We have 54 guests and no members online

Siku Ile Ziliponifikia Habari Za Kifo Cha Daud Mwangosi..

Posted On Monday, 04 September 2017 06:38 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Image may contain: 3 people, child and outdoor

Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting, shoes, child, shorts and outdoor

 

Ndugu zangu,

Naikumbuka vema alasiri ile ya Septemba 2 miaka mitano iliyopita. Jumamosi ile ilionekana ni siku ya kawaida Iringa.

Nakumbuka nilipita Soko Kuu asubuhi ya siku ya tukio. Nilishangaa kumwona kijana aitwaye Majeki akiwa mjini na si Mufindi.

Majeki alikuwa mkereketwa na mpiga debe mahiri wa Chadema.

Majeki akaniambia, huko leo siendi naona hali si nzuri.

Alasiri majira ya saa tisa nikawa na vijana wangu na wenzao kuwafundisha soka kwenye kiwanja cha shule yao. Ni kama inayoonekana kwenye picha ya tatu.

Katikati ya kufundisha soka, ikaita simu yangu. Niliangalia alikuwa Francis Godwin, mwandishi na bloga mashuhuri.

" Mwangosi ameuawa."

Francis hakuwa na maelezo zaidi ya kuniambia ni Mufindi kwenye mkutano wa Chadema.

Nikawajulisha vijana waliokuwa uwanjani kuwa kuna jambo kubwa la huzuni limetokea. Tukatishe mazoezi nifuatilie.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa mara ile nilipopokea taarifa hiyo. Kuanzia hapo nikaanza kuwasiliana na wanafamilia wenzangu wa habari kujua zaidi.

Picha ya pili ni mtoto wa Daudi Mwangosi. Hii ni moja ya picha zenye kunigusa nilizopata kupiga. Mtoto wa marehemu Daud Mwangosi anaonekana akimkumbatia kwa uchungu Dr . Wilbroad Slaa usiku wa Septemba 3, 2013.

Ilikuwa nyumbani kwa marehemu Mwangosi, Mtwivila, Iringa. Nilifika nyumbani hapo usiku huo na kuwakuta watu kadhaa wakiwa kwenye viti nje ya nyumba. Mmojawapo alikuwa Dr Slaa.

Mara akaja mtoto wa kiume wa Daud Mwangosi. Nakumbuka alivyomkubatia Dr Slaa kwa uchungu na kutokwa machozi.

Tuliokaa mahali hapo tulikumbwa na huzuni kuu. Kwenye hali hiyo pichani, anaonekana Mzee Arcado Ntagazwa, Waziri wa zamani kwenye Serikali ya Julius Nyerere.

Jana ilitimu miaka mitano tangu Daud Mwangosi atutoke kwa kuawa kinyama.

Daud ameacha mke na watoto wanne, wa mwisho alikuwa na miaka miwili tu wakati wa kifo chake.

Maggid,

Iringa.

Read 44 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi