We have 187 guests and no members online

RC DAR KUKUFUA MABASI 10 YA VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI

Posted On Wednesday, 01 November 2017 06:18 Written by
Rate this item
(0 votes)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Oktoba 31 amekabidhi mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach ili yafanyiwe matengenezo na kuwa ya kisasa.

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali.

RC Makonda amesema kuwa gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Coach kwa kujitolea kukarabati magari hayo bila kutumia pesa ya serikali.

Aidha Makonda amesema magari hayo yatafungwa vifaa vya kisasa ikiwemo kiyoyozi (AC), mfumo wa chaji ya simu kila kiti, runinga, radio, viti vya kisasa, vyoo vya ndani, bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.

RC Makonda amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu vyombo vya ulinzi na usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia wananchi na askari wajivunie kufanyakazi chini ya RC Makonda.

Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha ving’ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za ulinzi na usalama, magari ya wagonjwa ili kupunguza mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.

Katika hatua nyingine amewataka Wanasiasa kufanya Sasa za kistaarabu badala ya kutukana na kutoa lugha chafu kwa Serikali.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal Rajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James ambapo wote kwa pamoja wamempongeza RC Makonda.

Read 77 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart