We have 138 guests and no members online

Vya Krismas Vimepita, Wengine Tumerudi Kwenye Ugali Na Mlenda Wetu!

Posted On Friday, 28 December 2012 08:38 Written by M Mjengwa
Rate this item
(0 votes)
Vya Krismas Vimepita, Wengine Tumerudi Kwenye Ugali Na Mlenda Wetu!

Ndugu zangu,
Marehemu bibi yangu mzaa baba, Binti Ngondya Wa Senjonjo wa Nyeregete , Mbarali, yeye haikupita wiki bila kupika ugali na mlenda.

Na marehemu bibi yangu mzaa mama, Binti Muhando Mwaruka wa Mzenga, Kisarawe, naye pia haikupita wiki bila kupika 'pombo'- ni mlenda huo huo kwa ugali. Tuliokuwa wajukuu tulifaidi kweli.

Na hakika, hivyo ndivyo vyakula vya asili vilivyotukuza. Nikiwa hapa Iringa, mara moja moja huenda kwenye mgahawa wa dada Hanifa, hapo huwa naweka oda mapema; ya ugali na na mlenda, pembeni kuwe na tembele la chukuchuku lililochanganywa kwa nyanya na kitunguu maji.

Hapo pichani ni jana mchana, imekosekana pilipili shamba, na ilibidi waifuate sokoni ili ikamilishe ladha.

 Ijumaa Kareem kwenu nyote!

Maggid,
Iringa.

Read more http://www.mjengwablog.com/2012/12/vya-krismas-vimepita-wengine-tumerudi.html

Read 1798 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji