We have 125 guests and no members online

 

 Wakati tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi, imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya

Posted On Tuesday, 26 March 2013 14:09

CGP-MINJA b81f3

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali, John Minja (waliokaa wa kwanza kulia) akiwa na wakuu wa jeshi hilo wa nchi mbalimbali barani Afrika (waliokaa) pamoja na maofisa wao (waliosimama) baada ya kufanya mkutano wa Taasisi za Urekebishaji Barani Afrika (ACSA). Wakuu hao wa taasisi hiyo walifanya mkutano wao katika Hoteli ya Sun iliyopo mjini Livingstone, nchini Zambia mwishoni mwa wiki, wakijadili masuala mbalimbali ya kuyaboresha majeshi yao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Posted On Tuesday, 26 March 2013 13:34

216772 593280447366136 1672327420 n 44217

Picha na Joseph Mwaisango- Mbeya

Posted On Tuesday, 26 March 2013 13:18

picture 1

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso Akibandika moja ya kipeperushi cha Airtel yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo AirtelYatosha inayompa mteja,  Simkadi moja, taifa moja na bei moja.

Posted On Tuesday, 26 March 2013 09:58

 

67Bibi wa mwanafunzi Mwenjuma Magalu, Amina Mohamed (kulia) akizungumza na Mhariri wa mtandao wa The Habari. Mitandao1Mwenjuma Magalu (wa kwanza kulia mstari wa pili) ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha  pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo akiwa darasani na baadhi ya wanafunzi wenzake

Na: Thehabari.com, Handeni

UTAFITI wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 umefanikisha kumrudisha shuleni mwanafunzi wa

Posted On Tuesday, 26 March 2013 09:51

6 f372e

Yalichapwa kwenye gazeti la Ngurumo enzi hizoo...

Posted On Tuesday, 26 March 2013 07:00

2 725de

United Nations Road, Dar, this morning.

Posted On Tuesday, 26 March 2013 06:26

7 ec176

Mitaa ya kati, Upanga, leo asubuhi.

Posted On Tuesday, 26 March 2013 06:22

5 9394b

Leo asubuhi nimefanya jogging kupitia hapa. Ni masalia ya kiunga cha Marehemu Mzee Tambaza. Kiko Barabara ya Umoja wa Mataifa. Sir Andy Chande, kwenye kitabu chake; Knight In Africa anaandika pia juu ya Dar es Salaam ya utotoni mwake, enzi hizo ikiitwa Mzizima.

Naye, Andy Chande alisoma Agha Khan Secondary School ( Sasa Tambaza) . Andy Chande anasema alipokuwa akitembea kwenda shuleni njiani ilikuwa ni kawaida kukutana na ngedere. Mzee Tambaza alikuwa na kiunga kikubwa, kilifika mpaka maeneo ya Maktaba Kuu ya sasa. Inasemwa pia, kuwa hata eneo la Ikulu ya Magogoni ilikuwa ndani ya kiunga cha Mzee Tambaza. Alipotoa eneo hilo kwa Serikali ya Mjerumani aliomba tu makaburi yao yasichimbuliwe. Wengine mliopokea simulizi za Dar ya enzi hizo ziwekeni jamvini ili tujifunze.

Posted On Tuesday, 26 March 2013 06:14

 

  Mwananchi

  Imebainika kuwa mmoja wa watu ambao Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (pichani)anadaiwa kutumia jina lake kutafuta kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari ya Southern mkoani Mbeya ni

Posted On Tuesday, 26 March 2013 03:37

 

8E9U2296

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakiweka maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA huko katika kijiji cha Majohe,Ukonga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wa Rais Xi Jinping wakishuhudia(picha na Freddy Maro)

Posted On Tuesday, 26 March 2013 03:09

6 ec742

Ndugu zangu,
Jana pale Neshno Stadium kulikuwa na vituko. Ilianza na MC ambaye ama alisahau, au hakujua itifaki. Akatamka; " Tunaanza na wimbo wa Taifa wa Tanzania halafu unafuata wa Morocco!".
Usahihi, kiitifaki unaanza na wimbo wa taifa wa wageni halafu unakuja wa taifa mwenyeji.Basi, bendi ya polisi baada ya kumaliza wimbo wa taifa wa Morocco ( wao walijua wanachofanya) ukafuata wimbo wetu wa taifa. Hapo kikatokea kituko, baada ya verse ya kwanza kuna umati wa Watanzania ulioanza kupiga makofi  ukidhani kuwa wimbo umekwisha!Tafsiri yake?
Kuna Watanzania leo hawaujui wimbo wao wa Taifa. Unajiuliza, je huko shuleni siku hizi watoto hawajifunzi kuimba wimbo wa Taifa? Au ndio Bongo Flava iliyochukua nafasi yake?Tutajenga vipi Umoja wa Kitaifa kama hata wengine wetu hawaujui wimbo wetu wa Taifa? Tufanyeje? Tujadili...
Maggid Mjengwa,
Dar,
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz

Posted On Monday, 25 March 2013 16:02

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart