We have 71 guests and no members online

Olle Amenisimulia Habari Za Arabuni Alikofika

Posted On Sunday, 10 September 2017 17:14 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: one or more people, sky and outdoorNdugu zangu,

Kijana wetu Olle amefika salama kwenye mji wa Amman, Jordan.

Ananisimulia, kuwa Amaan ni mji mzuri na wenyeji ni wakarimu sana.

Pale airport, kutokana na mwonekano wa Olle, afisa wa Uhamiaji akamwambia Olle;
" Alaa, kwa hiyo wewe mama Msweden na baba yako Mwarabu."

Olle akamjibu, kuwa baba ni Mtanzania.
Afisa yule wa Uhamiaji akasema, anyway, najua Tanzania kuna Waarabu pia!

Olle anasimulia, kuwa Ijumaa kama leo shughuli zote ikiwamo maduka yanafungwa. Jioni kama hapo pichani ndipo maduka yanafunguliwa.

Kwamba ikifika muda wa kuswali unaweza kuwaona hapa na pale watu wakiacha shughuli zao na kuswali hata kando ya mitaa, kisha wanaendelea shughuli zao. Ni kama unavyowaona watu wawili wakiswali eneo la wazi pichani.

Ijumaa na Jumamosi ni siku za mapumziko. Jumapili ni Jumatatu yao.

Olle anasema wenyeji mitaani wanamchanganya na Waarabu, hivyo kila anakokwenda wanamsemesha Kiarabu!

Ananisimulia Olle.

Maggid.

 

Read 49 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi