We have 171 guests and no members online

BENKI YA PTA YABADILI JINA, SASA KUITWA BENKI YA TDB

Posted On Wednesday, 01 November 2017 06:15 Written by
Rate this item
(0 votes)

Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika, maarufu kama PTA imebadili jina rasmi la biashara na kuanzia sasa itatumia jina la Benki ya Biashara na Maendeleo (Trade and Development Bank) yaani TDB.

Mkurugenzi wa Maswala ya Ndani na Uhusiano wa Wawekezaji wa benki ya TDB, Mary Kamari akizungumza kuhusu PTA kubadili jina kuwa TDB na akielezea mipango mbalimbali ambayo benki hiyo wanayo ili kuliwezesha baa la Afrika kupata maendeleo makubwa.

Akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya kuzindua jina jipya, Mkurugenzi wa Maswala ya Ndani na Uhusiano wa Wawekezaji wa benki ya TDB, Mary Kamari alisema kubadili jina kumekuja baada ya miaka kadhaa ambapo ubora wa mali uliongezeka, upatikanaji wa faida, umepanda na ubunifu unatumika ipasavyo, vitu vilivyotokana na mageuzi kadhaa ya muundo mzima wa benki yanayolenga kuimarisha na kuifanya iwe ya kisasa zaidi.

“Tumeongeza kwa kaisi kikubwa uwezi wetu wa kutosheleza mahitaji ya bidhaa na huduma zatu, kup[itia mtandao imara tuliojenga ukijumuisha waliowekeza kwetu na wafadhili wetu. Wanahisa wetu wameongezeka kwa zaidi ya asilimia 50 katika miaka ya karibuni zikiwemo taasisi kadhaa mpya za uwekezaji na nchi wanachama,” alisema Kimari.

Alisema benki hiyo imejipanga kuendeleza utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye sekta zenye kupewa kipaumbele kama vile miundombinu, viwanda na biashara ya kilimo katika nchi 21 ambazo inafanya shughuli zake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

 Baadhi ya watu waliohudhuria hafla ya TPA kuabadili jina na kuwa TDB.

“Usanifu wa jina letu unaashiia kuwa tumeibuka na nguvu mpya na shamira mpya katika kutumia njia mbalimbali za ubunifu ili kuchangia kimalifu katika kuimarisha biashara, maendeleo na ushirikiano wa kikanda,” alisema Kimari na kuongeza.

“Katika miradi ya karibuni tumechochea kasi yetu na kutoa mikopo katika biashara, ujasiriamali na miundombinu na kuongeza mara tatu kwa fungu letu zima la mikopo katika miaka mitano iliyopita. Tumechangia kwa kaisi kikubwa katika ukuaji wa sasa wa uchumi na maendeleo ya miundombinu katika ukanda mzima.”

Alisema benki hiyo imetoa mikopo ili kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na mradi 711 wa Kawe, Dar unaoendeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Fibre Optic Backbone Project wa nchini Burunndi, miradi ya nishati endelevu ambayo inafanyika Kenya na Uganda na miradi ya viwanda vya simenti na chuma katika nchi ya Congo DRC, Djibouti, Zambia, Rwanda, Ethiopia na Zimbabwe.

Read 58 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart