We have 105 guests and no members online

Ndege ya British Airways

Waziri wa uchukuzi wa ndege nchini Ghana Cecelia Dapaah amelitahadharisha shirika la ndege la Uingereza, British Airways, kwamba huenda likaadhibiwa vikali.

Hii ni baada ya kunguni kugunduliwa katika baadhi ya ndege za shirika hilo.

Gazeti moja la Uingereza wiki hii liliripoti kwamba ndege moja ya BA ilizuiwa kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London kuelekea Accra baada ya kunguni kugunduliwa wakitambaa kwenye viti vya ndege hiyo.

Gazeti la The Sun lilichapisha habari kuwa wahudumu wa ndani ya ndege hiyo walipigwa na butwaa walipowaona kunguni wengi tu ndani ya ndege na kulazimu kuahirishwa kwa safari yao.

Wahudumu hao walizua taharuki walipokurupuka nje badala ya kuwaelekeza wasafiri kuingia ndani ya ndege hiyo.

Posted On Friday, 19 January 2018 15:37

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya matibabu ya bure kwa wazee, Johaness Chacha, moja wa wazee 280waliopatiwa vitambulishbo hivyo vitakavyowawezesha kutibiwa bure popote wilayani Serengeti katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya wilaya ya Mugumu Januari 18, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegawa kadi za matibabu kwa wazee 280 wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, kadi hizo zitawawezesha wazee hao kutibiwa bure.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu bure kwa wazee walio na umri wa kuanzia miaka 60.

Posted On Friday, 19 January 2018 15:29

"hatuwezi kucha jina la nchi yetu lichafuliwa na watu wanaofanya mambo kwa maslahi yao"- Rais wa Tanzania, John Magufuli

Rais Magufuli amewaagiza Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Tanzania pamoja na Waziri wa Ujenzi na Usafirishaji wa Zanzibar kusitisha usajili wa meli mpya nchini humo 'mpaka itakapotangazwa vinginevyo'.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais wa Tanzania ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa meli zote 470 ambazo zimesajiliwa Tanzania na zinapeperusha bendera ya Tanzania.

Agizo hilo limekuja baada ya serikali ya Tanzania kufuta usajili wa meli mbili za kigeni wiki hii, baada ya taarifa ya kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha zikiwa zinapeperusha

Posted On Friday, 19 January 2018 15:22

Mtu mmoja amefariki nchini Tanzania baada ya kuigonga ndege iliokuwa ikipaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza

Ndege inayopaa katika uwanja wa ndege

Mtu mmoja amefariki nchini Tanzania baada ya 'kuigonga ndege' iliyokuwa ikipaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa wafanyakazi wa kiwanja hicho cha ndege ameieleza BBC kuwa mtu huyo alivuka mpaka na kuingia eneo la uwanja wa ndege na moja kwa moja kwenye njia ya kurukia ndege ambapo alikutana na ndege ya shirika la ndege la Fast Jet iliyokuwa inaruka kuelekea jijini Dar es salaam.

Jeshi la polisi jijini Mwanza linasema tukio hilo la aina yake lilitokea usiku majira ya saa tatu Januari 17 na baada ya kuruka rubani wa ndege iliyohusika aliwajulisha wenzake kwenye mnara wa kuongozea ndege uwanjani hapo juu ya tukio hilo.

Mbona anadaiwa kuigonga ndege?

Posted On Friday, 19 January 2018 15:17

Rais Magufuli

Rais Magufuli

Kufuatia msimamo wa Raisi wa Tanzania John Pombe Magufuli kupiga maruku michango yote katika shule nchini Tanzania wadau wa sekta ya elimu wamekuwa na maoni mbali mbali

Michango hii imekuwa ikisaidia shughuli mbali mbali za maendeleo katika shule ikiwemo kusaidia upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi sambamba na mahitaji mengine muhimu kwa shule hizo ikiwemo maji na ulizinzi

Meneja wa miradi ya haki elimu nchini Tanzania bwana Bonventure Geofrey amesema tamko hilo linashitusha kufuatia hali halisi ya shule nchini Tanzanaia kuwa zenye changamoto kubwa ikiwemo uchakavu na uhaba wa miundombinu kama vile madarasa , vyoo na maabara kwa shule za sekondari

Posted On Thursday, 18 January 2018 17:25

Takribani tani 6 za samaki aina ya Sangara wenye thamani ya shilingi milioni 24 na nyavu haramu 912 zenye thamani ya shilingi milioni 22.8 zimekamatwa kwenye shamba la Bw. Joseph Kando maarufu kama Njiwa Pori katika kijiji cha Kawekamo kata ya  Nyampande Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Akithibitisha kukamatwa kwa  samaki hao kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Bwn. Alen Agustine amesema taarifa za uwepo wa samaki hao wamepewa na raia wema.

Bwn. Augustine amefafanua kuwa samaki pamoja na nyavu hizo zimekutwa kwenye shamba hilo lililopo umbali wa kilomita 50 kutoka usawa wa Ziwa Victoria.

Posted On Thursday, 18 January 2018 17:21

Meneja huduma za Airtel money Ibrahim Malando akiongea Jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza gawio kwa wateja na mawakala wa Airtel money ambapo jumla y sh bilioni 1.7 zitatilewa kwa robo ya mwaka iliyoisha Disemba 2017 katika ni Mkurugenzi wa masoko Airtel money Tanzania Isack Nchunda  na Meneja  uhusiano wa Airtel  Tanzania Jackson  Mmbando

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel imetangaza rasmi kugawa gawio la Sh.bilioni 1.7 kwa kila robo ya mwaka kwa wateja wake wote wanaotumia Airtel Money  ikiwa ni mara ya tano kufanyika tangu ianzishwe huduma hiyo mwaka 2015.

 Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masomo Airtel  Money Isack Nchunda, amesema kuwa leo wametoa rasmi Sh, bilioni 1.7 ambayo ni riba ya robo ya mwaka iliyopita  ikiwa zoezi hilo litakuwa endelevu badala ya ule utaratibu wa mwanzowa kila  miezi sita ambapo gawio hilo la faida litawafikia moja kwa moja  walengwa ambao ni wateja pamoja na mawakala wote wanaotumia huduma hiyo ya Airtel Money hapa nchini. 

Posted On Thursday, 18 January 2018 17:08

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi kavu na Majini nchini (SUMATRA) imetangaza kuanzisha njia mpya za mzunguko wa usafirishaji wa gari za abiria (daladala).

Hayo yamebainishwa leo Januari 17, 2018 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Johansen Kahatano katika kituo cha daladala cha Mbezi Louis jijini Dar es Salaam.

 Kahatano amesema lengo la uanzishwaji wa njia hizo mpya ni kuboresha huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

 Naye Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo amewataka madereva wa daladala kutii sheria na kanuni hasa kutokatisha safari.

Posted On Thursday, 18 January 2018 17:02

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (kulia)akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Mbarawa (kushoto) alipokagua jengo jipya 'One Stop Centre' la TPA leo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' la Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) lililopo bandarini leo jijini Dar es Salaam. 

 WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kuhakikisha kazi ya kukamilisha ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' inakamilika haraka na kuanza kutoa huduma kwa mamlaka hiyo na wadau wake wote.

Posted On Thursday, 18 January 2018 16:57

Bw Dotto Rangimoto ambaye ameshinda tuzo kitengo cha ushairi

Bw Dotto Rangimoto ambaye ameshinda tuzo kitengo cha ushairi

Watanzania wawili wametangazwa washindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2017.

Wawili hao watazawadiwa $5,000 kila mmoja katika sherehe ambayo itafanyika jijini Nairobi mwezi ujao.

Dotto Rangimoto alishinda kwenye kitengo cha ushairi kwa mswada wake Mwanangu Rudi Nyumbani naye Ali Hilal Ali akashinda kitengo cha riwaya kwa mswada wake wa Mmeza Fupa.

Waziri wa habari, utamaduni na Sanaa Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amewapongeza wawili hao kwa ushindi huo na kusema ushindi wao "unachagiza juhudi za serikali kuibidhaisha lugha ya Kiswahili."

"Ushindi wa Watanzania hawa ni ushindi wa taifa kwa ujumla," amesema Dkt Mwakyembe kupitia taarifa.

Posted On Thursday, 18 January 2018 16:53

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaasa wanaume wa wilaya ya Tarime kujiepusha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuachana na kilimo cha bangi.

Alitoa kauli hiyo Jumatano, Januari 17, 2018 wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Waziri Mkuu alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kilimo cha bangi vinaitia doa wilaya hiyo, hivyo hawana budi wakaepukana navyo.

“Serikali inakemea vitendo vya ukatili, achaneni navyo. Mtu unamchapa mtoto makofi hadi anazimia, kitendo hicho hakiwezi kuvumilika na pia kinaitia doa wilaya yenu.” alisema Majaliwa.

Posted On Thursday, 18 January 2018 16:47
 Wanawake wa Kimaasai eneo la Kajiado, Kenya       

Daktari mmoja nchini Kenya amewasilisha kesi mahakamani akitaka upashaji tohara wa wanawake ambao hufahamika pia kama ukeketaji uhalalishwe.

Dkt Tatu Kamau anasema sheria inayoharamisha ukeketaji wa wanawake na wasichana inakiuka utamaduni katika jamii nyingi za Kiafrika.

kadhalika, amesema ni ubaguzi dhidi ya wanawake ikizingatiwa kwamba upashaji tohara wa wanaume unakubalika kisheria.

Daktari huyo anataka pia bodi ambayo iliundwa nchini humo kukabiliana na upashaji tohara wa wanawake ivunjiliwe mbali.

Aliwasilisha kesi hiyo katika Mahakama Kuu mjini Machakos, mbele ya jaji David Kemei.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mwezi ujao.

Posted On Thursday, 18 January 2018 16:27
Page 10 of 1653

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart