We have 151 guests and no members online

 

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:11

Image may contain: 6 people, people smilingSwali; Ukiwaacha Anna Abdallah ( wa tatu kutoka kushoto), Therezia Makono ( wa nne kutoka kushoto) na Getrude Mongela ( wa kwanza kulia). Wajumbe wanne waliobaki ni akina nani? 
Atakayetaja majina mawili tu na walipo pichani ana zawadi ya mwenyekiti. Na majina yaliyobaki nitawasaidia kujibu.

Maggid

 
 
Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:10

Image may contain: 6 people, people smiling

Image may contain: 1 person, smiling

Image may contain: 1 person, smiling, indoor

 

Ndugu zangu,

Nilitaka nitajiwe majina ya viongozi watatu wanawake wa enzi hizo na walipo pichani.

Inaonekana mara hii swali lilikuwa gumu sana. Hata hivyo, wajumbe wangu wawili; Rosemary Jaha na Mystica Kalunde wamekuwa hodari sana wa kupata jina la tatu, maana wengi mmewatambua Getrude Mongela na Anna Abdallah. Jina la tatu lililotajwa na Rosemary ( Picha ya pili) na Mystica ( Picha ya tatu) kwa wakati mmoja ni Theresia Shija Makono. Ni wa nne pichani kutoka kushoto baada ya Anna Abdallah. Hongera sana Rosemary na Mystica!!

Maggid.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:06

Picha hii nimeipiga Mikumi jana jioni.
Maggid,
Dar Es Salaam.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 06:11

Picha no. 1

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka China Sun Long wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika hivi karibuni. Serikali ya China kila baada ya miaka miwili inatuma madaktari wake kwa ajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:58

Image may contain: outdoor and nature

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:56

1

Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango – Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy (wa tatu kutoka kushoto, mwenye tai nyekundu) na kiongozi wa ujumbe kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza Umaskini China, Bw. Xia Gengsheng (wanne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka China na  viongozi wa Tume ya Mipango.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:50

 

Hapo kulikuwa na ajali ya lori na kontena na njia ikafungwa kupisha kulitoa hapo. Magari yote kutoka na kuelekea Iringa yalisimamishwa.
Bahati kwenye kadhia hiyo nilikutana na ndugu yangu na mwanafamilia mwenzangu kwenye media, Assah Mwambene aliyetokea Mbeya kwenda Dar. Tulipata muda mwingi wa kuzungumza.
Maggid,
Dar.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:49

PIX1

Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi akielezea jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa taasisi hiyo Profesa Godwin Mjema na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:47

01

Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud akieleza mafanikio ya Jumuiya tokea ilipoasisiwa mwaka jana katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:41

Pix 1

Naibu Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla akihutimia washiriki kutoka nchi 13 za Afrika wanaoshiriki mkutano wa masuala ya huduma ya kisaikolojia katika maelezi na makuzi ya watoto na vijana unaofanyika ukumbi wa AICC mjini Arusha.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:40

index

Mkutano wa Nane wa Bunge unatarajiwa kuanza kesho Jumanne tarehe 5 Septemba, 2017 na kumalizika tarehe 15 Septemba 2017 Mjini Dodoma. Shughuli zilizopangwa kufanyika katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:-

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:38
Page 14 of 1598

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu