We have 111 guests and no members online

01 8b64a

Mbunge wa Jimbo la Magomeni Muhamad Amour Chombo akitoa nasaha kwa wanafunzi,na pia kuwapongeza kwa kufaulu kwao kabla ya kuwazawadia sare za Skuli kwa kila mwanafunzi,huko katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.)

Posted On Sunday, 17 March 2013 04:28

 

1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi Mji mpya wa Mabwe Pande (hawapo pichani) wakati alipofika katika mji huo jana Machi 14, 2013 akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Maji inayosimamiwa na Dawasa na kutembelea katika Mtambo wa Ruvu Chini kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. Kulia ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidik. Picha na OMR

Posted On Sunday, 17 March 2013 03:57

 

1AKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwasalimia wazee katika kijiji cha mradi wa wakulima wa kupunguza umasikini cha Nanchong, jimbo la Sichuan, China, alipotembelea kijiji hicho, Machi 16, 2013. Anayemsalimia ni Ning Xiu (78). Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo)

Posted On Saturday, 16 March 2013 19:04

576692 587994357894745 2097400902 n 1f84f

Picha na Joseph Mwaisango akiwa Mbeya

Posted On Saturday, 16 March 2013 18:09

100 5766 31114

Picha ni kijijini Mapanda Wilaya ya Mfundi,kata ya Kibengu...juma la jana.

Posted On Saturday, 16 March 2013 16:29

 

1A

Tatu Mwenda Mwenyekiti wa (UVIMA) vikundi vya akina mama vilivyopo chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayosimamiwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwakaribisha viongozi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii (NHIF) waliokwenda Majohe Pugu  jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kutoa Mafunzo ya huduma, haki na wajibu wa mwanachama wa (NHIF) ambapo wanawake mbalimbali wanachama wa vikundi hivyo wamepata nafasi ya kuelimishwa kuhusu huduma hizo, Kutoka kulia ni Philomena Marijani Meneja Uragibishi (WAMA), Michael Muhando Mkurugenzi wa Tathmini na Uhai wa Mfuko na Takwimu (NHIF)  kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen Mikongoti na Tabu Likoko Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji Wanawake T AWAMA

Posted On Saturday, 16 March 2013 14:17

 

ig11MKUU wa Wilaya ya Igunga, Tabora Elibariki Kingu, amemuondoa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka na kumrejesha kwa Mwajili wake kutokana na kushindwa kwake kusimamia Mradi wa maji katika Bwawa la Bulenya. Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kingu alisema alikwisha mwandikia barua

Posted On Saturday, 16 March 2013 04:12

 

mo2Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013  akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea.(PICHA NA IKULU)

Posted On Saturday, 16 March 2013 04:07

 

picha no. 1

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiwaonyesha wadau mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bura kijitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza mara baada ya kukizindua kitabu hicho  leo katika ukumbi wa mikutano wa  ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Tume Mary Massay.PICHA NA ANNA NKINDA

Posted On Saturday, 16 March 2013 04:02

 

1KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimpa zawadi ya kinyago cha ‘Ujamaa’, Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China  na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo. (Picha na Bashir)

Posted On Saturday, 16 March 2013 03:57

6 4d065

Ndugu zangu,

Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.

Namfahamu kijana Ludovik tangu  akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi  walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini.

Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi  kwa namna fulani nimeshtushwa nazo. Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii. Amekuwa na mchango mkubwa, na hata katika miezi ya karibuni,ndiye yeye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti  kwenye Mjengwablog kila asubuhi. Akiwa Dar na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali , amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice kwa watangazaji kwenye Mjengwablog. Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti'.

Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo  na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.

 

Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana.  Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima. Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo.

Hapa chini ni maelezo niliyoyaandika kwenye ukuta wangu wa facebook, siku ile Ludovick alipopatwa na mkasa wa kuvamiwa usiku;

... Na Msaidizi Wa Mwenyekiti Naye Alitekwa Na Majambazi Jana Usiku!

"Kijana Ludovik Joseph. Tulikula wote na kuongea pale Rose Garden jana usiku. Tuliondoka kwenye saa tano usiku. Nikamfikisha mpaka kona ya Shekilango na Morogoro Road. Hapo aliniambia angepata daladala öa kumfikisha nyumbani kwake. Nilimwuliza jambo tu; " Ni salama hapa kukuacha?"
Akanijibu ni salama maana amesafiri mara kadhaa katika muda huo.

Masikini, akafikwa na balaa la kutekwa na majambazi kwenye bajaji. Nilikofikia Dar nikaamshwa saa kumi za usiku. Mlinzi akaniambia kuna ndugu yako amekuja na teksi hata nguo hana. Amebaki na nguo ya ndani tu. Amekabwa na majambazi.

Nikamsaidia Ludovik. Na kwa vile yeye ni Yanga, basi, nikahakikisha nampa suruali na jezi ya Simba!

Naam, iko siku, kila mtu ataishabikia Simba!

Pichani Ludovick akisimulia mkasa uliomkuta kwa Mwanzo Millinga na Joseph Kulangwa. Ndugu yangu Kulangwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Habari Leo."

 

 

Posted On Friday, 15 March 2013 21:20

DSC06973Vespa yenye namba za usajili Z728 CB,iliokuwa ikiendeshwa na Muhidini Ali Ame mkaazi wa Nyerere ikiwa imepondana baada ya kupata ajali ya kugongana na Gari aina ya Toyota ya Nungwi katika Barabara ya Amani Daraja bovu Zanzibar. PICHA NA MAKAME MSHENGA

Posted On Friday, 15 March 2013 13:40

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart