We have 73 guests and no members online

Hii Ndio Shule Ya Jimboni Kwa Injinia Ngonyani Aliyejiuzuru Uwaziri...

Posted On Sunday, 10 September 2017 19:13 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: outdoor

Image may contain: one or more people, outdoor and nature

 

Ndugu zangu,

Mtakumbuka picha hizi, ni pale nilipofika Mputa, Namtumbo. Hii ni Shule ya Msingi Upendo, iko Namtumbo, jimbo la Mbunge Injinia Edwin Ngonyani ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano aliyejiuzuru juzi hapa baada ya kutajwa kwenye ripoti ya Kamati ya Bunge.

Kwenye shule hiyo baadhi ya watoto wanasomea madarasa ambayo asubuhi ni wanafunzi na jioni wanashinda mbuzi.

Tuhuma dhidi ya Injinia Ngonyani kama ilivyoripotiwa na Daily News Septemba 7 , ni pamoja na Injinia Ngonyani , akiwa Afisa wa ngazi ya juu Serikalini kuishauri Serikali kuaacha kuzirudisha( Reclaim au kuzinunua ( Buy) hisa za kampuni ya Tanzanite One zilipowekwa sokoni. Badala yake, Injinia Ngonyani alishiriki kwenye kuwezesha ( facilitation) kampuni ya Sky Associate Limited kununua hisa hizo .

Baadae, Injinia Ngonyani akateuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi kwenye kampuni ya Sky Associate Limited!

Na huwezi kuacha kucheka ukiangalia video yenye kumwonyesha Injinia aliyeinjia kampuni binafsi kununua hisa na yeye kuwa mjumbe wa Bodi akipiga magoti kuwashukuru wananchi wa jimbo lake, bila shaka kwa kumwezesha yote hayo!

https://www.youtube.com/watch?v=TkRKOcDLO34

Nchi ya Kusadikika haijawahi kukumbwa na ukame wa maajabu!

Maggid.

Read 59 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu