We have 168 guests and no members online

WANANCHI WA MKOA WA DAR WAFURIKA KWA WINGI KUPIMA AFYA ZAO BURE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

Posted On Thursday, 07 September 2017 05:27 Written by
Rate this item
(0 votes)

Zoezi la Upimaji wa Afya Bure limeanza leo kwenye Viwanja vya  Mnazi Mmoja  huku baadhi ya Wananchi wakitoka Mikoani kuja Dar es Salaam kufuata huduma na wengine wakiwahi kwenye Viwanja hivyo tokea  saa 10 Alfajiri.

RC Makonda  amesema kampeni hiyo ina malengo matatu ambayo ni Kujengea Wananchi utaratibu wa kupima Afya zao Mara kwa mara hata kama hawaumwi.

Kusaidia Wananchi Wanyonge wanaotamani kupima Afya lakini hawana Uwezo wa Fedha kupata fursa ya kupima Afya.

Kupunguza vifo   vitokanavyo na watu kutokujua historia ya Magonjwa yao hadi pale wanapougua.

Aidha  Makonda  amesema kila Mwananchi atakaefika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja atapimwa na kupatiwa Matibabu Bure.

Amesema  Wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa utaratibu wa kupima Afya Mara kwa Mara na pindi wanapozidiwa na kufikishwa Hospital Ugonjwa unakuwa tayari umekuwa sugu hivyo kupoteza maisha.

Amewapongeza  Madaktari na Wauguzi kutoka  Hospital za Umma, Jeshi na zile za Binafsi kwa kujitolea kumuunga mkono katika Kampeni hiyo.

Zoezi la upimaji Afya Bure litaendelea Kwenye Viwanja vya Mnazu Mmoja kwa muda wa siku tano kuanzia Asubuhi hadi Jioni.

Read 60 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi