We have 108 guests and no members online

100 6821 e9670

Kamera ya Mjengwa blog,imefika leo kijijini Mpanda,wilayani Mfundi na kunasa hii taswira ya watoto,wakicheza nje ya nyumba yao.

Posted On Saturday, 23 March 2013 15:00

 

                 Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Leslie Omari 

Na: Daniel Mjema, Mwananchi  Moshi.

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Leslie Omari, amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana hatia katika tuhuma zinazoangukia katika makosa ya vitendo vya ufisadi.Mbali na kifungo hicho, Mahakama pia imemwamuru mshtakiwa kuilipa Benki ya Exim Sh330 milioni, ambazo kampuni yake binafsi ya African Consulting Group (ACGL), ilikopa kwa kutumia dhamana ya jengo la

Posted On Saturday, 23 March 2013 14:42

 

1

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Adolph Mapunda akifungua mafunzo ya akina mama wajasiriamali wilayani Kilwa yaliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Posted On Friday, 22 March 2013 05:41

a5 b9bdd

Mkulima wa nyanya, Ilula. Kilolo, Iringa. Jana asubuhi.

Posted On Friday, 22 March 2013 05:31

4 f6bb4

Upendo ambaye pia ni mwanahabari alitutembelea ofisi za Mjengwablog/ Kwanza Jamii Iringa, hivi karibuni.

Posted On Friday, 22 March 2013 05:26

 

8E9U0419Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana Kinjekitile(picha na freddy Maro)

Posted On Friday, 22 March 2013 05:04

 

01 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, wakati akifungua mkutano huo wa siku tatu ulioanza leo Machi 21,2013 kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Posted On Friday, 22 March 2013 04:26

562819 10200259144094031 1989554065 n 51095

Leo amenibadilishia menu; samaki wa kupaka huyo. Haya, dada zangu akina Nuru, Mtage, Qamar na Karrima mseme eti wifi yenu hayajui mapishi! Naam, nimeingia Moro mchana huu. Moro imetulia, naipenda!

Posted On Thursday, 21 March 2013 16:10

 

OLYMPUS DIGITAL CAMERAMkurugenzi wa Usimamizi wa Mazingira wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(Nemc), Ignace Mchallo(kushoto) akimkabidhi cheti cha utunzaji bora wa mazingira Mhasibu Mkuu wa kampuni ya Great North Service, Joachim Mkao jijini Dar es Salaam jana. Picha na MpigaPicha Wetu.

KAMPUNI ya Great North Service Station imejipanga kuhakikisha inaokoa misitu hapa nchini kwa kutoa huduma ya kusambaza gesi Lpg  kwa bei rahisi kwa matumizi ya nyumbani na hotelini. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo  Bwana Robson Laseko baada ya

Posted On Thursday, 21 March 2013 14:12

 

 

Watafiti nawanasayansi nchini Tanzania wametakiwa kufanya tafiti za kiungunduzi ambazozitaleta manufaa na kusaidia jamaii ya watanzania .

Hayo yamesemana leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela(pichani juu)wakatiwa semina ya siku moja ya wagunduzi mbalimbali iliyoandaliwa kwa pamoja kati yaNIMR na Shirika la Grand Challenges la

Posted On Thursday, 21 March 2013 08:07

484345 10200253588835153 2005868033 n ebb05

Tangu enzi za Nyenzi ( Mwanzilishi wa Mitandao ya Kijamii Tanzania). Ni miaka ya 90. Baadae mimi na Nkwera tukawa tena pamoja kwenye Mtandao wa Tanzanet. Tukakutana tena kwenye Jamii Forums. Tupo pamoja kwenye Mtandao wa Mabadiliko pia. Niko nae pia kwenye Mjengwablog na Kwanzajamii! Huko kote tumekuwa tukiwasiliana, lakini jana Jumatano, kwa mara ya kwanza, tumekutana ana kwa ana! Ni watu kama kina Pd Nkwera naweza kusema kuwa wananifahamu. Na mtu kama Nkwera simtegemei kabisa anielezee mimi kama vile mtu aliyenifahamu tangu mwaka juzi. Na mimi hivyo hivyo kwa watu wa aina ya Nkwera. Naweza kabisa kusema kuwa nawafahamu.

Posted On Thursday, 21 March 2013 08:07

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart