We have 108 guests and no members online

 

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia Machi 28.Picha kwa hisani ya Ikulu

Posted On Sunday, 31 March 2013 03:00

 

 images a88a6

Posted On Saturday, 30 March 2013 19:30

01 4afdc

Watoto wakicheza mchezo wakuendesha Ringi kwa kupokezana kihesa kilolo Iringa.Picha na Said Ng'amilo

Posted On Saturday, 30 March 2013 14:59

JKJ2 9c029

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri;PICHA NA IKULU

Posted On Saturday, 30 March 2013 09:35

DSCF8741 bff5e

Wananchi wa mji wa Njombe wakipata huduma ya maji kutoka katika chanzo kisicho hifadhika

Picha na Said Ng'amilo

Posted On Saturday, 30 March 2013 09:13

10 707e1

Posted On Saturday, 30 March 2013 08:04

4 ee4e4


Mjengwablog na Kwanzajamii tuko kazini kama kawaida. Ofisi zetu ziko Akiba House, Iringa , ghorofa ya tatu, chumba nr 221. Niko kibaruani asubuhi hi,i na alasiri hii nitaichukua familia yangu kwenda mapumzikoni Ruaha National Park.

Huko kuna rafiki mwenye hotel amenipa ofa ya mapumziko na familia yangu kwa kuthamini mchango wa Mjengwablog na Kwanzajamii kwenye jamii.
Hakika, bado nchi yetu ina wengi wenye mioyo ya kizalendo na kuthamini juhudi za Watanzania wenzao. Pasaka Njema!

Posted On Saturday, 30 March 2013 08:00

08 2138e

The Citizen, leo Jumamosi.

Posted On Saturday, 30 March 2013 07:55

09 43b29

Ndugu zangu,

Jana usiku niliweza kuongea na ndugu yangu Absalom Kibanda kumtakia heri katika majira haya ya Pasaka.

Tofauti na nilivyoongea nae mara ya kwanza akiwa hospitalini usiku wa Machi 21, jana Absalom alionekana kuchangamka sana. Aliongea kwa sauti na kuonyesha umakini wake niliouzoea katika kuchambua mambo.

Absalom ameniambia pia, kuwa ameanza kusoma kama kawaida na kuwa anafuatilia habari za nyumbani kupitia mitandaoni. Inatia matumaini.

Natumia fursa hii, kwa niaba ya watembeleaji wa Mjengwablog/ Kwanzajamii, kumtakia, Absalom, Pasaka Njema na kila la kheri apone haraka.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
http://mjengwablog.co.tz/

Posted On Saturday, 30 March 2013 07:50

19 5799c

Mbunge wa ludewa Deo filikunjombe akiongea na wananchi wa kijiji cha lifuma mwambao wa ziwa nyasa wilaya ya ludewa hivi karibuni

Posted On Saturday, 30 March 2013 07:48

c1 00aedNdugu zangu,


Fikiri mtu mzima unajipitia na hamsini zako ukiwa umevalia nadhifu. Ghafla anatokea mtoto wa miaka sita anakumwagia bakuli la maji machafu. Unafanyaje?


Naam, hapo ndipo mwanadamu unatakiwa utangulize hekima na busara. Maana, kwa kawaida, katika hali kama hiyo, kwa hasira utamzabua kibao huyo mtoto.


Hapana, hupaswi kufanya hivyo hata kidogo. Unapaswa utulie kwanza kama mtu aliyemeza vipande vya barafu. Tafakari kwa kina. Utambue kuwa si bure. Huyo mtoto kuna aliyemtuma, tena si mtoto mwenziwe, bali mtu mzima kama wewe.


Na uione afadhali ya kumwagiwa bakuli la maji machafu kuliko ndoo ya matope. Jiendee zako taratibu. Na ukiweza, si vibaya ukampa pole huyo mtoto aliyekumwagia maji machafu, badala ya wewe kusubiri kupewa pole.

Na nini kingekutokea kama ungemzabua kibao mtoto huyo?


Jibu;


Ghafla ungemwona mtu mzima mwenzako, yawezekana akawa baba wa mtoto au mama wa mtoto. Na kama ni mama atakujia huku akiwa amejifunga kibwaya. Atakuuliza, imekuwaje umpige mtoto wake, na pengine utalipata na tusi la nguoni.


Na kama wewe ni mwanamme, basi, utataka kuonyesha uwanaume wako. Eti utamzabua kibao na mama mtu. Hapo sasa watakuja watu wazima wenzako. Wanaume kama wewe. Utaishia kugalagazwa kwenye matope. Kisa? Umempiga mtoto wa watu na kumdhalilisha mke wa mtu!


Naam, yameshakuwa makubwa hayo. Utatoka hapo ukiwa umechafuliwa haswa. Kile ambacho hukukijua, ni kuwa, mtoto yule aliyekumwagia bakuli la maji machafu katumwa na mtu au watu wazima kama wewe.


Ndio, mwogope mwanadamu. Anapokutafuta atakuwekea mitego mingi. Kama wewe ni mgumu kunasa, basi, atajaribu hata mtego wa kukutumia mtoto akumwagie maji machafu.


Na mwanadamu umeumbwa ili uchafuke. Lililo baya kwa mwanadamu ni kujichafua mwenyewe, lakini, siku zote kuchafuliwa kupo. Nako kuna viwango vyake. Yumkini kila siku inayokwenda kuna mwanadamu mwenzako mahali fulani atasema neno baya la kukuchafua. Ni wanadamu wenzako wasiokutakia mema.


Unapojisikia kuna aliyekuchafua, basi, jitahidi tu upasafishe mwenyewe palipochafuka. Na kama u raia mwema na mwenye adili, basi, jamii nayo imejaa raia wema. Watakusaidia kukusafisha.


Ni Neno Fupi La Usiku Huu. Pasaka Njema.


Maggid Mjengwa,


Iringa.

Posted On Friday, 29 March 2013 21:20

05 62e06

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Picha na OMR

 

Posted On Friday, 29 March 2013 19:54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart