafuatilia tuhuma hizo na kuzifanyia uchunguzi wa kina.CHANZO:BBC (Muro)

Posted On Monday, 04 May 2015 04:22

Wanajeshi wa nchini Nepal wakiwa wamebeba misaada kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi

Kwa Msaada wa mtandao.

Serikali ya Nepal imejitetea dhidi ya malalamiko juu ya misaada ya dharura, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Jumamosi nchini humo.

Mkuu wa masuala ya dharura wa Nepal,Rameshwor Dangal,ameambia BBC serikali inajitahidi iwezavyo, lakini mkasa huo ulikumba majimbo 20 nchini humo na hivyo mahitaji ni mengi sana ndiposasa serikali inaelemewa.

Hali ya kutamauka imewakumba wengi waliothiriwa na tetemeko hilo,na wengine wameonesha malalamiko yao kwa kulumbana na polisi huko Kathmandu, mji mkuu wa taifa hilo.

Posted On Wednesday, 29 April 2015 17:49

wahamiaji haramu

Utafiti mpya wa kituo cha Uingereza British Think-Tank unasema kuwa Biashara ya binaadamu ni tatizo kubwa linalokumba muungano wa ulaya .

Watafiti katika kituo hicho kinachoshughulikia masuala ya haki za jamii wanasema mafanikio katika vita dhidi ya kile walichokitaja kama biashara ya utumwa mambo leo yamezorota na kwamba mipaka iliyowazi pamoja na internet vimechangia biashara ya binadamu kuwa rahisi.

Ripoti hiyo imeelezea namna maelfu ya wanaume na wanawake na watoto wananavyouzwa kwenye mipaka na magenge na kulazimishwa kufanya kazi za ngono ,utumwa na uhalifu .

Imetoa wito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja za nchi za muungano wa ulaya kukabiliana na tatizo.CHANZO:BBC (Muro)

Posted On Thursday, 23 April 2015 10:02

Wahamiaji wanaoelekea Italy

Mkuu wa utawala wa waasi nchini Libya ameiambia BBC kuwa vikosi vyao vinafanya juhudi ziwezekanazo kuzuia wahamiaji haramu kuabiri meli kuelekea Ulaya .

Khalifa Al-Ghwell - ambaye serikali yake ya uokozi yenye makao yake mjini Tripoli haitambuliwi kimataifa anasema walinzi wa Libya wa mwambao wamekuwa wakiwashikilia karibu wahamiaji mia nne - kutoka nchi za Sahara barani Afrika katika kipindi cha siku chache zilizopita .

Bwana Ghwell amesema kuwa wahamiaji elfu 17 walikuwa wanaishi katika kambi ya hifadhi nchini Libya , lakini ni asilimia karibu tano walioweza kuvuka na kuingia Ulaya.CHANZO:BBC (Muro)

Posted On Thursday, 23 April 2015 10:00

Ndege ya jeshi la Saudi Arabia ikipaa kwenda kushambulia Yemen

Iran imeutaja uamuzi wa Saudi Arabia wa kusitisha mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen, kuwa hatua iliyo nzuri.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Java Zarif , alisema kuwa hatua hiyo inastahili kufuatiwa na mazungumzo pamoja na msaada wa dharura wa kibinadamu.

Msemaji wa muunganmo unaoongozwa na Saudi Arabia, alisema kuwa kwa sasa lengo ni kupatikana kwa suluhu la kisiasa kwa mzozo ulio nchini Yemen, lakini hata hivyo hakusema ikiwa nguvu za kijeshi hazitatumika.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 11:07

Waandamanaji wanaotaka demokrasia mjini Hong Kong

Serikali ya Hong Kong imetangaza mapendekezo kukusu kuchaguliwa kwa kiongozi wa eneo hilo mwaka 2017.

Licha ya kushuhudiwa maandamano barabarani ya kuitisha demokrasia zaidi na mazungumzo ya muda mrefu mipango hiyo inasalia kuwa sawa na ile iliyotangazwa na China mwaka uliopita.

Wenyeji wa Hong Kong watawapigia kura wagombea lakini wagombea hao watahitajika kuidhinishwa na kamati kutoka China.

Wagombea wa nafasi hiyo ni lazima wapate uungwaji mkono wa asilimia kubwa ya kamati ya uteuzi ambayo itawajumuisha wanachama wa chama cha kikomisti.

Hata hivyo mpango huo haukubaliki na baadhi ya wapiga kura nchini Hong Kong ambao wanataka uchaguzi wa wagombea ulio huru.CHANZO:BBC (Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 10:58

Mhe Balozi wa Rwanda Profesa Mathilda Mukantabana akiwa katika pich ya pamoja na Balozi wa AU Mhe. Amina Salum Ali alipotembelea ofisi za Umoja wa Afrika uliopo Washington, DC nchini Marekani .

Balozi Profesa Mathilda anachukua uongozi wa mikutano wa mabalozi wa Afrika katika kipindi cha mwezi April hadi July 2015 akiwakilisha kanda ya Afrika Mashariki.(Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 06:34
Page 1 of 10

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi