We have 48 guests and no members online

WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10

Posted On Tuesday, 12 September 2017 04:32 Written by
Rate this item
(0 votes)

IMGL3619

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi msaada wa sh. milioni 10 kwa Meneja wa Tbc 2. Bw. Godfrey Nago ili kumsaidia Msanii wa muziki wa dansi Bw. Ernest Masenga. Bw. Nago amepokea kwa niaba ya msanii huyo. Kushoto ni mjomba wa msanii huyo Bw. Kanuti Mloka. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Agosti 11/2017 katika ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa msaada wa sh. milioni 10 ili kumuwezesha Bw. Ernest Masenga kutatua changamoto zinazomkabili.

Bw. Masenga alikuwa msanii wa muziki wa dansi ambaye sasa anasumbuliwa na maradhi ya miguu. Pia makazi anayoishi si salama yanahitaji kukarabatiwa.

Waziri Mkuu ametoa msaada huo leo (Jumatatu, Septemba 11, 2017) katika makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar Es Salaam.

Ametoa msaada huo baada ya kuguswa na hali ya maisha ya msanii huyo aliyemuona kupitia kipindi maalumu kilichoonyeshwa na TBC Sempemba, 5, 2017. Kipindi hicho kiliongozwa na Bw. Godfrey Nago.

“Nawaomba Watanzania wenzangu tumsaidie mwezetu ili aweze kuishi vizuri kwa sababu sanaa yake imesaidia katika kuelimisha na kuburudisha umma .”

Kwa upande wake Bw. Nago ambaye amepokea msaada huo kwa niaba ya Bw. Masenga amesema atahakikisha anasimamia vizuri fedha hizo ili zitumike kama ilivyokusudiwa.

Pia Bw. Nago amesema anamshukuru Waziri Mkuu kwa kuwaunga mkono na kutoa msaada huo kwa sababu ameonesha kwamba Serikali inawajali wananchi wake na TBC itaendelea kuwaomba wadau mbalimbali wajitokeze na kumsaidia msanii huyo.

Naye Mjomba wa msanii huyo Bw. Kanuti Mloka ambaye ameiwakilisha familia amemshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo kwa kuwa familia imeshindwa kumsaidia Bw. Masenga kutokana hali duni ya maisha waliyonayo.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 

JUMATATU, SEPTEMBA 11, 2017.

Read 55 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi