We have 109 guests and no members online

 

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 50, Mhandisi wa Maji wa kampuni ya DRIMA __ Gound Woter Drilling, Melkion Mhagama kwa ajili ya uchimbaji wavisima 2 vya maji katika vijiji vya Iramba na Lukole Wilayani Mpwapwa hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Nishati  na Madini, George Simbachawene, Meneja wa TBL Kanda ya Kusini, James Bokela  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa,Alexzanda Nyauringo.

Posted On Monday, 18 March 2013 13:49

 

1Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema, akiweka jiwe la Msingi katika kituo cha Polisi Mji mpya wa mabwepande, Wilaya ya kinondoni Jijini  Dar es salaamu.

Posted On Monday, 18 March 2013 13:35

 

DSC_0107Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambw aakiwakabidhi vyeti na hundi ya dolla 200 moja ya washindi wa medani ya fedha Sharon Hamis (wakwanza kushoto) na Fatma Jeddah (wapili kutoka kushoto) kutoka shule ya wasichana ya Feza

Posted On Monday, 18 March 2013 13:19

 

photo5 5a214

 

Na: Happy Lazaro- Arusha.

Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amefanikisha kukusanywa kwa Sh85 milioni katika harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana, mkoani Arusha. Harambee hiyo iliyofanyika juzi, iliandaliwa na Umoja wa Waendesha Pikipiki (Uwapa) wa Jiji la Arusha. Akizungumza katika harambee hiyo, Lowasa ambaye pia

Posted On Monday, 18 March 2013 06:48

 

 Dereva  wa daladala  ambae  jina lake  halikuweza  kupatikana mara moja akiwa ameshika panga mkononi akitoka kumkoromea dereva  mwenzake aliyetaka kumsababishia ajali kwa kumchomekea  eneo la Mshindo mjini Iringa  leo. PICHA NA MAELEZO FRANCIS GODWIN

Posted On Monday, 18 March 2013 06:36

 

IMG_0138Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa mkewe Tunu wakiwahamasisha waumini  wa kanisa katoliki la Magomeni jijini Dar es salaam kuchangia ukarabati wa kanisa lao wakati alipohudhuria ibada kwenye kanisa hilo Machi 17, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Posted On Monday, 18 March 2013 05:55

12 0ce0d


Ndugu zangu,

Mafalisayo walimshangaa Yesu, wakatamka; " Hivi ni Yesu huyu huyu mwana wa Joseph fundi Seremala!"

Naam, duniani hapa usimwangalie mtu pale alipofikia sasa kwenye safari yake. Angalia alipoanzia safari yake. Pitia kwenye nyayo zake. Ndipo hapo unaweza kupata cha kujifunza.

Ni Neno Fupi La Asubuhi Hii. Good Morning!

Maggid Mjengwa,
Iringa.

Posted On Monday, 18 March 2013 05:40

100 5691 f5252

Wakulima wa miti wakipeleka miche ya miti shambani, ni kijiji cha Igeleke tarafa ya kibengu,Mfundi hivi karibuni

Posted On Monday, 18 March 2013 02:34

kp 16032013 bc66b

Posted On Monday, 18 March 2013 02:30


620-Ipex-Excel

KITUO CHA BIASHARA, LONDON (TANZANIA TRADE CENTRE) KINAPENDA KUWAFAHAMISHA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA, KUWEZA KUFIKA KATIKA JUMBA LA MAONYESHO LA EXCEL CENTRE, LONDON, KWENYE MAONYESHO MAKUBWA YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA CHAKULA, MAONYESHO HAYO YAJULIKANAYO KAMA INTERNATIONAL FOOD FESTIVAL (IFE 2013).

KWENYE MAONYESHO HAYO, MAKAMPUNI YAPATAYO SITA (6), YANAIWAKIRISHA NCHI YETU TANZANIA.

BIDHAA ZINAZO ONYESHWA NA MAKAMPUNI KUTOKA TANZANIA NI:-
CHAI, KAHAWA, VIUNGO MBALIMBALI VYA CHAKULA, MAFUTA YA KUPIKIA, MVINYO (WINE) ZA AINA MBALIMBALI.

MADHUMUNI MAKUBWA YA MAONYESHO HAYO KWA UPANDE WA TANZANIA, NI KUTANGAZA BIDHAA ZA TANZANIA KATIKA SOKO LA KIMATAIFA, NA KUWEZA KUINGIA MIKATABA NA MAKAMPUNI YA ULAYA, KWA MFANO, TESCO, SAINSBURY, MORRISON, ASDA, NA MENGINEYO MENGI NA HATIMAYE BIDHAA ZETU KUPATA SOKO KIMATAIFA. KIINGILIO KWENYE MAONYESHO HAYO NI £30.00 .

WATANZANIA WOTE MNAKARIBISHWA KUYAUNGA MKONO MAKAMPUNI KUTOKA TANZANIA KATIKA MAONYESHO HAYO.

ASANTENI SANA.

Posted On Monday, 18 March 2013 01:57

1 f106b

Neno La Leo; Na Tuyaishi Maisha Ya Kadiri...

Ndugu zangu,

DUNIANI hakuna miujiza katika kuyafikia mafanikio. Hakuna njia za mkato pia. Ni sharti tufanye kazi kwa bidii. Tusiwe ni watu wenye kutanguliza taamaa na hata kuwadhulumu wengine. Tuyaishi maisha ya kadiri. Ni kwa kuyafanya yale yaliyo ndani ya uwezo wetu. Si kuishi kwa kufikiri wengine wanavyotaka uishi.

Maana, ni wachache duniani walioweza kufanya miujiza kama tunayoambiwa kwenye vitabu vya dini; Bwana Yesu yu miongoni mwa wachache hao. Tunasoma, kuwa Mafalisayo  walimshangaa Yesu na mafanikio yake.  Wakatamka; “ Hivi ni Yesu huyu huyu mwana wa Joseph fundi Seremala!”

Naam, mwanadamu usitazame tu  alipofikia sasa mwanadamu mwenzako kwenye safari yake. Jitahidi uangalie mwanzo  wa safari yake. Alikotokea. Ndipo hapo utayapata ya kujifunza.

Papa Francis wa Kanisa Katoliki amefikia kiwango cha juu cha mafanikio kwenye ngazi ya kanisa. Ni rahisi kumwangalia hapo alipo, lakini ni muhimu kuiangalia safari yake ilipoanzia.

Tunasoma leo, kuwa  Papa Francis ni mtu wa kadiri. Muda wote wa uhai wake amejitahidi kuishi maisha ya kadiri. Papa si mtu wa makuu. Na kule Vatican wanashangazwa hata na mavazi yake yasio gharama kubwa, ikiwamo viatu pia.

Hapa kwetu Tanzania Julius  Nyerere ni mfano wa viongozi walioishi maisha ya kadiri. Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Ni mfano wa kuigwa.

Ni Neno La Leo

Maggid Mjengwa,

Iringa

Posted On Sunday, 17 March 2013 18:13

1 7e78e

 

Ndugu zangu habari za wikiendi. Yapo mambo machache ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa na pia kuzuia upotoshaji ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu, kwako au kwa mtu mwingine.

Mojawapo ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika suala la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and privacy lawas). Tumeshuhudia kufungwa kwa gazeti za News of The World, mali ya bilionea Rupert Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika simu zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy Laws). Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama kuvamia kwa mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na hata katika mitandao hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia mbona umenitumia kitu kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba si wewe uliyefanya hivyo.

Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma. Ni ajabu gazeti kuandika jambo lisilo la kweli huku wahusika wakiwa na kila uwezo wa kumfikia yule wanayedhani kwamba ameandika na kumhoji ili kuhakiki habari. Kazi ya uhariri ni kuhakiki. Ikiwa mtu atakimbilia kuandika jambo likuhusulo ambalo hana hakika nalo na alikuwa na kila uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukuuliza lazima utajiuliza maswali mengi. Kwanza: Nini hasa lengo lake na pili ufahamu wake wa kile anachokifanya kwa maana ya taaluma yake katika kazi anayoifanya.

Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.

Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao. Hii itasaidia 1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii 2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari 3. Kuzuia mikanganganyiko isiyo ya lazima. Haya yakizingatiwa nadhani hata sintofahamu hizi za uandishi wa habari unaotokana na hisia na  vyanzo vumbi na  ufahamu mdogo wa jambo utaondoka na tutakuwa na jamii ambayo haki na uwajibikikaji wa wanahabari kwa jamii utaonekana kutendeka 

Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo. Namuombea kwa Mungu ampe unafuu mapema zaidi ili arudi katika meza yake kuendeleze harakati za kupambana na mchango wake katika kuleta maendeleo ya kweli kwa nchi yetu. Pili, pole pia kwa wote ambao kwa namna moja au nyengine walikwazwa na uzushi huo, kwa kuwa sina tatizo lolote na Bwana Kibanda na wala nisingependa lililomtokea limtokee yeye wala mtu mwengine yeyote. 

Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana. 


Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.

Asanteni sana.

Ndugu yenu, 
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.

 
Posted On Sunday, 17 March 2013 17:08

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart