We have 157 guests and no members online

Donald Trump shakes hands with Dr Ronny Jackson after his annual physical exam at Walter Reed National Military Medical Center in Bethesda, Maryland, 12 January 2018
Bw Trump akimsalimia Dkt Jackson baada ya uchunguzi Ijumaa

Rais Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili kufuatia uchunguzi wa kiafya na yuko la afya nzuri, daktari wa White House amesema.

"Sina wasi wasi wowote kuhusu afya ya akili ya Trump," Ronny Jackson alisema Jumanne.

Posted On Wednesday, 17 January 2018 08:22
Fugu fish                            
Image captionFugu

Mji mmoja nchini Japan umetangaza onyo la dharura kuzuia watu kula samaki anayejulikana kama Fugu baada ya samaki huyo mwenye sumu kali kuuzwa kimakosa.

Maduka kwenye mji wa Gamagori yaliuza mifuko mitano ya Fugu bila ya kutoa maini yake ambayo yana sumu.

Posted On Tuesday, 16 January 2018 08:20

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka wa 2017 imeona jumla ya wagonjwa 64,093  kati ya hawa wagonjwa wa nje ni 60,796 na waliolazwa 3297. Wagonjwa waliolazwa 3010 waliruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri na wagonjwa 287 walipoteza maisha hii ikiwa ni  sawa na asilimia 8.7. 

Wagonjwa 225 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua ambapo wagonjwa 200 waliruhusiwa na wagonjwa  25  walifariki Dunia hii ikiwa ni sawa na asilimia 11 (wastani wa kimataifa ni asilimia 13).  Kati ya

Posted On Tuesday, 16 January 2018 08:12
Papa Francis akiwa ziarani nchini Chile,Amerika ya kusini.
Image captionPapa Francis akiwa ziarani nchini Chile,Amerika ya kusini.

Papa Farancis ameanza ziara yake nchini Chile huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea shambulizi,kufuatia tishio lililotolewa kupitia vipeperushi vilivyo tolewa katika shambulio la awali kabla ya kuanza kwa ziara hiyo.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Dunian alipokelewa kwa shangwe na zaidi katika uwanja wa Santiago mji mkuu wa nchi hiyo,ambapo waumini wa kanisa Katoliki,viongozi mbali mbali wakiongozwa na rais wa Chile Michelle Bachelet walikuwepo pia.

Posted On Tuesday, 16 January 2018 07:59

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemsaidia mama mjane Benadetha Rwendela aliedhulumiwa nyumba yake Plot No. 239 Block B Kunduchi Beach kwa kupigwa mnada na madalali kutoka kampuni ya Nkanya Ltd kinyume na taratibu kisha kuamrishwa kuondoka ndani ya siku 30.

Posted On Tuesday, 16 January 2018 07:56
David Allen Turpin (left) and Louise Anna Turpin
Image captionDavid Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.

Wazazi wawili wamekamatwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa mateka nyumbani kwao wakiwemo wengine waliofungiwa kwa vitanda vyao kwa minyororo na vifuli.

David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.

Posted On Tuesday, 16 January 2018 07:41

Mwalimu Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo Tukutane Januari Akaunti, ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla. 

 

Akizungumzia Kuhusu akaunti hii mpya ya akiba ya ‘Tukutane Januari’, Mkurugenzi Mkuu wa MCB, Bwana Ronald Manongi alisema, mteja ataweza kujiwekea akiba kidogo kidogo wakati wowote katika kipindi chote cha hadi kufikia Januari. Akaunti hii ina riba ya kuvutia ambayo mteja wetu atalipwa kila robo ya mwaka. 

 

Vilevile inamuwezesha mteja wetu kupata mkopo wa hadi asilimia 30 ya amana yake katika kipindi cha mwaka husika. Hivyo Mteja atakapoweka akiba zaidi atafaidika zaidi, na atakuwa na uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kulingana na akiba ya akaunti yake. 

 

Posted On Tuesday, 16 January 2018 07:34

Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida amehaidi kumalizia mifuko 200 ya saruji na nondo 100 ili kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kata ya Kinampanda ambayo imekosekana kwa miaka mingi.

Posted On Monday, 15 January 2018 05:30

Hatimaye Serikali imefungua Migodi ya Dhahabu ya Wachimbaji Wadogo iliyopo katika eneo la Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara baada ya kujiridhisha hali ya usalama katika migodi hiyo.

Posted On Monday, 15 January 2018 05:29

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya kikao na viongozi wa serikali pamoja na watendaji wa Tanesco, REA katika kikao cha maendeleo ya usambazaji umeme kilichofanyika ofisini kwake, Mjini Dodoma 

Posted On Monday, 15 January 2018 05:25

Rais Dkt. John Pombe Magufuli asikitishwa na hafurahishwi na mjadala wa kuongezwa kipindi cha Urais toka miaka 5 iliyowekwa kwa mujibu wa katiba hadi miaka 7.

Posted On Monday, 15 January 2018 05:22
Page 11 of 1653

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji