We have 125 guests and no members online

ki1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo  leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili, atakumbukwa kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia amefundisha nyota wengi wa  kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard, Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa Stars kutokea Yanga na Pan.

Posted On Monday, 11 March 2013 17:27

Picture 1

Mshindi wa pili wa tuzo za Mwanamakuka bi  Leila Mwambungu  (katikati) akifurahi kwa pamoja  na Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kulia)  wakati wa kukabidhiwa   mfano wa hundi ya shillingi million tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa  tuzo za mwanamakuka . Akishuhudia kushoto ni  Mke wa makamu wa raisi Asha Bilali na wa pili kushoto ni mwenyekiti  wa Unit of women Friends Esther Wakati.

Posted On Monday, 11 March 2013 13:40

Mkaguzi wa dawa wa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya kati, Dk.Engelbert Mbekenga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya msako unaoendelea wa kukamata bidhaa zilizokwisha muda wake wa kutumika na zile zilizopigwa marufuku kutumiwa.

Posted On Monday, 11 March 2013 12:40

100 5472 efd92

Imeandikwa na Albert Sanga, Iringa

Miezi kadhaa iliyopita kupitia Redio TBC Taifa, ofisa mmoja wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliulizwa swali hili, "Je, inawezekana watu binafsi kufungua mashamba ya miti na kufanya biashara ya kuuza miti ya mbao?" Ofisa huyo alijibu hivi, "...inaruhusiwa...hata mimi najilaumu kuwa miaka ile wakati tunapanda msitu wa serikali kule Mufindi mimi sikukumbuka kutafuta maeneo kwa wenyeji nikapanda miti. Kama ningefanya hivyo nadhani leo na mimi ningekuwa milionea". Mahojiano yale....SOMA ZAIDI

Posted On Monday, 11 March 2013 09:02

2 dd66e

" Only if Ezinma was a boy! ( Chinua Achebe, Things Fall Apart)

Ndugu zangu,

Leo ni siku yangu ya kuzaliwa. Nawashukuru wote mlionitumia salamu za kunitakia heri, pia nyote mnaoendelea kunitakia heri. Ahsanteni sana.

Wahenga walisema; Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Nitasimulia kidogo ya utoto wangu; Wazazi wangu wamechangia sana kunifanya niwe hivi nilivyo sasa. Kwa baba yangu, watoto wote tulikuwa sawa, hata dada zangu walikuwa muhimu kwake.

Tofauti na Okwonkwo kwenye Things Fall Apart ambaye hakuridhika kwa kumpata mwana aitwaye Nwoye ambaye alifanana kitabia na baba yake Okonkwo. Huyu Okonkwo hakumpenda baba yake, Unoka. Na binti yake Ezinma alikuwa na sifa ya uhodari , mweye akili sana pia. Hata hivyo, Okwonkwo hakufurahia, maana alikuwa msichana!

Posted On Monday, 11 March 2013 07:51

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika chuo kikuu cha Dar es Salaam ukumbi wa Nkurumah.

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini waliojumuika katika sherehe za kuadhimisha siku ya wamawake duniani iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Ukumbi wa Nkurumah.

Posted On Monday, 11 March 2013 03:25

SONY DSCWafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo maboksi ya sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kula, jozi za khanga na vitenge kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) iliyopo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni shemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Posted On Monday, 11 March 2013 02:19

Photo: Leo Nilishuka Uwanjani Kufundisha Soka Ya Watoto..
Na ukiwa uwanjani kama kocha kwenye timu yenye watoto wako, basi, lazima wajue, kuwa u-baba umeishia nyumbani. Usishangae ukifika uwanjani kuwasikia watoto wangu wakiita; " Kocha! Kocha!" Na ngumu kwa mzazi kwenye jukumu la ukocha ni pale unapomwambia mwanao akae benchi!

Posted On Sunday, 10 March 2013 20:43

Photo: Kambi Ya Kusoma Ya Kamanda Olle Na Wanafunzi Wenzake Imenikumbusha Maisha Ya Jeshini ( JKT)
Mimi nilishiriki Operesheni Kambarage- 90-91. Namba yangu ya jeshi iko kichwani; Z6212. 
Leo tuliwapikia wali na maharage. Nakumbuka JKT mlo huo ulikuwa wa kusubiriwa sana. Jeshini tulikuwa na kitu kinaitwa mustin. Tulikitumia kwa chakula na kunyewea maji na hata chai.
Hakika, maisha ya mwaka mmoja jeshini yalikuwa magumu mwanzoni, baadae wengi wetu tuliyafurahia pia. Uzuri wa jeshini kuna utaratibu ambao ni mwepesi kukariri. 
Haraka sana nilijifunza mambo matatu muhimu ili maisha yangu yasiwe magumu sana kambini; kutandika kitanda changu, kuvaa buti za jeshi zikiwa zimefungwa kamba ipasavyo, na kuhakikisha unajibu ' Ndio Afande' hata kwa jambo la kipuuzi unaloambiwa na afande wako. ( Tulipumzika kufikiri!) 
Na cha ziada kukumbuka ukishakuwa Service Man baada ya miezi sita? Ni kupiga saluti kwa wakubwa. Na kuepuka hilo, unapotembea na wenzako usipende kuwa mkono wa kulia, maana, aliye kulia ndiye anayetakiwa kupiga saluti!

Mimi nilishiriki Operesheni Kambarage- 90-91. Namba yangu ya jeshi iko kichwani; Z6212.
Leo tuliwapikia wali na maharage. Nakumbuka JKT mlo huo ulikuwa wa kusubiriwa sana. Jeshini tulikuwa na kitu kinaitwa mustin. Tulikitumia kwa chakula na kunyewea maji na hata chai.

Hakika, maisha ya mwaka mmoja jeshini yalikuwa magumu mwanzoni, baadae wengi wetu tuliyafurahia pia. Uzuri wa jeshini kuna utaratibu ambao ni mwepesi kukariri.

Haraka sana nilijifunza mambo matatu muhimu ili maisha yangu yasiwe magumu sana kambini; kutandika kitanda changu, kuvaa buti za jeshi zikiwa zimefungwa kamba ipasavyo, na kuhakikisha unajibu ' Ndio Afande' hata kwa jambo la kipuuzi unaloambiwa na afande wako. ( Tulipumzika kufikiri!)

Posted On Sunday, 10 March 2013 20:37

1 a245f

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) 

ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.

Posted On Sunday, 10 March 2013 16:49

Photo: Nilipowachekesha Makamanda Na Kisa Cha Hesabu Cha Njau Na Kalumekenge...!
Ndugu zangu,
KUNA kisa cha hakimu aliyepata tabu sana katika kuthibitisha ukweli wa urefu wa mtuhumiwa wa wizi. Mashahidi walikuwa wawili; Njau na Kalumekenge.
Wote wawili, Njau na Kalumekenge, walimwona mtuhumiwa akivunja mlango wa nyumba kabla ya kuingia ndani na kuiba. Utata wa ushahidi wao ni kuwa; shahidi Njau alitamka kwa kujiamini mahakamani kuwa mwizi alikuwa mfupi. 
Na shahidi Kalumekenge naye aliongea kwa kujiamini kuwa mwizi alikuwa mrefu. Huu ni ushahidi wenye utata uliopelekea Bwana Hakimu aumize kichwa kabla hajapata njia ya kutatua utata huo.
Hatimaye hakimu akapata njia ya kufahamu urefu halisi wa mtuhumiwa wa wizi. Ndio, hakimu alibaini, kuwa kwa vile shahidi Njau ni mrefu, yeye alimwona mwizi kuwa ni mfupi. Na kwa vile shahidi Kalumekenge ni mfupi, kwake mwizi huyo alikuwa ni mrefu. 
Basi, Bwana Hakimu alichofanya ni kutafuta wastani wa urefu wa Njau na Kalumekenge ili kupata urefu halisi wa mtuhumiwa wa wizi ambaye Njau na Kalumekenge walimwona kwa wakati mmoja.
Kuna tunachojifunza katika utata na utatuzi wa ushahidi huo. Na hakika, kisa hiki nilichopata kukisikia zamani sana, kimenisaidia katika kuyatafakari yanayotokea katika jamii yetu kwa sasa. Hata kama sifanikiwi mara zote, lakini nimejifunza kutafuta ‘ wastani’ wa mambo kabla ya kukurupuka na kuyatolea maoni. 
Ndio, aliye juu anaweza kuyaona mambo kwa mtazamo wake, na aliye chini vivyo hivyo. Kwamba wanadamu tunayoyaona, tunayaona kwa mitazamo tofauti. Vivyo hivyo kwa tunayoyasikia na kuyaangalia. Kwamba wanadamu tuna hulka ya kusikia tunachotaka kusikia, na kuona tunachotaka kuona. 
Na mjinga asipojua kuwa yeye ni mjinga unafanyaje? 
Maggid,
Iringa.

Ndugu zangu,

KUNA kisa cha hakimu aliyepata tabu sana katika kuthibitisha ukweli wa urefu wa mtuhumiwa wa wizi. Mashahidi walikuwa wawili; Njau na Kalumekenge.

Wote wawili, Njau na Kalumekenge, walimwona mtuhumiwa akivunja mlango wa nyumba kabla ya kuingia ndani na kuiba. Utata wa ushahidi wao ni kuwa; shahidi Njau alitamka kwa kujiamini mahakamani kuwa mwizi alikuwa mfupi.

Na shahidi Kalumekenge naye aliongea kwa kujiamini kuwa mwizi alikuwa mrefu. Huu ni ushahidi wenye utata uliopelekea Bwana Hakimu aumize kichwa kabla hajapata njia ya kutatua utata huo.

Posted On Sunday, 10 March 2013 16:05

Photo

Leo nilimkuta Kamanda wangu Olle na wenzake watatu wakiwa wanakokotoa hesabu kujiandaa na mitihani yao ya Form Four mwaka huu. Wenzake anasoma nao darasa moja. Wamepiga kambi nyumbani kwetu kuanzia jana mpaka leo Jumapili wakipiga kitabu. Ukweli mimi nilipata ' D' ya hesabu Form Four. Sikuwa mzuri kwenye hesabu. Shetani wa hesabu alinikaa kichwani, na mpaka hii leo hajaondoka! Basi, leo kazi yangu ilikuwa ni kuwapelekea maji vijana na kufanya kazi ya Nape Nnauye, kuwahamasisha!

Photo

Posted On Sunday, 10 March 2013 15:39

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi