habari

Jaku alia na vituo vya Polisi Zanzibar

on

 

Na Mwandishi wetu

Dodoma. Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM) Jaku Hashimu Ayoub amesema kwa muda mrefu askari wa jeshi la polisi Zanziabr wamekua wakifanya kazi katika mazingira yasioridhisha kutokana na uchakavu wa vituo vyua polisi mijini na vijijini.

Jaku ameyasema hayo wakati wa kikao cha Bunge Dodoma na kusema kwa mazingira ya aina hio maafisa wa jeshi la polisi wakati mwengine wamekua wakifanya kazi zao kinyume na matarajio.

Akijibu swali hilo Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema vituo vingi vimejengwa au kukarabatiwa katika miaka tofauti ikiwemo vituo vya Mwembe Madafu na Mbweni katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Vingine ni Kituo cha Mchanga Mdogo Mkoani Kaskazini Pemba, vituo vya Chwaka na Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja, Chakechake na Mtambile vilivyopo Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema ujenzi wa vituo vingi vya polisi ulikuwa ni ushirikiano kutoka kwa wananchi wa ameneo husika kufuatia kero mbali mbali wanazokabiliana nazo.

 

Hata hivyo Lugola ametolea mfano  Mkandarasi MS Albatina Construction Company Ltd anayejenga Kituo cha Polisi Mkokotoni ambaye kazi bado inaendelea.

 

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *