We have 258 guests and no members online

Oh! Oh! Akina Malima Bado Wanaandamwa Na Mikasa Yenye Kuhusisha Magari...!

Posted On Thursday, 18 May 2017 07:20 Written by
Rate this item
(0 votes)

- Malima Baba naye alipata kuingia matatani kuhusiana na magari baada ya kutoka madarakani...

Ndugu zangu,

Juzi hapa aliyepata kuwa Waziri wa Serikali mwenye dhamana ya hazina, Adam Malima, aliingia matatani na dola kwenye yenye kuhusiana na parking ya gari.

Katika pekuapekua yangu, nimeona kwenye maktaba yangu, kuwa hata baba yake Adam Malima, naye alipata kuingia matatani na dola kwenye yenye kuhusiana na magari.

Gazeti la Daily News la Juni 7, 1995 liliripoti, kuwa aliyekuwa Waziri wa Fedha na Viwanda, Profesa Kighoma Ali Malima alijipa haki ya kukwepa kodi kwa kununua magari mawili, mwaka 1993; Mercedes Benz na Audi na kulipa shilingi milioni moja tu, hivyo alitakiwa kulipa shilingi milioni tano zaidi.

Na kwenye Daily News la Juni 12, 1995, Profesa Malima aliripotiwa kuahidi kulipa mara moja, deni la kodi analodaiwa na Serikali, shilingi milioni tano na laki mbili.

Yumkini, hata mara hii, Malima mwana, Adam Malima, kuna malipo atatakiwa kuyalipa kuhusiana na parking ile ya gari lake!

Maggid.

Read 105 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi