We have 92 guests and no members online

Image result for omar al bashir

Taarifa iliyotolewa na Shirika la habari la Sudan-SUNA iliripoti kwamba Rais wa Sudan Omar al-Bashir amemuondoa madarakani mkuu wake wa usalama na kumrudisha ofisa mwandamizi ambaye alisaidia kuanzisha mashauriano ya usalama na Marekani baada ya mashambulizi ya Septemba 11 yaliyotokea mjini Washington na New York nchini Marekani.

Posted On Monday, 12 February 2018 04:30

Image result for boko haram release 13 prisoners

Wanamgambo wa Boko Haram wamewaachia huru mahabusu 13 kaskazini mashariki mwa Nigeria.Walioachiwa huru ni pamoja na wasichana 10 waliotekwa nyara mwezi Juni uliopita, pamoja na wataalam watatu wa jeolojia kutoka chuo kikuu cha Maiduguri.

Posted On Sunday, 11 February 2018 15:21


Image result for Lethebo RabalagoImage result for Lethebo RabalagoNa BBC.

Muhubiri moja nchini Afrika Kusini anayejiita 'nabii' anayewapulizia wafuasi wake dawa ya kuua wadudu, doom, amepatikana na hatia ya unyanyasaji , kulingana na vyombo vya habari. Lethebo Rabalago, maarufu 'Muhubiri wa doom' alipatikana na hatia ya kukiuka sheria ya kukabiliana na wadudu ,ulisema uamuzi.

Posted On Sunday, 11 February 2018 03:45

Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Elimu Tanzania Graceana Shirima amesema ni matumaini yao kuwa fedha hizo zitatumika kwa ufanisi mkubwa na makusudio waliyoyaweka na matokeo yake yaonekane kwani kiasi kilichotolewa ni kikubwa.

Posted On Sunday, 11 February 2018 03:05

Image result for syria attacks

Mashambulizi ya anga ya Syria na Urusi katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi yamewaua raia 230 katika kipindi cha wiki iliyopita ikiwa ni miongoni mwa mashambulizi mabaya ambayo yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu wa kivita.

Posted On Saturday, 10 February 2018 16:11

Image result for ajali ya bajaji

Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha baada ya bajaji yenye namba za usajili MC 957AHQ waliyokuwa wamepanda kugongwa na gari aina ya Toyota Land Cruser namba T999 EGS maeneo ya Shele ya Msingi Mapambano jijini Dar es Salaam.

Posted On Saturday, 10 February 2018 10:12

Related image

Mwanafuni mmoja wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga nchini Kenya, ameuwawa wakati wa ugoomvi wa kwenye baa.Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya Daily Nation, makamu mkuu wa chuo hicho Prof Stephen Agong’ amesema uliibuka ugomvi kati ya baadhi ya wanafunzi kutoka chuo hicho na wahudumu wa baa katika mji wa Bondo usiku wa kuamkia Jumamosi hii,

Posted On Saturday, 10 February 2018 09:07

Image result for egypt new army operation

Jana Ijumaa Februari 9, Msemaji wa jeshi la Misri ametangaza  kuwa jeshi la nchi hiyo limezindua operesheni kabambe dhidi ya ugaidi inayoitwa "Sinai 2018". Msemaji huyo amesema operesheni hiyo itakuwa "pana" na haitahusu tu eneo la Sinai lakini pia itahusu maeneo mengine ya nchi.

Posted On Saturday, 10 February 2018 03:42

 

Image result for citizen tvImage result for inooro tv

Vituo vya runinga vya Citizen TV na Inooro Tv vimefunguliwa tena nchini Kenya baada ya kufungiwa kwa zaidi ya wiki moja. Vituo hivi viwili ndivyo vilivyokuwa vimesalia kurejeshwa hewani, baada ya KTN News na NTV kufunguliwa mapema wiki hii.

Posted On Friday, 09 February 2018 09:26

Image result for Nicolas Niyibikora in the court

Muhubiri mmoja wa Rwanda huenda akajapata mashakani mbele ya vyombo vya habari baada ya kuwaita wanawake ''chanzo cha uovu'' katika mahubiri ya redio. Muhubiri hiyo wa kanisa la Seventh Day Adventist Nicolas Niyibikora aliwambia wanawake kwamba hawapendwi na Mungu wakati wa matangazo ya idhaa ya redio ya Amazing Grace mwezi Januari akionya kuwa ''hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwa wanawake''.

Posted On Friday, 09 February 2018 06:21

Image result for UKAME MALAWI

Hali ya ukame nchini Malawi inaelezewa hivi sasa inachochea kuibuka kwa ghasia na shutuma za uchawi. Maeneo ya kusini mwa Malawi ndiyo ambayo yamekumbwa zaidi ya kipindi kikavu na hivyo kuibua ghasia za makundi dhidi ya wakazi wa baadhi ya vijiji nchini humo.  Januari 29 mwaka huu, ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Aidah Waisonina kamwe hataisahau. Yeye ni mkazi wa kijiji cha Nthambula nchini Malawi katika wilaya ya kusini ya Phalombe.

Posted On Friday, 09 February 2018 05:56

Related image

Serikali ya Burundi inakanusha vikali takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi-UNHCR kuwa ni wakimbizi wakirundi zaidi ya 430,000 wanaohitaji misaada mwaka huu.

Posted On Friday, 09 February 2018 05:46
Page 2 of 1653

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart