We have 57 guests and no members online

Afrika Hapo Zamani: Mitindo Ilikuja, Ikaondoka, Ikaja Mipya, Ikaondoka..!

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:18 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: 5 people, people smiling, people standingNdugu zangu, 

Sisi tuliokua tukiiona bendera ya TANU ikipepea tumeona mengi pia.

Nimesoma kwenye Daily News leo, kuwa Tamasha La Utamaduni Afrika Mashariki linaanza Kampala Alhamisi hii.

Hakika ningependa kuwepo Kampala kushuhudia utamaduni wa A.Mashariki ni upi kwa sasa.

Na hivi, utamaduni ni nini hasa? 
Unahusu mengi, lugha, chakula na hata mavazi.

Nakumbuka utotoni kuna jambo lilinihuzunisha sana wakati nikikua pale Ilala miaka ya 70 katikati.

Kulikuwa na marufuku ya wanawake kuvaa nguo fupi.

Nakumbuka msichana yule aliyekimbilia nyumbani kwetu na kuomba hifadhi asije akachapwa bakora na mgambo wa TANU, kwa vile tu kavaa sketi fupi.

Nakumbuka nilipokuwa nikicheza mtaani na wenzangu nilihuzunika sana kuwaona akina mama wakitembea kwa mashaka. Ilikuwa kawaida kuwaona wanawake wakikimbilia vichochoroni kuwakwepa mgambo wa TANU.

Kama vile waliambizana, wanawake wakaja na mtindo wa kuvaa gauni ndefu maarufu ikiitwa max. Chini kulia gauni la max lilikatwa.
Ilikuwa ni kama protest ya unyanyasaji waliofanyiwa.

Kiukweli gauni la max halikuwapendeza wanawake. Bila shaka, hao hao wanaume waliopiga marufuku ya sketi fupi kuna waliotamani wanawake warejee kwenye kuvaa sketi fupi.

Naam, mitindo hii inakuja na kuondoka, ya miaka ya 70 tunaiona ikirudi tena. 

Si ndio utamaduni wenyewe...!

Zilipendwa...

‘Le Bûcheron’ ... https://www.youtube.com/watch?v=LvDn11AEoas

Picha Ya Maktaba: mjengwablog.com

Read 60 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi