We have 109 guests and no members online

6 0bbf6

Mwenyekiti,

Salamu nyingi saaana toka JBG!

I could not resist! Yes I cried! But Absalom is the same person I knew last two months! Amesimama!

Mungu ni Mwema!!!

Hoyce

Posted On Monday, 25 March 2013 07:19

1 aeb07

Ndugu Zangu,
 Bwana Yesu alipotembelea mto Galilaya, aliwakuta wavuvi wakivua samaki, Simoni alikuwa ni miongoni mwa wavuvi hao. Yesu akasema; " Simoni, acha kuvua samaki,nifuate ukawe mvuvi wa watu.
 
Naam, watu wengi wanaangamia kwa kukosa uelewa. Kwa kutojitambua. Wanahitaji ukombozi wa kifikra. Na siku zote, haki uinua taifa, vivyo hivyo, dhulma huangamiza taifa. Na mahala pasipo na haki, basi, hapo hapatukuwa na amani.
 
Oneni, maovu yametamalaki katika dunia tunamoishi. Siku zote, kujipendelea ndilo shina la maovu. Si tuna mifano hai.
Oneni, wale wenzetu waliokaa na wakaamua kuuza nyumba za Serikali. Na Waziri mwenye dhamana  alisimamia utekelezaji wa dhulma ile kwa Watanzania, huku naye akiwa ameshajikwapulia nyumba yake. Lililopelekea uamuzi wa hila na ghilba wa kuuza nyumba za serikali ni ubinafsi na hulka ya baadhi ya viongozi kutaka kujipendelea.  
 
Karibu wote waliouziwa au kujiuzia nyumba hizo za Serikali, nyumba za wananchi, tayari walikuwa na nyumba kabla. Siku zote, hamu inakuwa ni jambo jema, endapo binadamu ataweza kuitawala hamu/tamaa yake.Wanadamu tusipoitawala hamu yetu, tukaanza kujipendelea, kuwasahau wengine, basi, hilo huwa ndio chimbuko la maovu.
 
Hupelekea kutoelewana baina ya wanandugu, na hata kwa marafiki walioshibana. Hupelekea vurugu na machafuko katika jamii. Tunazungumzia uwepo wa upendo, haki na usawa.
 
Dini nyingi zinazungumzia umuhimu wa upendo, haki na usawa katika jamii. Iwe ni Uislamu na Ukristo vivyo hivyo.
 
” Naapa kwa zama . Hakika binadamu wote wamo katika hasara isipokuwa wale walioamini na wakafanya matendo mema. Wakahusiana na haki na wakahusiana na subira” (Koran tukufu, Surat ASWR) Biblia nayo inasema; kuwa Kaini alikuwa mtu wa kujipendelea mno, akamwua nduguye. Mfalme Saulo alijipendelea mno, akamdhulumu Daudi. Yuda alijipendelea mno, akakubali kumsaliti Yesu kwa Vipande thelathini vya fedha. Hatimaye,  akamsaliti Yesu. 
 
Na ufufuko wa Bwana Yesu utukumbushe jukumu letu la kupambana na maovu katika jamii. Utukumbushe jukumu la kusaidia kazi ya kuwakomboa kifikra wanadamu wenzetu.
Kama Bwana Yesu alivyomkumbusha Simoni kwa kumwambia; ” Simoni, acha kuvua samaki. E nenda ukawe mvuvi wa watu.
 
Ni Neno la Leo.
Pasaka Njema.
 
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam
0788 111 765
 
Posted On Monday, 25 March 2013 06:21

f4 8f5c7
Kikongo Village, Mlandizi, Kibaha, yesterday.

Posted On Monday, 25 March 2013 05:28

f1 81497
.. Unaweza kudeka pia. Pichani ni Mzenga, Kisarawe, jana asubuhi. Siku zote najisikia furaha ninapokutana na mama yangu mzazi. Kwa kiasi kikubwa sana amechangia niwe kama nilivyo. Mama yangu alifanya kazi Idara ya Kupiga Chapa ya Serikali- Government Press. Alifahamu tangu nikiwa na miaka sita tu, kuwa nilipenda sana picha na maandishi. Naye kila alipotoka kazini alikuja na makaratasi yenye picha na maandishi. Ndiye aliyenifanya niweze kusoma na kuandika hata kabla sijaanza darasa la kwanza. Na ikafika wakati akawa ananiletea gazeti la Serikali- Goverment Gazetta. Wengine hufikiri gazeti la Serikali ni Daily News, hapana, Serikali ina gazeti lake na husambazwa kwenye Idara zake Serikalini.

Posted On Monday, 25 March 2013 05:17

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akijadili na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) Asteria Mlambo pamoja na watendaji wengine umuhimu wa kufanyika mkutano wa pamoja ili kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza wakati ziara yake ya kukagua ujenzi wa barabara ya magari yaendayo kwa kasi katika barabara ya Morogoro hadi Sokoine.

Posted On Monday, 25 March 2013 03:53

 

picha no. 1

Na Frank John – Maelezo

 Watumishi wa  umma wametakiwa kuwa mfano wa kuigwa  katika kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taaluma zao hasa katika kitengo cha manunuzi ili sekta binafsi ziweze kujifunza kutoka kwao. Wito huo umetolewa hivi karibuni   na Kamishna wa Idara ya  Manunuzi ya Umma kutoka wizara ya Fedha  Dk. Fredrick Mwakibinga katika kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi lililofanyika katika ukumbi wa

Posted On Monday, 25 March 2013 03:47

 

27145 10200275027771113 2048244979 n 5ba45.. Unaweza kudeka pia. Pichani ni Mzenga, Kisarawe, leo asubuhi. Siku zote najisikia furaha ninapokutana na mama yangu mzazi. Kwa kiasi kikubwa sana amechangia niwe kama nilivyo. Mama yangu alifanya kazi Idara ya Kupiga Chapa ya Serikali- Government Press. Alifahamu tangu nikiwa na miaka sita tu, kuwa nilipenda sana picha na maandishi. Naye kila alipotoka kazini alikuja na makaratasi yenye picha na maandishi. Ndiye aliyenifanya niweze kusoma na kuandika hata kabla sijaanza darasa la kwanza. Na

Posted On Sunday, 24 March 2013 17:20

 

 

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Picha na OMR 2

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Kulia ni Mke wa Mzee Kingunge. Picha na OMR

Posted On Sunday, 24 March 2013 16:38
Baraka Frank mwenyekiti wa waendesha bodaboda Mafinga akihojiwa

 

Semu ya maegesho ya bodaboda Mafinga mbele ya stendi ya mabasi

 

Na: Gustav Chahe, Mafinga

MAGARI ya serikali yamedaiwa kuwa ni chanzo cha ajali barabarani kwa kukiuka sheria na taratibu za matumizi ya barabara.Haya yamesemwa mwenyekiti wa waendesha pikipiki (bodaboda) Mafinga Baraka Frank katika mahojiano maalumu na mtandao huu yaliyofanyika katika maegesho ya pikipiki zao maeneo ya stendi. Frank amesema madereva wa magari hayo wamekuwa wavunjaji makusudi wa sheria za barabarani kutokana na mwendo wao kuwa mkali na kutozingatia alama zilizop

Posted On Sunday, 24 March 2013 10:55

images 79c22

Wachimbaji wa madini wamekuwa wakitumia raslimali nyingi kama vile fedha, nguvu kazi na mashine ili kuweza kuchimba ardhi, kuvunja miamba na kupembua mchanga na udongo ili kupata madini ya dhahabu kwenye maeneo ya machimbo.

Kwa mfano hapa nchini Serikali imekuwa ikitoa msamaha wa mabilioni ya kodi mbalimbali kila mwaka kwa kigezo cha wawekezaji kutumia fedha nyingi katika kufanikisha upatikanaji wa madini.
Kutokana na kigezo hicho cha msamaha wa kodi pamoja na mapato kidogo yanayokusanywa na serikali kwenye sekta ya madini ukilinganisha na fedha nyingi za mauzo, imekuwa ikiwakatisha tamaa Watanzania wengi kiasi cha kutaka mikataba ivunjwe.
Watanzania wengi wanaamini kwamba madini mengi yanayochimbwa na wawekezaji yanawafaidisha tu wawekezaji na kuwaacha wananchi wakiendelea kuogelea kwenye dimbwi la umaskini.

Dhahabu hupatikana hapa nchini na ni moja ya madini yenye thamani kubwa duniani na bidhaa zote zinazotokana nayo, huuzwa kwa bei kubwa.
Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha McMaster kilichopo nchini Canada wamekuja na ugunduzi ambao unatoa picha kwamba huenda madini ya dhahabu yakatengenezwa maabara na kuachana na mtindo wa kutumia fedha nyingi kuyachimba ardhini.

Posted On Sunday, 24 March 2013 06:41
 Zitto-Kabwe-akikokota-mpira1 23190
TaifaStars ninyi ndio tumaini letu kubwa wakati huu nchi yetu imejaa changamoto nyingi na kukata tamaa. Wakati Umoja wa Taifa upo mashakani, ninyi mnatufanya tuvae na kupeperusha Bendera yetu nzuri ya Taifa. Dakika tisini uwanjani Tanzania inakuwa moja, ushindi hutupa fahari kubwa na kusahau vyama vyetu, Dini zetu, madaraja ya Maisha nk. Ingieni uwanjani Kwa ufahari mkubwa. Tupeni raha #TaifaStars #TZBrazil2014

 

Nimezungumza kwa simu na nahodha wa Timu ya Taifa, #TaifaStars Tanzania one @JumaKaseja . Morale ya Vijana wetu ipo juu sana. Wanaomba mjae uwanjani na kuwashangilia Kwa Nguvu. Kila Mtu ashike Bendera ya Taifa au Rangi za Bendera ya Taifa. Mliopo Dar msituangushe, uwanja wa Taifa ujae pomoni. #Nyumbani tushinde. Ushindi Ni lazima. Go stars Go

 

Posted On Saturday, 23 March 2013 15:52

 

 

Mwandishi Maarufu wa vitabu duniani Chinua Achebe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82. Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika kwa ujumla.Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru. Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua Achebe kuwa

Posted On Saturday, 23 March 2013 15:34

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart