We have 146 guests and no members online

DSCF2178 3f4ce

Mkurugenzi  wa TMF ndugu Ernest Sungura na mkuu wa kitengo  cha ruzuku ndugu Alex Kanyambo leo wametembelea ofisi za Ikolo Investments LTD yalipo makao ya Mjengwa Blog na Kwanzajamii.com,Mkoani Iringa

Posted On Friday, 15 March 2013 08:53

 

mo19

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na mmoja wa wahadhiri Profesa Juma Mikidadi Mtupa (aliyeketi) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro, Mama Mwantumu Malale, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Hamza Mustafa Njozi na wadau baada ya kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.

Posted On Friday, 15 March 2013 02:22

Jakaya-Kikwete 2e088 

 

Mzee Kitwana Suleiman Kondo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF);Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro; Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro; Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro; Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na Jumuiya mliohudhuria; Wageni waalikwa; Mabibi na Mabwana;-

Niruhusuni niungane na wenzangu walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa. Nakushukuru sana Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na viongozi wenzako kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya ufunguzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Mmenipa heshima kubwa ya kuwa sehemu ya historia ya Chuo hiki. Kwa kweli, nimefarijika sana kuona Chuo chetu kinazidi kupata mafanikio ya kutia moyo hasa ukizingatia ukweli kwamba kina muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake. Ndugu Mkuu wa

Posted On Thursday, 14 March 2013 14:27

 

 3Na: Gladness Mushi-Arusha

 IMEELEZWA kuwa endapo kama Wamkiliki wa shule binafsi  wataweza kusaidia jamii za watoto yatima na wanaotokea katika mazingira magumu katika shule zao basi watachangia kwa kiwango kikubwa sana kupunguza tatizo la watoto wa mitaani. Asilimia kubwa ya watoto wanaokimbilia mitaani wanakwena huko kwa kuwa baadhi ya familia zao hazina uwezo wa kuwasaidia katika masuala ya elimu hali ambayo nayo kwa wakati mwingine inasababisha wimbi la watoto hao. Kauli hiyo imetolewa na  Bi  Isabela Daniel ambaye ni

Posted On Thursday, 14 March 2013 13:59

 

PIX 1.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi nchini (TSIA), Athuman Maige (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Isaya Maiseli. Viongozi hao walikutana na waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya chama hicho na wizara.

Posted On Thursday, 14 March 2013 13:32

000000000ttttttt dec9f

Argentine Cardinal Jorge Mario Bergoglio has greeted crowds in Rome's St Peter's Square after his election as the Catholic Church's new Pope.

Appearing on a balcony over the square, he asked the faithful to pray for him. Cheers erupted as he gave a blessing.

The first Latin American and the first Jesuit to be pontiff, he will call himself Francis I.

An hour earlier, white smoke from the Sistine Chapel chimney announced the new Pope's election.

Pope Francis, 76, replaces Benedict XVI, who resigned last month at the age of 85, saying he was not strong enough to lead the Church.

Posted On Wednesday, 13 March 2013 19:53

Photo: Neno La Leo; Mwenye Akili Ya Darasani Yumkini  Punguani Wa Mtaani!
Ndugu zangu,
Nimepata kuandika, kuwa Delirium ni hali ya mwanadamu kuwa katika mkanganyiko ( kuchanganyikiwa). Ni maradhi.
Tunayoyashuhudia sasa ni dalili za kuwa tumo kwenye hali ya Mkanganyiko- Delirium.
 
Katika dunia hii fasihi imetusaidia sana kutujengea uwezo wa kuyapembua mambo. Kuchagua kati ya chuya na mchele.
Wengine elimu yao ni ya darasani tu, mitaani humu tunamoishi haiwasaidii.  Ni kama punguani tu.
Leo katika Tanzania hii kuna watu wanakwenda kuombewa ili wenye kuwadai wayasahau madeni yao. Ni kuchanganyikiwa.
Na tatizo ni hili. Mwanadamu huyu akisimama mtaani na kutamka kwa sauti kuwa anamwomba Mungu wa mbinguni amsaidie anayemdai asahau deni lake, basi, sisi tunaopita njia tutamtazama na kuambiana; " Mwendawazimu yule!".
Lakini, ' mwendawazimu' yule akikusanyika na wengine  wakafika hamsini, na mbele akasimama  anayefanya maombezi, ambaye kimsingi anafanya kazi kama ya ' waganga' wa kienyeji, akitamka; " Nawaombea kwa Mungu enyi mnaodaiwa na NBC au CRDB, Mungu   awasaidie wenye kuwadai wasayasahau madeni yao!"
Hapo tunaopita njia tutaambiana; " Aisee, pale kuna muhubiri anayewaombea wenye kudaiwa wadai wao wayasahau madeni yao!"
Kumbe, lile ni kusanyiko tu la wenye kuota ndoto za mchana. Wenye kuota kuwa NBC au CRDB itayasahau madeni yao waliyokopa.  Na watatokea wengine wenye kutoa ushuhuda wa kusamehewa madeni yao na NBC na CRDB.
Kwenye kitabu cha ' Things Fall Apart' hata Unoka, baba yake Okonkwo anayesemwa kuwa alikuwa dhaifu na mtu ambaye Okwonkwo hakupenda afanane naye, alikuwa na cha kutufundisha. 
Kuwa kwa mwanadamu anayedaiwa lazima atambue kuwa anadaiwa. Kama umekopa ni sharti ulikubali deni lako. Ndio uungwana.
Anayekudai hawezi kirahisi kusahau deni lake. Wakati wewe utaomba kwa Mungu asahau deni lake, naye pia ataomba kwa Mungu huyo huyo deni lake ulilipe!
Wenye kudai kuwa wanaweza kuwaombea wanadamu wengine ili wenye kuwadai wayasahau madeni yao, hao kimsingi wanajipatia fedha kirahisi kutoka kwa wenye kudaiwa. 
Na wengine wenye kudaiwa elimu zao ni za darasani tu, mitaani ni punguani!
Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa.
<a href=

 

Ndugu zangu,

Nimepata kuandika, kuwa Delirium ni hali ya mwanadamu kuwa katika mkanganyiko ( kuchanganyikiwa). Ni maradhi.

Tunayoyashuhudia sasa ni dalili za kuwa tumo kwenye hali ya Mkanganyiko- Delirium.

Katika dunia hii fasihi imetusaidia sana kutujengea uwezo wa kuyapembua mambo. Kuchagua kati ya chuya na mchele.

Wengine elimu yao ni ya darasani tu, mitaani humu tunamoishi haiwasaidii. Ni kama punguani tu.

Posted On Wednesday, 13 March 2013 17:06

Photo: Nimemkuta Kamanda John Akiwa Kazini...!
Maktaba ya Iringa International School, leo asubuhi.

Maktaba ya Iringa International School, leo asubuhi.

 

 

Posted On Wednesday, 13 March 2013 16:49

000mmmmmllll b23fa

Mhe. Jaji Engera Mmari Kileo, akizungumzia  uzoefu wa  Majaji Wanawake wa Tanzania katika kukabiliana na  tatizo la  matumizi mabaya  ya mamlaka kudhalilisha kijinsia na kushawishi rushwa ya mapenzi  ( sextortion) wakati Chama cha Majaji   Wanawake- Tawi la Tanzania  kilipoanda mkutano wa pembezoni ( side-event) sambamba na   mkutano unaoendelea wa 57 wa Kamisheni ya  Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya  Wanawake ( CSW). aliyekaa kati kati ya  Jaji Kileo, na  Naibu Mwakilishi wa Kudumu  Balozi Ramadhan Mwinyi ni,  Bw. John Hendra aliyewahi kuwa Mratibu wa UNDP nchini Tanzania,  Bw. Hendra ndiye aliyekuwa mwendashaji wa mkutano huo, bado anakumbuka vizuri kiswahili, kwa sasa ni Katibu Mkuu Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa   Sera na Mipango katika Taasisi ya UN- Women

Posted On Wednesday, 13 March 2013 15:51

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekipongeza kituo cha utamaduni cha Bujora kwa kutunza na kuhifadhi  utamaduni wa mtanzania unaolitambulisha kabila la wasukuma jambo litakalosaidia kizazi kijacho kuweza kujifunza utamaduni huo.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo (WAMA) ametoa pongezi hizo hivi karibuni alipokitembelea kituo hicho kilichopo wilayani Magu katika mkoa wa Mwanza.

 

Posted On Wednesday, 13 March 2013 15:45

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi (katikati) kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya EU na wizara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Posted On Wednesday, 13 March 2013 15:38

9 e4bc6

Mpendwa Mjengwa,
Ikiwezekana naomba utangaze kwa watu wa Iringa, Mufindi, na ndugu zao, habari zinazosikitisha kwamba Dk Alison Redmayne (Semugongolwa kwa jina la Kihehe), ambaye alikuwa ni mtafiti na mwanahistoria wa mambo ya Kihehe na majirani yao, rafiki na msaidizi wa wanavijiji na wanamji wengi, amefariki dunia hivi karibuni, tarehe 20 Februari, hospitalini Oxford akiwa anauma na ugonjwa wa kansa aina ya "lymphoma". Alizaliwa 1 Oktoba 1936 na amekufa akiwa na miaka 76.

Atazikwa leo Jumatano tarehe 13 huko Oxford.

Watu wengi watamkumbuka Alison/Semugongolwa, wakubwa na wadogo, wazee na vijana, na kifo chake ni hasara kwa sisi sote.

Nashukuru sana.
Dk Martin Walsh
Cambridge

Posted On Wednesday, 13 March 2013 14:25

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart