We have 265 guests and no members online

Tukumbushane: Siku Nyerere Alipocheka Sana Ikulu!

Posted On Friday, 19 May 2017 11:50 Written by
Rate this item
(0 votes)

Picha ya Maggid Mjengwa

Picha ya Maggid MjengwaInasimuliwa, kuwa katika siku za mwanzo za kukaa kwake Ikulu, Julius Nyerere alijulishwa kuwa angekuja Balozi mpya wa Swaziland kuwasilisha nyaraka zake....

Ikafika siku, mara Julius Nyerere akamuona Mheshimiwa Balozi anaingia akiwa ametinga na vazi la jadi la Waswazi. Mkononi kashika bakora pia. Kwa macho ya Nyerere , alimwona Mheshimiwa kama mtu aliyeingia Ikulu nusu uchi. Nyerere akabanwa na kicheko. Alikivumilia.

Mgeni alipoondoka , Nyerere akawageukia wasaidizi wake na kuangua kicheko cha nguvu hadi akashikilia mbavu zake. Alisema;

"Jamani ee, mbona hamkuniambia mapema kuwa Balozi angeingia Ikulu kwa staili ile?" Nyerere akaendelea kucheka, na wasaidizi wake nao wakaangua kicheko. Wote wakacheka sana.

Masikini, Mheshimiwa Balozi yule wa Swaziland hajapata kujulishwa juu ya kicheko alichokiacha nyuma, pale Ikulu ya Magogoni!

Maggid,

Read 211 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi