We have 127 guests and no members online

 

 

8E9U7984

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo.Kushoto anayeangalia ni mbunge wa Ubungo John Mnyika. 8E9U7995

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Madabida,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik,Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda na kushoto ni Mbunge wa Ubungo Mhe.John Mnyika.

Posted On Wednesday, 20 March 2013 19:24

00 b30a2


Ndugu zangu,

Kwenye moja ya mashairi ya Marcelino Dos Santos wa Msumbiji ( Pichani kulia) anasema; " We Must Plant". Kwa maana ya tuna lazima ya kupanda.

Dos Santos hazungumzii kupanda mbegu za mahindi au mtama, bali kupanda fikra za kimapinduzi kwa wanajamii.

Ni Fikra zitakazowasaidia kutoka katika hali iliyopo na kwenda kwenye hali nyingine iliyo bora zaidi.

Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu;

” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndiko njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite.

Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Haya ya ya kuendekeza abrakadabra za Freemasons ni kielelezo cha Watanzania, kama ilivyokuwa kwa Babu wa Loliondo, kuamua kuacha kufikiri. Ndiyo, kuna waliojifunika vilemba vya ujinga. Wako gizani. Wanahitaji mwanga.
Ni Neno La Usiku. ( Pichani nilipokutana na Mjamaa mwenzangu, Marcelino Dos Santos, Nairobi , 2007)
Maggid Mjengwa,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz/

Posted On Wednesday, 20 March 2013 18:03

1 27047


Nyingine ni mikanganyiko inayowaacha wasomaji wakielea! Pichani ni Iringa leo asubuhi.

Posted On Wednesday, 20 March 2013 10:28

 

2 ffc7c

Gari aina ya Pick up likiwa limebeba mizigo katikati ya mji wa iringa ( Picha na Said Ngamilo)

 

 
Posted On Wednesday, 20 March 2013 06:00

 

kikwete 1316Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akifungua mkutano wa wadau wa Mawasiliano ulioandaliwa na TCRA mkoani humo kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazokabili sekta hiyo jana kikwete 1319

                         Wadau  mbalimbali Mawasiliano wakiwa katika mkutano huo

Na Mwandishi wetu,Kigoma

Mkuu wa mkoa kigoma Issa Machibya amezitaka kampuni za simu za mkononi kuweka udhibiti wa kutosha kwa mitandao yao ya simu ili kuzuia vitendo vya utapeli na uhalifu ambavyo vimechangiwa na simu hizo. Akifungua kikao cha

Posted On Wednesday, 20 March 2013 06:00

 

NO 1Mwenyekiti wa SARPCCO IGP Said Mwema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) baada ya kufungua mkutano wao wa siku mbili jijini Dar es Salaam.Mkutano huo utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Posted On Wednesday, 20 March 2013 05:50

 

DSC07005

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo Fakihi Haji Mbarouk akitoa hotuba ya makaribisho kwa waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria namba 5 ya mwaka 1985 hapo katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar.  PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Posted On Wednesday, 20 March 2013 05:44

 

Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau akifafanua jambo mbele ya wajumbwe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa daraja la Kingamboni jijini Dar es Salaam

Posted On Wednesday, 20 March 2013 05:38


4

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Prince David, mtoto wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, marehemu WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Picha na OMR

3

Picha ya Marehemu enzi za uhai wake.

Posted On Wednesday, 20 March 2013 05:33

kp18032013 1505b

Posted On Wednesday, 20 March 2013 05:30

 

n3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweha saini kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani msiba wa Askari wa Usalama Barabarani aliyegongwa na gari baada ya msafara wa Rais kupita jana WP 2942 Koplo Elikiza nyumbani kwa marehemu sehemu za Ununio,Machi 19, 2013

Posted On Wednesday, 20 March 2013 02:05

a1 ac941


"Ndugu zangu,
Hatari kubwa ninayoiona mbele yetu ni kwamba, uzalendo, utu na udugu miongoni mwetu Watanzania unaondoka kwa kasi ya ajabu, nyuma yake kumeachwa ubinafsi uliotamalaki na wenye kutanguliza zaidi maslahi- na si maslahi ya umma, ni ya binafsi.Maana, unajiuliza; ni kwa nini mtu anayekufahamu vizuri anashindwa kukuelezea kwa uhalisia jinsi anavyokufahamu. Badala yake, kwa makusudi, na kwa nia ovu, anaupotosha ukweli? Na bado atakuita  ndugu!"- Tafadhali Usininukuu.Maggid Mjengwa,
Iringa

Posted On Tuesday, 19 March 2013 15:58

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart