We have 72 guests and no members online

Neno La Leo: Afrika Bara Gumu...

Posted On Sunday, 10 September 2017 19:22 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: people sitting and indoorNdugu zangu, 

Wala si baragumu, ni Bara Gumu. Nasoma juzuu ya Martin Meridith, The State Of Africa.

Ukurasa wa 199 kuna mahali yanazungumziwa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1966 kule Nigeria.

Ni mapinduzi yaliyofagilia mbali viongozi mafisadi na utawala uliopoteza heshima na uhalali kwa umma.

Wananchi walishangilia kama wendawazimu. Viongozi wa mapinduzi yale wakatajwa kuwa ni mashujaa.

Wanasiasa wakasinyaa machoni mwa watu, ni kwa usiku mmoja.

Madhambi na uhalifu wa wanasiasa wa utawala wa nyuma vikaanza kuanikwa hadharani. Magazeti, redio, watumishi wa umma na wasomi waliokaa kimya muda wote wakaanza kusema. Wanasiasa walivuliwa nguo kwa ufisadi wao. Umma ukaanza kuwatambua kwa majina mafisadi wao. Umma ukashuhudia mafisadi wakihukumiwa na mali zao kutaifishwa.

Mwandishi yule mahiri Chinua Achebe mwaka ule wa 1966 ndipo akaandika kitabu chake; A Man Of The People.

Ukimsoma Chinua Achebe, kwenye A Man Of The People utaelewa ninachosema, kuwa Afrika ni Bara Gumu, si baragumu.

Ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa.

 

Read 52 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu