We have 95 guests and no members online

Tokeo la picha la kuzimwa vituo vya tv kenya

Mkurugenzi Mkuu wa Royal Media Services inayomiliki Televisheni ya Citizen TV, Waruru Wachira, amelaani hatua iliyochukuliwa na serikali kufunga mawasiliano katika vituo vya runinga na kusema kuwa binafsi hakutaarifiwa lolote kuhusu hatua hiyo iliyokuja ghafla ambayo pia imeathiri kituo chake cha Citizen TV. Katika hatua hiyo iliyoamuliwa na serikali vituo kadhaa vimeathirika ikiwa ni pamoja na kituo cha Citizen TV, KTN News na NTV.

Posted On Tuesday, 30 January 2018 12:07

Tokeo la picha la nectaKatika matokeo yaliyotangazwa na Katibu mtendaji wa baraza la Taifa la mitihani NECTA Dkt. Charles Msonde ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.22 tofauti na mwaka 2016, ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 70.35 mwaka 2016 na sasa ni asilimia 77.57.

Posted On Tuesday, 30 January 2018 10:24

media

Rais wa Marekani Donald Trump amekua akikosolewa kuhusu agizo lake dhidi ya wakimbizi kutoka nchi 11

Posted On Tuesday, 30 January 2018 08:30


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh. trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine kutoka Global Fund.

Posted On Tuesday, 30 January 2018 08:10

Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) ukiendelea kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 

Posted On Tuesday, 30 January 2018 08:07

Image result for Kassim Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Posted On Tuesday, 30 January 2018 08:03

Kwa mara ya kwanza tangu kurejea nchini Tanzania, balozi mteule Dkt Wilbroad Slaa amekutana na kufanya mazungumzo na rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao na Rais, Dkt Slaa amesema ameamua kukubali kufanya kazi na Rais baada ya kuridhika na kazi kubwa inayofanywa na Rais kwa wananchi.

Posted On Monday, 29 January 2018 13:04

Tokeo la picha la fire break in langata nairobi

Watu wanne wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya moto uliotokea usiku wa kuamkia leo January 29 katika mtaa wa Kijiji eneo la Langata-Nairobi, huku wengine wakiripotiwa kukesha baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa moto.

Kwa mujibu wa Maafisa wa serikali nchini humo, nyumba 6,000 makazi ya watu karibu 14,000 ziliharibiwa na moto huo.

Posted On Monday, 29 January 2018 12:06

Picha inayohusiana

Waziri wa mifugo na uvuvu Luhaga Mpina amesema uvuvi haramu ni moja kati ya majanga yanayomaliza rasilimali za wananchi ambazo zingetumika kufanya shughuli nyingine kama uwasomesha watoto.

Posted On Monday, 29 January 2018 04:50

Meli iliyokuwa na manusura (L) na meli ya uokozi katika bahari ya Pacific. Januari. 28, 2018.

Kikosi cha anga cha New Zealand kimewagundua Jumla ya watu sita akiwemo mtoto mmoja, waliokutwa wakiwa hawajitambui baada ya kuelea kwenye maji zaidi ya wiki moja katika boti ndogo ya mbao katika bahari ya Pacific.

Posted On Sunday, 28 January 2018 22:03

Tokeo la picha la RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA JAJI KISANGA

Tokeo la picha la RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA JAJI KISANGA

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Bi.Mama Janeth Magufuli, wameyaongoza mamia ya waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Jaji mstaafu Robert Kisanga ambaye alifariki Dunia mwezi January 23 mwaka huu.

Posted On Sunday, 28 January 2018 16:08

Picha inayohusiana

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewasimamisha kazi Afisa mifugo wa wilaya ya karatu, mtendaji wa kijiji na Afisa mifugo wa kijiji. Gambo amechukua hatua hiyo baada ya watendaji hao kushindwa kusimamia vizuri zoezi kupiga chapa mifugo ambalo pia ni la kitaifa, na kuagiza katibu tawala wa mkoa kuwaandikia barua ya kuwaonya mkurugenzi na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu

Posted On Sunday, 28 January 2018 15:34
Page 6 of 1653

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart