We have 246 guests and no members online

Busara Za Wanazuoni: Alichoandika Profesa Chachage...

Posted On Monday, 11 September 2017 06:06 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: 1 person, sitting


Ndugu zangu, 

Mmoja wa wanazuoni mahiri kupata kutokea kwenye nchi hii ni Profesa Sethy Chachage. Nilipata bahati ya kukutana na kuongea nae.
Lakini, leo nitaweka hapa moja ya andiko lake lililojaa busara;

"Profesa Chachage anaandika….

“ Haitoshi kabisa kulifahamu jambo. Kuambiwa ni habari tu, unaambiwa na unafahamu, unajua kwamba tukio fulani limetokea.

Gumu zaidi ni kuelewa mantiki ya hilo jambo, na hata baada ya kufikiria na kulifahamu, ugumu mwingine huja pale ambapo inabidi ulieleze lieleweke na maelezo yakajitosheleza yenyewe na kumfanya kila asikilizaye kuridhika kwamba jambo linaeleweka. 

Haitoshi wewe kulielewa, bali na wewe kulielezea na mtu mwingine akaelewa. Hapa umuhimu wa kufikiria unachukua nafasi ya pekee. 

Hii ndio maana ya mawasiliano.” – Profesa Chachage Seithy Chachage ( Makuadi Wa Soko Hurua, ukurasa 117)

Naam, ndugu yetu Chachage anatutaka tufikiri kwa bidii. Na kimsingi anachoandika Chachage kinahusu pia dhana nzima ya maarifa na namna tunavyoyapata.

Maana, ukiweza kuelewa ulichojifunza na ukaweza kumwelezea mtu mwingine akakuelewa, basi, kwako hayo uliyoyaelezea yakaeleweka ndio maarifa yabisi uliyoyapata.

Maggid Mjengwa.

Whatsapp: 0688 37 36 52

Read 51 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu