We have 194 guests and no members online

Marekani yatishia kuishambulia kijeshi Korea Kaskazini

Posted On Monday, 04 September 2017 06:57 Written by
Rate this item
(0 votes)

media

Rais wa Marekani Donald Trump.

Siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la hidrojeni, Rais wa Marekani Donald Trump amelaani vitendo ambavyo ni "vibaya mno na hatari kwa Marekani".

Siku ya Jumapili rais wa Marekani aliitisha timu yake ya usalama wa taifa ili kujiandaa kwa vikwazo vipya dhidi ya serikali ya Pyongyang. Waziri wa Marekani wa Ulinzi James Mattis alithibitisha kwamba nchi yake iko tayari "kujibu kijeshi". Marekani iko tayari kutumia uwezo wake wa nyuklia ikiwa Korea ya Kaskazini itaendelea kuitishia au kuwatishia washirika wake, ikulu ya White House ilitangaza siku ya Jumapili. Ikiwa mvutano kati ya nchi hizo mbili unaonekana kuongezeka kwa miezi kadhaa, jaribio hili jipya la Korea Kaskazini linaitia wasiwasi Marekani.

Rais Donald Trump alizungumza kwenye simu na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, ikulu ya White House ilisema katika taarifa ya siku ya Jumapili usiku kuamkia Jumatatu hii. "Rais Trump alithibitisha ahadi ya Marekani kutetea nchi yetu, maeneo yetu na washirika wetu kwa kutumia upeo kamili wa uwezo wa kidiplomasia, wa kawaida na wa nyuklia tunao," ilisema taarifa ya ofisi ya rais wa Marekani.

"Sera ya kuvumiliana kwa serikali ya Kim Jung-Un imeshindwa. Korea ya Kaskazini ni taifa lenye la kijnga ambalo limekuwa tishio kubwa na chanzo cha matatizo kwa China, ambayo inajaribu kusaidia lakini kwa mafanikio madogo. "

Hiyo ndivyo Rais wa Marekani alivyochapisha mapema siku ya Jumapili kwenye mitandao ya kijamii, akiomba kutumia njia mpya, bila hata hivyo ni njia gani itakayotumiwa. siku ya Jumapili asubuhi mwishoni baada ya kushiriki misa, Donald Trump alijibu swali la lililoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu uwezekano wa kushambulia Korea ya Kaskazini: "Tutaangalia vizuri," Donald Trump alisema, kabla ya kuondoka, amesema mwandishi wa RFI mjini New York, Grégoire Pourtier.

Donald Trump alikutana na timu yake ya usalama wa taifa siku ya Jumapili ili kujadili vikwazo vipya dhidi ya Korea ya Kaskazini, pamoja na vkwazo ambavyo tayari vimewekwa na Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Fedha wa Marekani amesema kuwa "wale wanaofanya biashara na Pyongyang hawataweza kufanya biasharahiyo na Wamarekani." Vikwazo hivi vinapaswa kupitishwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Wawili hawa wanadai vikwazo vikali zaidi vya Umoja wa Ulaya dhidi ya serikali ya Pyongyang.

Ikiwa Marekani inataka kufafanua kwamba inakusudia kufanya kazi na washirika wake pamoja na China, mfululizo huu mpya wa vikwazo unaweza kueleweka vibaya na serikali ya Beijing, moja ya nchi chache amnbazo bado zinafanya biashara na Korea Kaskazini na hasa ni nchi ambayo inapokea mauzo ya nje ya Korea ya Kaskazini kwa asilimia 90.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litajadili tena suala hili kwa haraka leo Jumatatu. Mwenendo wa Pyongyang utajadiliwa na kulaaniwa tu kama kawaida. Lakini sasa jumuiya ya kimataifa inapaswa pia kutoa msimamo wake dhidi ya matangazo ya vita ya Marekani.

Chanzo:RFI

Read 177 times

Add comment

Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu