We have 137 guests and no members online

Image may contain: 1 person, smiling, closeup

 

Ndugu zangu,

Kwa ushindi huo wa mke wa mjomba wangu hata aje Jecha, matokeo hayafutwi!

Pichani wabunge wawili kama alivyowataja Hawa Mniga ( Pichani kulia) ni Kingunge Ngombale Mwiru aliyekaa kushoto akifuatiwa na Gibbons Mwaikambo mwenye miwani.

Hongera Sana Shangazi yangu Hawa Mniga!

Maggid.

Posted On Sunday, 10 September 2017 16:33

Image may contain: 1 person, standingNdugu zangu,

Nimemsikitikia sana ndugu yangu, Comrade George Simbachawene.

Kwa kusoma Daily News la Septemba 7, inaonyesha dhahiri kuwa akiwa amepanda kuwa Waziri Kamili wa Nishati na Madini, ndani ya siku saba ndipo makosa yanayomtaja kwenye ripoti ya Bunge yalipofanyika. 

Ni kama vile mchezaji anapoanza kucheza mechi uwanjani. Pasi za awali hutokea kuwa hazina macho. Ni mpaka pale atulie, baada ya dakika za awali kupita.

Na kubwa, makosa ya Simbachawene hayaonekani kabisa kuwa aliyafanya ili yamnufaishe yeye binafsi, tofauti na mwenzake Injinia Ngonyani ambaye, baada ya kutengeneza ushawishi kwa kampuni ya Tanzanite One kununua hisa , naye akaja kuwa Mjumbe wa Bodi wa kampuni hiyo hiyo. George Simbachawene yeye alisaini kuhamishwa kwa hisa bila kufuata taratibu. Duniani hakuna asiyefanya makosa, na ukizingatoa alikuwa mpya kama waziri Kamili, hilo lingeweza kutarajiwa. Amewajibika kwa vile limetokea katika wakati wake. Ameondoka kwa heshima ili kupisha uchunguzi.

Kwangu binafsi Simbachawene ni kiongozi mwenye kujali yaliyo na maslahi kwa wengi. Ni mchapakazi, mtu asiyependa urasimu kwa maana ya kuchelewesha mambo. 

Nilipata kuwa na kazi yenye kuhusisha TAMISEMI, nilishuhudia jinsi anavyofanyia kazi yenye maslahi kwa umma, wakati wowote ule, iwe mchana au usiku.

Nimemsikiliza mara kadhaa George Simbachawene akijenga hoja ndani ya Bunge. Binafsi, kwa kupima hoja zake, naamini kuwa Simbachawene mara zote anasimamia upande wa wengi. 

Simbachawene anayajua vema mahitaji ya wananchi wa vijijini , kule Kibakwe na kwengineko Tanzania. 

Wahenga walisema; kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. 
Ni imani yangu, kuwa Simbachawene ataendelea kuchapa kazi, na kwamba siku moja tutamwona akirudi tena kwenye nafasi ya juu kuwatumikia wananchi wengi zaidi ya wale wa jimboni kwake Kibakwe.

Maggid Mjengwa,

Dar es Salaam.

Posted On Sunday, 10 September 2017 16:31

 

Posted On Sunday, 10 September 2017 16:28

Related image

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye, ataongoza Maafisa na Askari katika zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu na kutoa heshima za mwisho (Kwa Paredi Maalum), kwa aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, ambaye alifariki dunia Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:23

Image result for miraji mtaturu

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU KUKAMATWA WAFUASI WA CHADEMA IKUNGI

Septemba 9, 2017:

Kumekuwa na taarifa potofu katika mitandao ya kijamii kuwa wafuasi 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Ikungi walikamatwa kwa kosa la kuendesha michango kwa ajili ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu aliyejeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:23

1 (2)

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia), akizungumza na Ma IGP wastaafu na makamishna wastaafu na waliopo kazini (hawapo pichani) wakati alipokutana nao leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mpango wa kubadilishana uzoefu wa kikazi pamoja na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo, kulia ni IGP mstaafu Said Mwema, wa kwanza kushoto ni IGP msataafu Ernest Mangu na IGP mstaafu Omari Mahita.

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:22

1 (1)

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles Kichere(kulia) Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:18

index

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa 10 inayolima pamba nchini wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi.

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:10

KAMATI 1

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Rashid Chuachua akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo kilichikutana kwa ajili ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Reli wa mwaka 2017, Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:09

1Baadhi ya Maafisa Waandimizi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za Kilimo kutoka wakulima kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizotolewa na Wenyeviti wa Mkutano huo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:09

IMGL3493

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa  inayolima zao la pamba nchini kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 9, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo na wanne kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Posted On Sunday, 10 September 2017 05:08

pik1

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Pikipiki za Traffic 10, Computer 100 na Baiskel za kisasa 200 kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polis Dar es Salaam na kulifanya kuwa la kisasa.

Posted On Saturday, 09 September 2017 04:21
Page 9 of 1596

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji