We have 107 guests and no members online

6 41f64

Ili usigombane na tembo, unachotakiwa ni kupima upepo; kama unaelekea kulia, basi, pita njia ya kushoto, na kinyume chake. Pichani ni Hifadhi ya Ruaha, majuzi.

Posted On Wednesday, 03 April 2013 19:42

06 2f5aa

Niko Kwenye Mazungumzo Na Mwanafunzi Wangu Wa Zamani!
Bwana Mafungu, Chuo Cha Maendeleo Ya Wananchi, Ilula, Kilolo, Iringa, leo mchana.

Posted On Wednesday, 03 April 2013 19:16

 

Mpishi wa Bia wa kampuni hiyo, Kelvin Nkya, akiwapatia maelezo maofisa wa majeshi ya Rwanda na Ghana, kuhusu idara mbalimbali za uzalishaji walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam hivi karibuni. Maofisa hao waliongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

Posted On Wednesday, 03 April 2013 14:05

04 9a44b

Iringa, Tanzania.

Posted On Wednesday, 03 April 2013 06:17

4 c5b86


Jana nilimsindikiza mgeni wangu asiyeona na anayetoka kwenye chama cha wasiiona Sweden. Tulitembelea ofisi za chama cha wasiiona Iringa.
Kwenye kikao kile cha ajabu kwangu ni kuwa chumba kilikuwa giza. Nikamwuliza mwenyeji: kulikoni giza?
Akanijibu; Tanesco wametukatia umeme, lakini si tatizo kwetu!
Naam, tatizo lilikuwa langu ninayeona!

Posted On Wednesday, 03 April 2013 06:11

a06 f5be8


Pichani ni vijana wanaojitolea kwa nyakati tofauti kuhakikisha kuwa unafikiwa na habari na picha kwa wakati. Ikiwamo magazeti pia. T
Tuko Iringa, Akiba House, Ghrofa ya Pili Chumba namba 221, karibu sana!

( Pichani ni jana alasiri)

Posted On Wednesday, 03 April 2013 06:01

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyepoteza maisha  kutokana na  kuporomoka kwa udongo katika machimbo ya Moramu yaliyopo eneo la Moshono, Arusha.

Posted On Wednesday, 03 April 2013 03:08

PIX 4a 83b16

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akiwa ndani ya  moja ya mabasi yaliyozinduliwa kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.

PIX 5 39367

Sehemu ya magari matano ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,

Posted On Tuesday, 02 April 2013 13:19

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara, Rais Kikwete amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.

Mhe Rais pia alimueleza Mhe Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.

Alielelezea matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.ru4 1a350

 

 JK akimuongoza kuelekea kwenye chakula cha mchana  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto na mkewe Rachel Chebet katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

 

ru5 42b9a

JK akipozi na familia ya  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto.

ru31 d84c7

JK akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto

CHANZO: IKULU

Posted On Tuesday, 02 April 2013 03:45

1 14151

Mfanyakazi wa kikundi cha(TANDAMTI WOMEN GROUP) kinachojishughulisha na usafi wa mazingira,
akifanyakazi bilakuvaa vifaa maalum vya kujikinga mikononi.
PICHA NA Said Ng'amilo: Iringa.
Posted On Monday, 01 April 2013 15:47

DSC 0026 18f3e

Posted On Monday, 01 April 2013 09:57

http://1.bp.blogspot.com/-Rn65-wWtjLA/UVgVCapkkyI/AAAAAAAAE4E/YE9F6XGSJKs/s1600/changudoa+%281%29.jpg

WANAWAKE watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na
kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).

Posted On Sunday, 31 March 2013 15:26

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart