We have 53 guests and no members online

" Ewe, Simbachawene, Umeondoka Kwa Heshima "

Posted On Sunday, 10 September 2017 16:31 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: 1 person, standingNdugu zangu,

Nimemsikitikia sana ndugu yangu, Comrade George Simbachawene.

Kwa kusoma Daily News la Septemba 7, inaonyesha dhahiri kuwa akiwa amepanda kuwa Waziri Kamili wa Nishati na Madini, ndani ya siku saba ndipo makosa yanayomtaja kwenye ripoti ya Bunge yalipofanyika. 

Ni kama vile mchezaji anapoanza kucheza mechi uwanjani. Pasi za awali hutokea kuwa hazina macho. Ni mpaka pale atulie, baada ya dakika za awali kupita.

Na kubwa, makosa ya Simbachawene hayaonekani kabisa kuwa aliyafanya ili yamnufaishe yeye binafsi, tofauti na mwenzake Injinia Ngonyani ambaye, baada ya kutengeneza ushawishi kwa kampuni ya Tanzanite One kununua hisa , naye akaja kuwa Mjumbe wa Bodi wa kampuni hiyo hiyo. George Simbachawene yeye alisaini kuhamishwa kwa hisa bila kufuata taratibu. Duniani hakuna asiyefanya makosa, na ukizingatoa alikuwa mpya kama waziri Kamili, hilo lingeweza kutarajiwa. Amewajibika kwa vile limetokea katika wakati wake. Ameondoka kwa heshima ili kupisha uchunguzi.

Kwangu binafsi Simbachawene ni kiongozi mwenye kujali yaliyo na maslahi kwa wengi. Ni mchapakazi, mtu asiyependa urasimu kwa maana ya kuchelewesha mambo. 

Nilipata kuwa na kazi yenye kuhusisha TAMISEMI, nilishuhudia jinsi anavyofanyia kazi yenye maslahi kwa umma, wakati wowote ule, iwe mchana au usiku.

Nimemsikiliza mara kadhaa George Simbachawene akijenga hoja ndani ya Bunge. Binafsi, kwa kupima hoja zake, naamini kuwa Simbachawene mara zote anasimamia upande wa wengi. 

Simbachawene anayajua vema mahitaji ya wananchi wa vijijini , kule Kibakwe na kwengineko Tanzania. 

Wahenga walisema; kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. 
Ni imani yangu, kuwa Simbachawene ataendelea kuchapa kazi, na kwamba siku moja tutamwona akirudi tena kwenye nafasi ya juu kuwatumikia wananchi wengi zaidi ya wale wa jimboni kwake Kibakwe.

Maggid Mjengwa,

Dar es Salaam.

Read 53 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi